Lissu alivyomkaanga Mpelelezi Mkuu wa kesi yake

Lissu alivyomkaanga Mpelelezi Mkuu wa kesi yake

Sema kama ni kweli serikali italizima hili jambo Leo Leo.

Ila kama mahamba ameshafariki na mahamba huyu ni mtumishi hewa lissu aweke cheti cha kifo na , force number na vyeti vya elimu.. hapo ngoma itakua NGUMU.

Hiii inaitwa shahidi batili kutoa Ushahidi batili kwenye kesi batili....
Nasikia mahamba originally alikuwa SACP Tena mtu wa Njombe au Ruvuma,Eti huyu mjitaa!
 
Hivi hawa police huwa wanaajiriwa kwa kutumia merits zipi?
Mbona. Weupe hivyo vichwani?
 
View attachment 3648282
Leo Agosti 11, 2026 katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu anayeshitakiwa kwa kesi ya uhaini, ameendelea kumhoji shahidi wa 16, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP), Amini Mahamba.

Kesi hiyo inasikilizwa na majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.

Utata wa Ushahidi Mahakamani vs Maelezo ya Polisi

Lissu:
rafiki habari yako? Umelala vizuri?

Shahidi; Nipo vizuri.

Lissu: Jana nilikupitisha kwenye ushaidi kwa jinsi ulivyoandika polisi. Naomba ujibu kwa sauti kama mpelelezi mbobevu na askari anaweza kuongoza gwaride.

Jana ulieleza kwamba uliteuliwa kuwa OC CID wilaya ya Kyela anayewasimamia wapelelezi.

Shahidi: Ni kweli.

Lissu: waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo ya polisi.

Shahidi: hayapo.

Lissu; Ukasema kuwa ulipandishwa cheo na kuw ampelelezi RCO Ruvuma.

Shahidi: Ni kweli

Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yapo kwenye maelezo uliyoadika polisi.

Shahidi: Hayapo

Lissu: Leo tutakwenda vizuri.

Lissu: Kwenye ushaidi wako ukasema 2025 ukahamishiwa Dar es Slaam kwa ZCO mkoa unaosimamia wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke.

Waeleze waheshimiwa majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo uliyoandika polisi.

Shahidi: Hayapo.

Lissu: Mwaka 2025, ukateuliwa kuwa RCO Kinondoni

Mnajiandikia andikia tu halafu mnamshitaki mwenyekiti wa chama kwa uhaini.



Siku ya Tarehe 8 Aprili na Kielelezo D15



Lissu;
sasa nataka tuzungumze ya Tarehe 8 April 2025. Kwenye ushaidi wako jana ulisema mnamo April 8 nikiwa ofisini kwangu nilipigiwa simu na mkuu wangu wa kazi, CP Ramadhani Kingai kwenda ofisi za polisi Dar es Salaam kufungua kesi ya uhaini inayomhusu mtuhumiwa Tundu Lissu. Waeleze majaji kama hayo maelezo yapo.

Shahidi; Yapo.

Lissu: Mpeni Exhibit D15

Katuga anasimama kumtaka Lissu kutotoa kauli za kuagiza badala yake aombe.

Lissu: Samahani majaji. (Anayasoma maelezo ya kielelezo, kisha anamuuliza shahidi)

Hayo maelezo yapo?

Shahidi: Yapo.

Lissu: Kuna jina la Lissu?

Shahidi: Yapo.

Lissu: Kwa kawaida ACP Mahamba una akili timamu?

Shahidi: Ndiyo

Lissu: Unajifanya mjanja sana lakini hauna kitu.

Shahidi; suala ni jalada kuwepo.

Lissu; Anasoma tena exhibit. Swali langu hayo maneno yapo? Kwenye ushaiidi sio kutoa kichwani mwako.

Shahidi: Hayapo.

