Uchaguzi 2020 Lissu akamilisha ujazaji wa fomu za Urais Tanzania

Uchaguzi 2020 Lissu akamilisha ujazaji wa fomu za Urais Tanzania

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, amekamilisha hatua za mwisho za ujazaji fomu za uteuzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Leo Ijumaa tarehe 21 Agosti 2020, Lissu akiambatana na mgombea mwenza, Salum Mwalimu, wamefika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kisheria ya ujazaji wa fomu zao za kugombea.

Akizungumza baada ya kukamilisha hatua hiyo, Lissu amesema wamefika katika mahakama hiyo kula kiapo cha ujazaji wa fomu hizo.

“Mimi ni mteule wa CHADEMA kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Salum anagombea makamo wa rais, taratibu ya sheria ya uchaguzi baada ya kutafuta wadhamini.”

“Kinachofuata ule kiapo mbele ya Jaji Mkuu, ukija kula kiapo kama sehemu ya kukamilisha ujazaji fomu ya uteuzi wa kugombea kinachofuata ni safari ya Dodoma kuwasiliha fomu za uteuzi siku ya Jumanne,” amesema Lissu.

Uteuzi wa wagombea urais itafanyika tarehe 25 Agosti 2020 Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma.

Baada ya uteuzi wa wagombea, kampeni za uchaguzi huo zitafanyika kuanzia tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.
Huyu ndiye mfano Daudi, aliyepitia uvuli wa mauti mikononi mwa Sauli kutokana simulizi zilizopo ndani ya maandiko matakatifu, na Mola akamlinda.
 
Mungu Baba wa Mbinguni aliyemponya mja wake kwenye tukio baya kabisa la kushambuliwa kwa risasi, tunakuomba tena na tena Mungu Baba wa Mbinguni ukawe na mja wako huyu katika safari yake ya kutafuta kibali machoni pako cha kuwatumikia wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. AMINA

Pamoja sana.

Nami amuombea kwa Mungu kuwa huyu mtu aliyetamka wazi kuwa alikusudia kumuua Tundu Lissu kwa kutuma kikundi kwenda kumpiga risasi AFE KIFO CHA AIBU WAKATI WA KAMPENI. MUNGU TUONDOLEE MTU HUYU MWENYE ROHO OVU MUUWAJI HATUMTAKI. NAJUA MUNGU UNASIKILIZA MAOMBI HAYA NA UTAYAJIBU KWA HARAKA. AMEN
 
Hivi nimakundi gani hasa yenye ushawishi ktk jamii yanayomuunga mkono Lissu.
Anaota kwenda ikulu kwa kura zipi hasa, maana idadi ya watu waliohamia ccm ndani ya miaka mitano si ya kubezwa.

Hamna watu wapiga kura wa upinzani waliohamia ccm zaidi ya viongozi wachache wapigania tumbo.
 
Congratulations Tundu Lissu...

Hakuna cha kukuzuia kaka Lissu....

Kila hatua, Bwana Mungu Yehova ameisafisha na kuongoza njia yako...
å Uponyaji wako
å Safari back home from Kenya & Belgian after 3 yrs of Magufuli's bullets healings
å Kuteuliwa na Chama chako
å Kupokea fomu ya uteuzi NEC
å Kutafuta wadhamini

Na Leo utakula kiapo bila shaka yoyote maana alipo Mungu muumba (siyo ile miungu yao), hakuna kinachoshindikana....

Kisha nenda hatua zinazofuata;
å Kurudisha fomu ya uteuzi wa kuuendea Urais wa nchi hii, NEC - Dodoma
å Anza kampeni rasmi
å Shinda uchaguzi
å Tangazwa na kuwa Rais Mteule
å Apishwa kuwa Rais wa nchi hii.
å Ondoa kinga za kutoshitakiwa za waliojiwekea wahalifu wote wa nchi hii ili waanze kuonja matokeo ya dhambi zao..

KARIBU SANA MH. RAIS TUNDU A.M. LISSU...!!

Wewe unajua kaka yako Lissu kisha sema uongo wa kufa mtu??! Eti, eti, eti... anahitaji malori baadaye ya kupeleka forms za wadhamini Dodoma. Ingawaje tume inahitaji 2300tu.
 
Kigogo hajielewi.

Huwa hapendi kukosolewa kama Jiwe.

Muda wote anajikuta yeye yupo sahihi
Hahaha huyu mwamba ni shujaa wa taifa. Katusaidia sana kututoa matongotongo watanzania. Wasiojulikana bila huyu wangetupoteza sana
 
LISSU ARUKA KIHUNZI CHA MAHAKAMA MBIO ZA URAIS TANZANIA

 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kipindi hiki kinatembea kifua mbele kwa ujasiri! Maana Mgombea Wetu ni Chadema kweli kweli, Wale waliokua wanasema chadema kimekufa nawashauri wajitoe tu Kwenye Uchaguzi wamuachie Lissu sababu yeye ndio anaekwenda kushinda Uchaguzi.
 
Mtaa wa saba wanafikiri tume ni yao..eti wamejifumgia wanatengeneza pingamizi la Lissu kuanza kampeni mapema...

Watu wasiojia sheria ni balaa...

Yale yale ya Ugaidi wa watu wawili miaka ile!!
 
Back
Top Bottom