REJESHO HURU
JF-Expert Member
- Mar 6, 2014
- 5,283
- 11,558
Wamuachie tu chiba arudi mtaani
Samaki huoza toka mkianiKama nchi tuna safari ndefu sana
Kesi imeisha hapaLissu: nilisema tune ya uchaguzi ni ya CCM inateuliwa na mwenyekiti wa CCM? NI KWELI
Shahidi: Ni kweli
Kivipi Amin Mashamba ameshaeleza ACP Shahid aliyefariki ni wa Singida na huyu ni wa Goba DarSijui kama mnaelewa, huyu siyo Mahamba mwenyewe, hili bomu litafumuka kesho
Wanaweza kulitegeu nje ya uwanja lisilete madharaSijui kama mnaelewa, huyu siyo Mahamba mwenyewe, hili bomu litafumuka kesho
Huyo atakuwa kagushi identity. Subiri tuKivipi Amin Mashamba ameshaeleza ACP Shahid aliyefariki ni wa Singida na huyu ni wa Goba Dar
Hapa kuna uwezekano WA mambo ya vyetí féki, n.kKivipi Amin Mashamba ameshaeleza ACP Shahid aliyefariki ni wa Singida na huyu ni wa Goba Dar
Aisee...View attachment 3648282
Leo Agosti 11, 2026 katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu anayeshitakiwa kwa kesi ya uhaini, ameendelea kumhoji shahidi wa 16, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP), Amini Mahamba.
Kesi hiyo inasikilizwa na majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.
Utata wa Ushahidi Mahakamani vs Maelezo ya Polisi
Lissu: rafiki habari yako? Umelala vizuri?
Shahidi; Nipo vizuri.
Lissu: Jana nilikupitisha kwenye ushaidi kwa jinsi ulivyoandika polisi. Naomba ujibu kwa sauti kama mpelelezi mbobevu na askari anaweza kuongoza gwaride.
Jana ulieleza kwamba uliteuliwa kuwa OC CID wilaya ya Kyela anayewasimamia wapelelezi.
Shahidi: Ni kweli.
Lissu: waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo ya polisi.
Shahidi: hayapo.
Lissu; Ukasema kuwa ulipandishwa cheo na kuw ampelelezi RCO Ruvuma.
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yapo kwenye maelezo uliyoadika polisi.
Shahidi: Hayapo
Lissu: Leo tutakwenda vizuri.
Lissu: Kwenye ushaidi wako ukasema 2025 ukahamishiwa Dar es Slaam kwa ZCO mkoa unaosimamia wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke.
Waeleze waheshimiwa majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo uliyoandika polisi.
Shahidi: Hayapo.
Lissu: Mwaka 2025, ukateuliwa kuwa RCO Kinondoni
Mnajiandikia andikia tu halafu mnamshitaki mwenyekiti wa chama kwa uhaini.
Siku ya Tarehe 8 Aprili na Kielelezo D15
Lissu; sasa nataka tuzungumze ya Tarehe 8 April 2025. Kwenye ushaidi wako jana ulisema mnamo April 8 nikiwa ofisini kwangu nilipigiwa simu na mkuu wangu wa kazi, CP Ramadhani Kingai kwenda ofisi za polisi Dar es Salaam kufungua kesi ya uhaini inayomhusu mtuhumiwa Tundu Lissu. Waeleze majaji kama hayo maelezo yapo.
Shahidi; Yapo.
Lissu: Mpeni Exhibit D15
Katuga anasimama kumtaka Lissu kutotoa kauli za kuagiza badala yake aombe.
Lissu: Samahani majaji. (Anayasoma maelezo ya kielelezo, kisha anamuuliza shahidi)
Hayo maelezo yapo?
Shahidi: Yapo.
Lissu: Kuna jina la Lissu?
Shahidi: Yapo.
Lissu: Kwa kawaida ACP Mahamba una akili timamu?
Shahidi: Ndiyo
Lissu: Unajifanya mjanja sana lakini hauna kitu.
Shahidi; suala ni jalada kuwepo.
Lissu; Anasoma tena exhibit. Swali langu hayo maneno yapo? Kwenye ushaiidi sio kutoa kichwani mwako.
Shahidi: Hayapo.
Lissu: Ulipofika kwenye ofisi ya upelelezi kwa Bagyemu uliunda timu tatu za upellezi. Timu ya kwanza ilikuwa na (anawataja). Waeleze majaji hayo maelezo yapo kwenye ushahidi?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Umeeleza katika timu ya upelelezi, alikuwepo George Bagyemu...Waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo uliyoandika polisi,
Shahidi: hayapo
Lissu: Kuandika andika tu. Ulisema katika tumu uliyoita legal advisor ili mwonekano wa kutumia sheria.