Lissu: Ulipofika kwenye ofisi ya upelelezi kwa Bagyemu uliunda timu tatu za upellezi. Timu ya kwanza ilikuwa na (anawataja). Waeleze majaji hayo maelezo yapo kwenye ushahidi?

Shahidi: Hayapo

Lissu: Umeeleza katika timu ya upelelezi, alikuwepo George Bagyemu...Waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo uliyoandika polisi,

Shahidi: hayapo

Lissu: Kuandika andika tu. Ulisema katika tumu uliyoita legal advisor ili mwonekano wa kutumia sheria.

Umesema kulikuwa na mwanasheria mwenye jina la Kibantu na mimi ni Mbatu anaweza kuwa Mnyaturu. Nilipomhoji shahidi namba 1 George Bagyemu alisemakulikuwa na Mwanasheria na wewe unasema kulikiwa na mwanasheria. Majaji wamwamini nani?

Shahidi: Hakukuwa na mwanasheria

Lissu: George Nagyemu ni liongo.

Lissu: Ulisema mlichukua kompyuta inayomilikiwa na (anamtaja) kwa saa mbili. Hayo maelezo yapo?

Shahidi: Hayapo

Lissu: Shahidi George Bagyemu alisema hiyo video ya Jambo TV aliiangalia kutoja kwa Inspector Kaaya tena aliangalia vipande vipande. Wewe unasema mliangalia kwa saa mbili.

Katuga: Anamkosesha shahidi anaposema Bagyemu aliangalia kwa vipande. Hiyo ilikuwa tarehe 4 na yeye anazungumzia tarehe 8 ni vitu viwili tofauti.

Majaji wanajadiliana.

Lissu:
waheshimiwa Majaji. Mawakili wa Serikali si watakuja kufanya re examination? Kwa nini waniulize sasa hivi? Si wana haki yabkuniuliza wakati wa re examination? Kwani kuongoea ndio mwisho?

Pili, mawakili wa serikali wako wanane wna haki ya kunipangia nini cha kuuliza?

Jaji Ndunguru; naomba tuendele, lakini tuzingatie...

Lissu: Narudia swali: majaji wafuate ushaidi wa nani?

Shahidi: Jayo ni matukio mawili tofauti, hiyo ilikiwa Aprili 4 aliingalia kwa vipande kabla mimi sijateuliwa na hayo yabpili tuliangalia kwa saa 2.

Lissu: Sawa, maelezo ya George Bagyemu yapo kwenye information ambayo nimeshitakiwa nayo nilikuyataka nimaoigwa chini. Lakini nibrekodi ya mahakama.

Katuga anaingilia, lakini Jaji Ndunguru, anamkatisha akisema asubiri kwanza shahidi aongee.

Lissu; ahsante majaji, kilichonileta mahakamani ni haya maelezo (anaonyesha hati ya mashitaka).

Shahidi: Mimi sina hayo maelezo ni kielelezo cha mahakama.

Lissu: Wewe hujui, acha nikujulishe. Hayo ni maelezo ya polisi ni maelezo mliyokusanya wenyewe.

Shahidi: Hayo maelezo yaliandikwa na Bahlgyamu yakaletwa.

Lissu: uliyasoma?

Shahidi: niliyasoma.

Lissu: sasa waeleze majaji. Waheshimiwa majaji, ayasome hayo.maelezo:

Shahidi: anayasoma.

Lissu: mpaka hapo kuba mahali mmeangalia video?

Shahidi: hakuna

Lissu: kwenye maelezo yako ya jana, ulisema ulimwona Mh. Lissu akiwa amevaa kombati ya Hadema na nyuma yake kulikuwa na balendera ya Chadema na bendera ya Taifa. Hayo maelezo yapo kwenye maelezo yapo?

Shajidi: Hayapo

Lissu: ulisema jana kwamba Mh Lissu alikiwa anahitubia Taifa. Waeleze majaji kama maelezo yako uapo.

Shahidi: hayapo.

Lissu: shahidi ulisema baada ya hapo uliwasiliana na Idara ya Uhamiaji ambayo iliwathibitishia kwamba Lissu ji raia. Ni kwelj?

Shajidi; Ni kweli

Lissu: Waeleze majaji

Shahidi: hayapo

Lissu; Waeleze majaji kama umewasilisha mahakamani barua ya uhamiaji

Sahidi: Barua ipo

Lissu: Umewasilisha

Wakili Nasoro Katuga ameeingiliabtena akisema kwamba hiyo baruabsio lazina iletwe lakini Jaji Ndunguru amemkatisha Katuga akisema swali liko sawa.

Lissu: Swali langu lijibiwe.

Shaidi: Anatoa maelezo

Jaji Ndunguru; Shahidi nikusaidie, jibu swali.



Mjadala Kuhusu Katiba, Video, na Vielelezo Vilivyokosekana



Lissu:
Kwenye maelezo yako ulisema nilichapisha hayo maneno kwenye mtandao wa Youtube wa Jambo TV, waeleze malezo yapo kwenye maelezo yako.

Shahidi: Hapana.

Lissu: kwenye maelezo yako kwamba jitavuruga uchaguzi. Ukasema mlinzi wa sheria na katiba ni serikali, ni kweli?

Shajidi; ni kweli

Lissu: Umewahi kusoma Katiba (ya Jamhuri ya Muungano)?

Shajidi: Miaka ya nyuma

Lissu: Katiba inasema ibara ya 26. Kila mtu ana wajibu wa kuifuata na kuitii na kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano. Wewe unasemaje?

Shahidi: Hiyo ni kuitii

Lissu: Na kuilibna

Shahidi: Hapo amesema kuiitii.

LIssu: Kama huelewi sema sieleqi.

Lissu: Umesema kukikuwa na mipango ya kuvuruga uchaguzi kulikuwa na mipango ya kupiga mawe na mambo mbalimbali. Waeleze majaji kama hayo maneno yapo.

Shahidi: Hayapo

Lissu: Ulisema hiyo video iliwekwa kwenye memory card ikafikishwa kwenye maabara ya uchunguzi wa kisayansi na kupata taarifa kwam ahiyo ni video halisi. Ni kweli? Waelwze majaji kama hayo maneno yapo?

Shahidi:Hayapo

Lissu: kwa kuwa wewe ni shahidi wa 16 na kuna mashahidi wengine 15 waliopita hakuna hata mmoja aliyeonyesha hiyo video, naomba uwaambie majaji kama umewasilisha hiyo video.

Shahidi: Sijawasilisha.

Lissu; kwakuwa wewe jshajidi wa 16 na wale wengine 15 hawakuleta repot ya uchunguzi hawakuileta.waelwze majaji kama umewasilisha.

Shahidi: sijawasilisha.

Lissu: Ulisema ulimwelekeza mchunguzi alete hivyo vielelwzo na hivyo vielelzo vilikabidhiwa kwa kukabidhiwa kwa Mkaguzi msaidizi wa polisi (anataja jina). Hayo maelezo yapo?

Shaidi: Hayapo.

Lissu: Ahsante sana. Kwenye ushaidi wako wa jana ulisema baada ya kufanya yote hayo uliwasiliana na ma RCO mikoa nchi nzima ili kuona kama hayo maneno yalikiwa yamesambaa.

Ukasema ukawaambia wakueletee taarifa ni baadhi tu na ulitaja mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya Ruvuma na Dares Salaam. Kweli si kweli? Kwenye maelezo ulitaja majalada kutoa mikoa mbalimbali ikiwamo Ruvuma, Mbeya na Dar es Slaam.

Waeleze majaji kama hilo jalada lipo kwenye maelezo yako.

Shahidi: halipo

Lissu; kwenye ushahidi umeeleza ya Aprili 9 2025, umesema mtuhumiwa alikamatwa na kusafirishwa siku hiyo hiyo na kufikishwa kituo cha polisi Dar es Salaam na alipelekwa kwa ofisi ya Deputy ZCO na alisomewa tuhuma zake.