Umesema kulikuwa na mwanasheria mwenye jina la Kibantu na mimi ni Mbatu anaweza kuwa Mnyaturu. Nilipomhoji shahidi namba 1 George Bagyemu alisemakulikuwa na Mwanasheria na wewe unasema kulikiwa na mwanasheria. Majaji wamwamini nani?
Shahidi: Hakukuwa na mwanasheria
Lissu: George Nagyemu ni liongo.
Lissu: Ulisema mlichukua kompyuta inayomilikiwa na (anamtaja) kwa saa mbili. Hayo maelezo yapo?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Shahidi George Bagyemu alisema hiyo video ya Jambo TV aliiangalia kutoja kwa Inspector Kaaya tena aliangalia vipande vipande. Wewe unasema mliangalia kwa saa mbili.
Katuga: Anamkosesha shahidi anaposema Bagyemu aliangalia kwa vipande. Hiyo ilikuwa tarehe 4 na yeye anazungumzia tarehe 8 ni vitu viwili tofauti.
Majaji wanajadiliana.
Lissu: waheshimiwa Majaji. Mawakili wa Serikali si watakuja kufanya re examination? Kwa nini waniulize sasa hivi? Si wana haki yabkuniuliza wakati wa re examination? Kwani kuongoea ndio mwisho?
Pili, mawakili wa serikali wako wanane wna haki ya kunipangia nini cha kuuliza?
Jaji Ndunguru; naomba tuendele, lakini tuzingatie...
Lissu: Narudia swali: majaji wafuate ushaidi wa nani?
Shahidi: Jayo ni matukio mawili tofauti, hiyo ilikiwa Aprili 4 aliingalia kwa vipande kabla mimi sijateuliwa na hayo yabpili tuliangalia kwa saa 2.
Lissu: Sawa, maelezo ya George Bagyemu yapo kwenye information ambayo nimeshitakiwa nayo nilikuyataka nimaoigwa chini. Lakini nibrekodi ya mahakama.
Katuga anaingilia, lakini Jaji Ndunguru, anamkatisha akisema asubiri kwanza shahidi aongee.
Lissu; ahsante majaji, kilichonileta mahakamani ni haya maelezo (anaonyesha hati ya mashitaka).
Shahidi: Mimi sina hayo maelezo ni kielelezo cha mahakama.
Lissu: Wewe hujui, acha nikujulishe. Hayo ni maelezo ya polisi ni maelezo mliyokusanya wenyewe.
Shahidi: Hayo maelezo yaliandikwa na Bahlgyamu yakaletwa.
Lissu: uliyasoma?
Shahidi: niliyasoma.
Lissu: sasa waeleze majaji. Waheshimiwa majaji, ayasome hayo.maelezo:
Shahidi: anayasoma.
Lissu: mpaka hapo kuba mahali mmeangalia video?
Shahidi: hakuna
Lissu: kwenye maelezo yako ya jana, ulisema ulimwona Mh. Lissu akiwa amevaa kombati ya Hadema na nyuma yake kulikuwa na balendera ya Chadema na bendera ya Taifa. Hayo maelezo yapo kwenye maelezo yapo?
Shajidi: Hayapo
Lissu: ulisema jana kwamba Mh Lissu alikiwa anahitubia Taifa. Waeleze majaji kama maelezo yako uapo.
Shahidi: hayapo.
Lissu: shahidi ulisema baada ya hapo uliwasiliana na Idara ya Uhamiaji ambayo iliwathibitishia kwamba Lissu ji raia. Ni kwelj?
Shajidi; Ni kweli
Lissu: Waeleze majaji
Shahidi: hayapo
Lissu; Waeleze majaji kama umewasilisha mahakamani barua ya uhamiaji
Sahidi: Barua ipo
Lissu: Umewasilisha
Wakili Nasoro Katuga ameeingiliabtena akisema kwamba hiyo baruabsio lazina iletwe lakini Jaji Ndunguru amemkatisha Katuga akisema swali liko sawa.
Lissu: Swali langu lijibiwe.
Shaidi: Anatoa maelezo
Jaji Ndunguru; Shahidi nikusaidie, jibu swali.