Waeleze majaji hayo maelezo yako yapo.

Shahidi: Hayapo.

Lissu: Ulieleza baada ya hapobukapeleka failing kwenye ofisi ya mashitaka. A jalada la upeleleze lilirudishwa kwetu kue delea na upelelezi. Waeleze majaji hayo maneno kuendelea na upelelwzi yapo.

Shahidi: Hayapo.

Lissu: katika maelezo yako umesema mashahidi kutishiwa wakati mnaendelea na upelelezi. Hayo ma enough yapo?

Shahidi: Yapo kwenye affidavit

Lissu: Nimekuukiza affidavit? Usinipleke huko nitakufikisha. Ulieleza kwamba mashahidi walitishiwa kwenye mutabdao kwamba watawasalimia, wanawatishia wakija kutoa ushahidi na ulisema ulipitia mitandao na ulitaja Instagram na Facebook ukaona vitisho.hayo maelezo yapo?

Ulisema kuna haja kuomba ulinzi wa mashahidi? Hayo maneno yapo?Waeleze majaji kwamba uliwasiliasha barua ya mawasiliano ya kuomba ulinzi.

Shahidi: Sijawasiliasha.

Hayo ni maeneo niliyosema bakupitisha, sasa twende kwingine. Kwenye maelezo yako ulisema ulikula kiapo, waeleze waheshimiwa majaji kama.a uliiputia hiyo affidavit.

Shahidi: Nimeipitia.

Lissu: Hata mimi ninau. Hii affidavit ni ya kuombabulinzi wa mashahidi. Ni kweli?

Shahidi: Ni kweli?

Lissu: waeleze majaji kama ulitaja jina la shahidi yoyote?

Shahidi: sikutaja lakini...

Lissu: inatosha hayo menginenutaeleza kwa hao mawakili. Waeleze majaji kama ulitaja maji la mtu aliyewatishà. Swali lingine, waeleze majaji kama a ulitaja ya wanachama wa Chadema?

Ulitaja tarehe, siku mahali walipotishiwa hao mashahidi?

Shahidi;Anaongea

Lissu: Ulitaja ai a ya vitisho? Kama ni kuua au kujeruhi?

Shahidi: Nilitaja.

Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimsomee.

Anasima wakili wa serikali mwenye ushungi anamtaka Lissu afuate utaratibu. Hiyo nyaraka ilikuwa kwenye kesi nyingine na ilitolewa hukumu. Lakini anatumia nyaraka kumhoji mtu kwa.kesi nyingine.

Lissu; utaratibu upi?

Majaji wanajadiliana:

Lissu: Nimekaa gerezani muda mrefu nimeanza kusahau taratibu. Umeona hiyo affidavit, angalia uliposaini mbele ya kamishna Rosemary Mbawa. Kesi ya uhaini haijawahi kuwa rahisi.

Kuna mahali popote uliposema kwamba una shahidi ametoshiwa kupigwa?

Shahidi: Anasoma kisha anasema; ipo lakini kwenye ushahidi...

Lissu: usilete mae enough ya huko. Niambie kama kwenye ushaidi kuna neno kutisha.

Shahidi: lipo, anasoma

Lissu; Body harm inamaana kuchoma moto, kupiga...Kuna shahidi aliyeambiwa tutapiga ndugu zako? Kuna shahidi aliyesema atauliwa?

Shahidi: Hapana.

Lissu: Mashahidi wote waliokuja hapa wote niliwauliza wakaasema hawakutishiwa.

Kati ya maelezo ya mashahidi na maelezo yako majaji wafuate ushahidi wa nani?

Shahidi; Mimi sikuwaona

Lissu; Mimi niliwahoji wakasema hawakutishiwa.

Shahidi: Wafuate ushahidi wangu.