Mjadala Kuhusu Katiba, Video, na Vielelezo Vilivyokosekana
Lissu: Kwenye maelezo yako ulisema nilichapisha hayo maneno kwenye mtandao wa Youtube wa Jambo TV, waeleze malezo yapo kwenye maelezo yako.
Shahidi: Hapana.
Lissu: kwenye maelezo yako kwamba jitavuruga uchaguzi. Ukasema mlinzi wa sheria na katiba ni serikali, ni kweli?
Shajidi; ni kweli
Lissu: Umewahi kusoma Katiba (ya Jamhuri ya Muungano)?
Shajidi: Miaka ya nyuma
Lissu: Katiba inasema ibara ya 26. Kila mtu ana wajibu wa kuifuata na kuitii na kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano. Wewe unasemaje?
Shahidi: Hiyo ni kuitii
Lissu: Na kuilibna
Shahidi: Hapo amesema kuiitii.
LIssu: Kama huelewi sema sieleqi.
Lissu: Umesema kukikuwa na mipango ya kuvuruga uchaguzi kulikuwa na mipango ya kupiga mawe na mambo mbalimbali. Waeleze majaji kama hayo maneno yapo.
Shahidi: Hayapo
Lissu: Ulisema hiyo video iliwekwa kwenye memory card ikafikishwa kwenye maabara ya uchunguzi wa kisayansi na kupata taarifa kwam ahiyo ni video halisi. Ni kweli? Waelwze majaji kama hayo maneno yapo?
Shahidi:Hayapo
Lissu: kwa kuwa wewe ni shahidi wa 16 na kuna mashahidi wengine 15 waliopita hakuna hata mmoja aliyeonyesha hiyo video, naomba uwaambie majaji kama umewasilisha hiyo video.
Shahidi: Sijawasilisha.
Lissu; kwakuwa wewe jshajidi wa 16 na wale wengine 15 hawakuleta repot ya uchunguzi hawakuileta.waelwze majaji kama umewasilisha.
Shahidi: sijawasilisha.
Lissu: Ulisema ulimwelekeza mchunguzi alete hivyo vielelwzo na hivyo vielelzo vilikabidhiwa kwa kukabidhiwa kwa Mkaguzi msaidizi wa polisi (anataja jina). Hayo maelezo yapo?
Shaidi: Hayapo.
Lissu: Ahsante sana. Kwenye ushaidi wako wa jana ulisema baada ya kufanya yote hayo uliwasiliana na ma RCO mikoa nchi nzima ili kuona kama hayo maneno yalikiwa yamesambaa.
Ukasema ukawaambia wakueletee taarifa ni baadhi tu na ulitaja mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya Ruvuma na Dares Salaam. Kweli si kweli? Kwenye maelezo ulitaja majalada kutoa mikoa mbalimbali ikiwamo Ruvuma, Mbeya na Dar es Slaam.
Waeleze majaji kama hilo jalada lipo kwenye maelezo yako.
Shahidi: halipo
Lissu; kwenye ushahidi umeeleza ya Aprili 9 2025, umesema mtuhumiwa alikamatwa na kusafirishwa siku hiyo hiyo na kufikishwa kituo cha polisi Dar es Salaam na alipelekwa kwa ofisi ya Deputy ZCO na alisomewa tuhuma zake.
Waeleze majaji hayo maelezo yako yapo.
Shahidi: Hayapo.
Lissu: Ulieleza baada ya hapobukapeleka failing kwenye ofisi ya mashitaka. A jalada la upeleleze lilirudishwa kwetu kue delea na upelelezi. Waeleze majaji hayo maneno kuendelea na upelelwzi yapo.
Shahidi: Hayapo.
Lissu: katika maelezo yako umesema mashahidi kutishiwa wakati mnaendelea na upelelezi. Hayo ma enough yapo?
Shahidi: Yapo kwenye affidavit
Lissu: Nimekuukiza affidavit? Usinipleke huko nitakufikisha. Ulieleza kwamba mashahidi walitishiwa kwenye mutabdao kwamba watawasalimia, wanawatishia wakija kutoa ushahidi na ulisema ulipitia mitandao na ulitaja Instagram na Facebook ukaona vitisho.hayo maelezo yapo?
Ulisema kuna haja kuomba ulinzi wa mashahidi? Hayo maneno yapo?Waeleze majaji kwamba uliwasiliasha barua ya mawasiliano ya kuomba ulinzi.
Shahidi: Sijawasiliasha.
Hayo ni maeneo niliyosema bakupitisha, sasa twende kwingine. Kwenye maelezo yako ulisema ulikula kiapo, waeleze waheshimiwa majaji kama.a uliiputia hiyo affidavit.
Shahidi: Nimeipitia.
Lissu: Hata mimi ninau. Hii affidavit ni ya kuombabulinzi wa mashahidi. Ni kweli?
Shahidi: Ni kweli?
Lissu: waeleze majaji kama ulitaja jina la shahidi yoyote?
Shahidi: sikutaja lakini...
Lissu: inatosha hayo menginenutaeleza kwa hao mawakili. Waeleze majaji kama ulitaja maji la mtu aliyewatishà. Swali lingine, waeleze majaji kama a ulitaja ya wanachama wa Chadema?
Ulitaja tarehe, siku mahali walipotishiwa hao mashahidi?
Shahidi;Anaongea
Lissu: Ulitaja ai a ya vitisho? Kama ni kuua au kujeruhi?
Shahidi: Nilitaja.
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimsomee.
Anasima wakili wa serikali mwenye ushungi anamtaka Lissu afuate utaratibu. Hiyo nyaraka ilikuwa kwenye kesi nyingine na ilitolewa hukumu. Lakini anatumia nyaraka kumhoji mtu kwa.kesi nyingine.
Lissu; utaratibu upi?
Majaji wanajadiliana:
Lissu: Nimekaa gerezani muda mrefu nimeanza kusahau taratibu. Umeona hiyo affidavit, angalia uliposaini mbele ya kamishna Rosemary Mbawa. Kesi ya uhaini haijawahi kuwa rahisi.
Kuna mahali popote uliposema kwamba una shahidi ametoshiwa kupigwa?
Shahidi: Anasoma kisha anasema; ipo lakini kwenye ushahidi...
Lissu: usilete mae enough ya huko. Niambie kama kwenye ushaidi kuna neno kutisha.
Shahidi: lipo, anasoma
Lissu; Body harm inamaana kuchoma moto, kupiga...Kuna shahidi aliyeambiwa tutapiga ndugu zako? Kuna shahidi aliyesema atauliwa?
Shahidi: Hapana.
Lissu: Mashahidi wote waliokuja hapa wote niliwauliza wakaasema hawakutishiwa.
Kati ya maelezo ya mashahidi na maelezo yako majaji wafuate ushahidi wa nani?
Shahidi; Mimi sikuwaona
Lissu; Mimi niliwahoji wakasema hawakutishiwa.
Shahidi: Wafuate ushahidi wangu.
Utata wa Mahali Anapoishi Mpelelezi na Kujiandikia Maelezo
Lissu: angalia kielezo chako. Maelezo ulipoandika kazi yako. Amin Mahamba, kazi askari polisi, kabila Mjita, dini Muislamu, umri 49 jana umesema 50. Makazi Goba, Cobalt njia 4, mtaa Matosa. Sasa hapo kwenye makazi.
Waeleze waheshimiwa majaji, Cobalt ipo Halmashair ya manispaa ya Ubungo.
Shajidi: kiutawala?
Lissu: ndio kwani iko Mbeya? Kuba mbunge wa ubungo zamani hapo atakusaidia.
Shahidi: mimi sijaelewa unataka nini
Lissu: Itanielewa vizuri
Anasoma tangazo la serikali la mgawanyo wa maeneo.
Jaji Ndunguru: kwa ninin usiulize tu swali?
Lissu; nataka nimwelewe maana anajifanya smart lakini hana lolote? (Anataka majina ya kata)
Kata ya Goba, umesema Kata ya Matosa.
Shahidi: Mtaa wa Mwaksusa
Lissu: Kuna mtaa wa Mwakasusa hapo? Askari mpelelwzi mbobevu hujui hata mtaa unaokaa.
Twende kwenye kuelelezo D 15 Waeleze majaji nani aliyeandika hicho kielelezo.
Shahidi; Nimeandika mwenyewe.
Lissu; hayo ni maelezo ya onyo
Shahidi: hayo maelezo yangu.
Lissu: Waeleze majaji kama shahidi ana mamlaka ya kujiandikia maelezo?
Shahidi: Mimi ni shahidi mpelelezi.
Lissu: Tutakuja huko.
Shahidi: Sheria haijafafanua, lakini imesema, utaratibu ni kwamba shahidi anaandikiwa maelezo na ofisa wa polisi, lakini hapo tunaandika tu.
Lissu: kwa kuw anibyi la polisi mnajiandikia tu?
Shahidi: Tuanandika tu.
Lissu: Ulipewa onyo na nani?