Utata wa Mahali Anapoishi Mpelelezi na Kujiandikia Maelezo

Lissu
: angalia kielezo chako. Maelezo ulipoandika kazi yako. Amin Mahamba, kazi askari polisi, kabila Mjita, dini Muislamu, umri 49 jana umesema 50. Makazi Goba, Cobalt njia 4, mtaa Matosa. Sasa hapo kwenye makazi.

Waeleze waheshimiwa majaji, Cobalt ipo Halmashair ya manispaa ya Ubungo.

Shajidi: kiutawala?

Lissu: ndio kwani iko Mbeya? Kuba mbunge wa ubungo zamani hapo atakusaidia.

Shahidi: mimi sijaelewa unataka nini

Lissu: Itanielewa vizuri

Anasoma tangazo la serikali la mgawanyo wa maeneo.

Jaji Ndunguru: kwa ninin usiulize tu swali?

Lissu; nataka nimwelewe maana anajifanya smart lakini hana lolote? (Anataka majina ya kata)

Kata ya Goba, umesema Kata ya Matosa.

Shahidi: Mtaa wa Mwaksusa

Lissu: Kuna mtaa wa Mwakasusa hapo? Askari mpelelwzi mbobevu hujui hata mtaa unaokaa.

Twende kwenye kuelelezo D 15 Waeleze majaji nani aliyeandika hicho kielelezo.

Shahidi; Nimeandika mwenyewe.

Lissu; hayo ni maelezo ya onyo

Shahidi: hayo maelezo yangu.

Lissu: Waeleze majaji kama shahidi ana mamlaka ya kujiandikia maelezo?

Shahidi: Mimi ni shahidi mpelelezi.

Lissu: Tutakuja huko.

Shahidi: Sheria haijafafanua, lakini imesema, utaratibu ni kwamba shahidi anaandikiwa maelezo na ofisa wa polisi, lakini hapo tunaandika tu.

Lissu: kwa kuw anibyi la polisi mnajiandikia tu?

Shahidi: Tuanandika tu.

Lissu: Ulipewa onyo na nani?

Shahidi: Tunatoa tamko

Lissu: Hilo tamko umelitoa mbele ya nani?

Shahidi: Mimi polisi.

Lissu; Wewe ni polisi mimi ni mwanasheria.

Shahidi: Nimeandika mwenyewe.

Lissu: Hapo kwenye saini ya mtoa maelezo saini ya nani?

Shahidi; Yangu mwenyewe.

Lissu; Kwenye majukumu yako umesema hivi, majuku yangu yangu ya msingi nikiwa ofisa wa polisi ni kulinda raia na mali zao. Ni kweli?

Shahidi: Ni kweli

Lissu: ulisema upo kitengo X

Lissu: Waeleze majaji ukinzi wa raia na mali zao unahisika na kitengo X

Shahidi: Vinahusiana.

Lissu: Anafahamu PGO? Naomba ninwonyeshe PGO 6 para 8 anampa mshitakiwa PGO. Waeleze waheshimiwa kama hayo majukumu ya kitengo X ni pamoja na kulinda raia na mali zao.

Shahidi: ni sehemu ya majukumu (anasoma)

Kama hiyo raia na mali zao.

Unaposema kulinda raia, ni usalama.

Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kwamba kuna ku akitengo Y

Shahidi: Ndio

Sasa hapo unataka kunitoa nje?

Lissu: Nataka nikutoe nikurudishe hadi tutafika. waeleze.majaji lazi za kitengo Y

Shahidi: ni usalama wa nchi.

Amini Mahamba wa Singida ni yupi?

Lissu
: Waleze majaji kama umewahi kuwa RCO Mkoa wa Singida

Shahidi: hapana, sijawahi hata kufanya kazi Singida.

Lissu. Katika kipindi ulichofanya kazi kama RCO kulikuwa na mtu mwingine anayeitwa SSP Amini Mahakmba aliyekuwa RCO Singida?

Shahidi: Majina ylikuwa yanafanana.