Shahidi: Tunatoa tamko
Lissu: Hilo tamko umelitoa mbele ya nani?
Shahidi: Mimi polisi.
Lissu; Wewe ni polisi mimi ni mwanasheria.
Shahidi: Nimeandika mwenyewe.
Lissu: Hapo kwenye saini ya mtoa maelezo saini ya nani?
Shahidi; Yangu mwenyewe.
Lissu; Kwenye majukumu yako umesema hivi, majuku yangu yangu ya msingi nikiwa ofisa wa polisi ni kulinda raia na mali zao. Ni kweli?
Shahidi: Ni kweli
Lissu: ulisema upo kitengo X
Lissu: Waeleze majaji ukinzi wa raia na mali zao unahisika na kitengo X
Shahidi: Vinahusiana.
Lissu: Anafahamu PGO? Naomba ninwonyeshe PGO 6 para 8 anampa mshitakiwa PGO. Waeleze waheshimiwa kama hayo majukumu ya kitengo X ni pamoja na kulinda raia na mali zao.
Shahidi: ni sehemu ya majukumu (anasoma)
Kama hiyo raia na mali zao.
Unaposema kulinda raia, ni usalama.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kwamba kuna ku akitengo Y
Shahidi: Ndio
Sasa hapo unataka kunitoa nje?
Lissu: Nataka nikutoe nikurudishe hadi tutafika. waeleze.majaji lazi za kitengo Y
Shahidi: ni usalama wa nchi.
Amini Mahamba wa Singida ni yupi?
Lissu: Waleze majaji kama umewahi kuwa RCO Mkoa wa Singida
Shahidi: hapana, sijawahi hata kufanya kazi Singida.
Lissu. Katika kipindi ulichofanya kazi kama RCO kulikuwa na mtu mwingine anayeitwa SSP Amini Mahakmba aliyekuwa RCO Singida?
Shahidi: Majina ylikuwa yanafanana.
Lissu: Waheshimiwa majaji shahidi anadanga kuwa ana oath. (Anasoma kesi)
Amini Mahamba anayezungumzwa na Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa torture. Swali langu, huyo Amini Mahamba nibyupi?
Shahidi: Sio mimi, ila majina yanafanana na bahati mbaya ameshakufa.
Lissu: no stone will be lest unturned this is the treason case. Umesema kitengo Y ni usalama wa Taifa. Waeleze majaji kama ulimshirikisha Regional security Officer.
Shajidi: Sio majukumu yake.
Lissu: waeleze.majaji kama kwenye upelelezi wako uliwashirikisha Mkurugenzi Mkuu wa TISS
Shahidi, sikuwashirkisha
Lissu: Ulishirikisha ofisa yoyote wa Idara ya Usala.a wa Taifa na Ujasusi.
Shahidi: sikuwashiikisha.
Lissu; Waeleze majaji kama unafanya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Waeleze waheshimiwa majaji kama uliishirikisha.
Shahidi: Sikuwashirikisha
Lissu: Waeleze majaji kama ulishirikisha Ikulu, Ofisi ya maamu wa rais, ofkiso ya waziri mkuu.
Shahidi: Sikuwashirikisha
Lissu: Waeleze majaji uliwashirikisha DPP?
Shahidi: Niliwashirikisha kupitia ofisi ya Mashitaka Mheshmiwa Mayenga.
Lissu: Waeleze majaji kama katika kielezo D15 umeeleza hilo
Shahidi: sijaeleza.
Lissu: kwa mujibu wa sheria, mwenye jukumu la kuratobu wa upelelezi wa makosa ya jinai ni DPP kupitia mawakili wake. Ni DPP yupi au ofisa gani aliyeratibu upelelezi?
Shahidi: Nilipata makao makuu ya ofisi ya mashitaka Dodoma.
Lissu: Swali langu mtu aliyekuwa anaratibu upelelezi wa kesi hii? Ni DPP mwemyewe au ofisa wake.
Shahidi: Ni ofisi ya Dpp, ku a mtu aliyetuliwa. Alitoka ofisi ya DPP.
Lissu: anaitwa nani?
Shahidi: ana majina magumu ya Kibantu.
Lissu: Tutapeleka kwa DPP Mwakitalu atupe jina.
Lissu: Kwenye kielelezo D15 umesema wewe ni mbonevu, je umewahi kusimamia au kupeleleza kesi ya kisiasa?
Shahidi: Kesi ya jinai au kisiasa?
Lissu; kesi ya uhaini ndio kesi kubwa ya kisiasa ndio wameshitakiwa mwenyewekiti.
Waeleze majaji kama umewahi kupeleleza kesi ya mtu aliyelwahi kuwa mbu au kiongozi kama mimi Lissu.
Sahidi: Sijawahi.
Lissu: umesema kitengo X kinasimamia kesi ya makosa ya mtandao. Waeleze majaji kama aunewahi kusimamia kesi ya mtavdao.
Shahidi: Nimewahi. Kesi ya mheshimiwa Mbowe na Slaa.
Lissu: Ni kesi ya mwenyewekiti wangu mtangulizi (Freeman) Mbowe na katibu mkuu wake (Dk Wilbrod) Slaa.
Shahidi: Ilikuwa kesi ya uchoxhezi.
Lissu: Kesi iliishije?
Shahidi: Iliisha tu.
Lissu: iliishaje au mliona mambo yamekuwa magumu mkaifuta mka8ngiza nolle?
Shahidi: kesi iliisha baada ya kukosa ushahidi.
Lissu; mlianzisha kesi bila kuwa na ushahidi?
Nitakuwa sahihi kwa ubobevu wako wote wa miaka 26 uneishia kusimamia kesi mmoja tu ya siasa na ikafutwa?
Shahidi: Kesi ilifutwa.
Lissu: Sasa tuje kwenye ushahidi. Ulisema mimi diye niliyechapisha hiyo video kwenye Jambo TV? NI kweli? Waeleze majaji maana ya neno kuchapisha au nikusomee?
Shahidi: Kosa ulikoshitakiwa ni la jinai sio kwa sheria hiyo.
Lissu: wewe si ndio umesema nilichapisha? Ngoja nikusomee: "kuchapisha ni distrbuting" waeleze majaji kwamba mimi ndoye sambaza
Shahidi: Ni wewe.
Lissu: Transmitting: waambie majaji kama ni mimi ndiye transmit?
Shahidi: Ni wewe
Lissu: publishing ni dissemination, circulation. Waeleze majaji kama mimi niliye...
Shahidi: ni wewe.
Lissu waeleze majaji kama wewe ni mkurugenzi au mtumishi wa Jambo TV.
Shahidi: sina uhakika
Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mpiga picha qa Jambo TV
Waeleze majaji kama mimi ni password ya Jambo TV
Shahidi; su a uhakika
Lissu: wewe ndiye ulikiwa mpelelwzi wa Mambo yote ba huna uhakika? Tuendelee.
Ni kweli kwamba hiyo video mnaosema nilituhumiqa ilichukuliqa na shahidi P1
Shajidi: sio P1 sijajua.
Lissu ulisoma maelezo ya P1?
SHAHIDI; Nilisoma
Lissu: Ni kweli kwamba siku hiyo tulikuwa na camera 3 na camera moja aina ya Sony tulikuwa tunarusha mubashara kupitia channel ya YouTube ya Jambo TV.
Kwenye maelezo yake alisema tulipofika makao makuu ya polisi Dodoma ofisa wa polisi alitutaka tukabidi memory card kwa polisi.
Shahidi: ni kweli.
Lissu: kuna shahidi anaitwa P
Ni kweli kwamba yeye kwa kutumia camera ya Sony NX ndiyekuwa akipiga pocha na kurusha mubashara.
Ni kweli kwamba huyo P na wenzake wayatu ndio walisema kwamba wao ndio walikuwa wakifabya live streaming?
Shahidi: ni kweli.
Lissu: Ni kweli kwamba P alisema kwamba yeye ndiyehifadhi jayo mahudhui?
Shahidi: Ni kweli.
Lissu: uliyasoma maelezo ya George Bagyemu
Shahidi: nilisoma.
Lissu: huyo Bagyemu Deputy ZCO alisema hiyo video ilirekodiwa na kurushwa na wafanyakazi wa Jambo TV. Ni kweli
Shahidi: Ni kweli.
Lissu: Ni kweli kwamba hao P na P1 walipewa.maelekezo ya kurekodi mkutabo wangu na Mkurugenzi wa Jambo TV John Marwa na alipewa mwaliko na mkurugenzi wa habari wa Chadema.
Shahidi: Ni kweli.
Lissu: Nimekaa gerezani leo siku 490 mwaka na miezi minne kwa tuhuma kwamba jilichapisha video, wakati monyi mna ushahidi kwam a waliochapisha ni Jambo TV. Nina familia kama wewe, nina watoto niba ndugu hawa. Waeleze majaji huo ndio utendaji wa Jeshi la polisi?
Shahidi; Hao walichapisha P na P1 lakini walialikwa?
Lissu; mimi ndio nauliza maswali, nyamaza. Mlimuhoji mtu yoyote Chadema? Waelwze majaji kama mlimuhoji naibu Katibu mkuu, Golugwa? Mlimuhoji Makamu Mwenyekiti huyo hapo awaeleze Mkurugenzi wa habari ni nani?
Shahidi: Hao ni viongozi wa Chadema na wewe i kiongozi.
Lissu: Kwa hiyo mwenyekiti wa chama anawajibika kijinai na makosa yabayofanywa na viongozi wenzake? Waheshimiwa majaji shahidi ajibu swali langu.
Jaji Ndunguru: jibu swali.
Shahidi: Hawajibiki.
Lissu; Hotuba yangu ilikuwa inahusu matatizo ya uchaguzi mkuu na matatizo yake?
Shahidi: ndio
Lissu: Naomba uwaleze majaji: kwa katiba hii mtu anahamasisha kuzuia uchaguzi anafanya kosa la uhaini.
Shahidi: katiba haijaanisha hilo.
Lissu: Unaifahamu kwamba unaifahamu sheria ya uchaguzi wa rais wabunge na madiwani. Waeleze majaji kama kwa Sheria hiyo inasema ni kosa la jinai kuzuia uchaguzi au kuhamasiaha watu kuvuruga uchaguzi
Shahidi: Sina uhakika sana.
Lissu: Mimi nina uhakika kwamba kwa Sheria hii kuhamasiaha kuvuruga uchaguzi sio kosa lolote? Wewe unasemaje?
Shahidi: wewe umesgitakiwa kwa uhaini.
Lissu: Kabla ya uhaini nimeshitakiwa kwa kuhamasisha kuvuruga uchaguzi.
Jana umeulizwa ukatumia sheria ya Penal code 39(2) d, waeleze waheshimiwa majaji kwamba uhaini ni oamoja na kivururuga uchaguzi.
Lissu: kwenye hayo uliyosoma kunaneno linaloeleza uchaguzi?
Shahidi: Lipo?
Lissu: nauliza tena, una akili timamu?
Shahidi: Ndio
Lissu: ACP. Hicho kifungu kinaeleza mtu anayetishia serikali, Bunge na mahakama. Mimi nilitishia serikali, bunge na mahakama?
Shahidi: wewe ulitishia serikali
Lissu: Nilitishia bunge? Nilitishia, mahakama?
Shahidi: hapana.
Lissu: Anasoma hati ya mashitaka.
Shahidi: Wewe ndio uliyepeleleza hayo maneno.
Lissu: Niambie maana ya serikali.
Shahidi: Ni mamlaka ina mihimili mikuu mitatu, mamlaka, mahakama na Bunge.
Lissu: naomba nimsomee Katiba ya Jamhuri ibara ya 151:1.
Kwenye hayo maelezo, wapi nilitaja Serikali ya Jamhuri ya Muungano?
Shahidi: umeyataja
Lissu: Shahidi una akili timamu?
Shahidi: Ndio.
Lissu; Nimetaja Serikali ya Mapinduzi ya Zanibar? Kuba mahali nimetaja halmashauri ya jiji la Dar es Salaam au jiji lolote? Au halmshauri youote?
Shahidi; umetaja.
Lissu: Waeleze majaji kama nimetaja jina la Rais Samia Suluhu Hassan
Shahidi: Hujataja
Waeleze majaji kama nilimtaja Makamu wa Rais wakati huo, Dk Philip Isidory Mpango na Waziri mkuu Kassima Majaliwa?
Shahidi hapana.
Lissu: Uchaguzi unasimamiwa na chombo gani?
Shahidi; Tume ya uchaguzi
Lissu: Nilitaja Tume ya uchaguzi?
Shahidi: ulitaja mambo ya uchaguzi
Lissu nilitaja Tume ya uchaguzi?
Shahidi; Hapana.
Lissu: Kwenye ushahidi wako kuna Inspekta anaitwa Andrew Churu aliyechukua ile hifadhi ya video na kuleta Dar es Salaam?
Shahidi; Ndio
Lissu: Waeleze majaji kama umesoma maelezobya Inspector Andrew Churu?
Shahidi: nimesoma
Lissu; maelezo Churu kwamba haonwafanyakazi wa Jambo TV ndio waliorekodi na kurusha ...
Shahidi: Ndio
Lissu: Umesoma maelezonya P?
Shahidi: Nimeyasoma.
Lissu: Anasoma maelezo ya P. Shahidi waeleze majaji, mnanitesea mimi nini ikiwa mna ushahidi wa waliofanya hayo makosa?
Shahid: Kazi yangu ni kuthibitisha kosa
Lissu kama hayo wameyasema waliyofanya na polisi wenzako, mnanitesea nini?
Shahidi: wewe ndio umesema hujateswa.
Lissu: Mwaka mmoja na zaidi niko gerezani.
Lissu: Turudi kwenye PGO 1 aya ya 25.
Upelelezi wa makosa unapaswa kufuata sheria. Makosa ni matendo yaliyotajwa na sheria. Swali: Penal code 39 inataja kuvuruga uchaguzi?
Shahidi: Ni kutishia serikalj sio kuvuruga uchaguzi. PGO kila askari polisi ana wajibu kuheshimu haki na uhuru wa wananchi kwa.mujibu wa katiba na sheria za nchi. Kweli?
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Haki yangu ya Katiba, ibara ya 15:1.
Waeleze waheshimiwa majaji kwamba ku a mahali popote katika maelezo yako polisi uliheshimu uhuru wangu?
Shahidi; Wewe ulihojiwa na askari wengine
Lissu; hao wengine nilishamalizana nao nakuuliza wewe. Kosa nimeshaeleza mengine hakuna lolote.
Shahidi: Hakuna.
Lissu: Anasoma Ibara ya Ibara 19(1) ya Katiba ya Jamhuiri ya Muungano inayohusu Uhuru wa maoni, mawazo. Mlizingatia uhuru wangu wa mawazo kwenye kazi zangu? Ibara 20 Uhuru wa kukutana na watu wengine kwa uhuru na kutoa maoni yake hadharani kwa amani.
Chama changu kiliitisha mkutano wa watia nia, wakaitisha waandishi wa habari kuna p P1. Mwemyekiti akahutubia. Mlizingatia uhurubwangu wa kukutana a kutoa maoni?
Shahidi: wewe uliitisha Serikali
Lissu: Nimemtisha nani?
Shahidi Serikali.
Lissu; Ndio maana nikasema inawezekana tunazungumza na mtu ambaye ugonjwa wa akili upo.
Lissu: nilisema tune ya uchaguzi ni ya CCM inateuliwa na mwenyekiti wa CCM? NI KWELI
Shahidi: Ni kweli
Lissu; nilisema Tume yabuchaguzi imekuwa na tabia yabkuengua wagombea wa upinzani?
Shahidi: Ni kweli. Nikasema Mheshimiwa Rais Samia ndio amekuwa akielekeza?
Shahidi: Ni kweli.
Jaji Ndunguru ameahirisha kesi hadi saa 8: 10 mchana.
Usiondoke jfKivipi Amin Mashamba ameshaeleza ACP Shahid aliyefariki ni wa Singida na huyu ni wa Goba Dar
Taarifa zote tunazoHapa kuna uwezekano WA mambo ya vyetí féki, n.k
Hivi ni Saa Nane? au Saa Mbili?View attachment 3648282

Kwahiyo huyu ameji impersonate kuwa ni Amini kumbe siye! Ni jinai for impersonationSijui kama mnaelewa, huyu siyo Mahamba mwenyewe, hili bomu litafumuka kesho
Incompetence iliyopo kwenye hivyo vyombo ni very very huge inatisha. Ni kutumia nguvu tu ila kichwani ni empty headsHii kesi imetupa ushahidi wa ukilaza wa watumishi wa vyombo vya dola, wingi wa watumishi feki/hewa na wasio na uwezo wa kutimiza majukumu yao.
Hakila kesi hii inathibitisha yale aliyoyasema Prof. M. Assad kuhusu 60% ya watumishi wa umma ni hawana uwezo.
Ni wa kukamatwa hapo hapo kwa kujifanya afisa wa serikali.Kwahiyo huyu ameji impersonate kuwa ni Amini kumbe siye! Ni jinai for impersonation
Impersonation—legally termed "false personation" or "personation"—is a criminal offense under penal codes where an individual falsely pretends to be someone else, or pretends to hold a public office, with the intent to deceive, defraud, or gain an unlawful benefit
Trust me wako wengi sana haswa polis, too much forgery serikal ikiwa serious inaweza chomoa 60% ya hawa watu kaziniHapa kuna uwezekano WA mambo ya vyetí féki, n.k
Msitoe siri jamaniKwahiyo huyu ameji impersonate kuwa ni Amini kumbe siye! Ni jinai for impersonation