Lissu: Waheshimiwa majaji shahidi anadanga kuwa ana oath. (Anasoma kesi)

Amini Mahamba anayezungumzwa na Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa torture. Swali langu, huyo Amini Mahamba nibyupi?

Shahidi: Sio mimi, ila majina yanafanana na bahati mbaya ameshakufa.

Lissu: no stone will be lest unturned this is the treason case. Umesema kitengo Y ni usalama wa Taifa. Waeleze majaji kama ulimshirikisha Regional security Officer.

Shajidi: Sio majukumu yake.

Lissu: waeleze.majaji kama kwenye upelelezi wako uliwashirikisha Mkurugenzi Mkuu wa TISS

Shahidi, sikuwashirkisha

Lissu: Ulishirikisha ofisa yoyote wa Idara ya Usala.a wa Taifa na Ujasusi.

Shahidi: sikuwashiikisha.

Lissu; Waeleze majaji kama unafanya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Waeleze waheshimiwa majaji kama uliishirikisha.

Shahidi: Sikuwashirikisha

Lissu: Waeleze majaji kama ulishirikisha Ikulu, Ofisi ya maamu wa rais, ofkiso ya waziri mkuu.

Shahidi: Sikuwashirikisha

Lissu: Waeleze majaji uliwashirikisha DPP?

Shahidi: Niliwashirikisha kupitia ofisi ya Mashitaka Mheshmiwa Mayenga.

Lissu: Waeleze majaji kama katika kielezo D15 umeeleza hilo

Shahidi: sijaeleza.

Lissu: kwa mujibu wa sheria, mwenye jukumu la kuratobu wa upelelezi wa makosa ya jinai ni DPP kupitia mawakili wake. Ni DPP yupi au ofisa gani aliyeratibu upelelezi?

Shahidi: Nilipata makao makuu ya ofisi ya mashitaka Dodoma.



Lissu: Swali langu mtu aliyekuwa anaratibu upelelezi wa kesi hii? Ni DPP mwemyewe au ofisa wake.

Shahidi: Ni ofisi ya Dpp, ku a mtu aliyetuliwa. Alitoka ofisi ya DPP.

Lissu: anaitwa nani?

Shahidi: ana majina magumu ya Kibantu.

Lissu: Tutapeleka kwa DPP Mwakitalu atupe jina.

Lissu: Kwenye kielelezo D15 umesema wewe ni mbonevu, je umewahi kusimamia au kupeleleza kesi ya kisiasa?

Shahidi: Kesi ya jinai au kisiasa?

Lissu; kesi ya uhaini ndio kesi kubwa ya kisiasa ndio wameshitakiwa mwenyewekiti.

Waeleze majaji kama umewahi kupeleleza kesi ya mtu aliyelwahi kuwa mbu au kiongozi kama mimi Lissu.

Sahidi: Sijawahi.

Lissu: umesema kitengo X kinasimamia kesi ya makosa ya mtandao. Waeleze majaji kama aunewahi kusimamia kesi ya mtavdao.

Shahidi: Nimewahi. Kesi ya mheshimiwa Mbowe na Slaa.



Lissu: Ni kesi ya mwenyewekiti wangu mtangulizi (Freeman) Mbowe na katibu mkuu wake (Dk Wilbrod) Slaa.

Shahidi: Ilikuwa kesi ya uchoxhezi.

Lissu: Kesi iliishije?

Shahidi: Iliisha tu.

Lissu: iliishaje au mliona mambo yamekuwa magumu mkaifuta mka8ngiza nolle?

Shahidi: kesi iliisha baada ya kukosa ushahidi.

Lissu; mlianzisha kesi bila kuwa na ushahidi?

Nitakuwa sahihi kwa ubobevu wako wote wa miaka 26 uneishia kusimamia kesi mmoja tu ya siasa na ikafutwa?

Shahidi: Kesi ilifutwa.



Lissu: Sasa tuje kwenye ushahidi. Ulisema mimi diye niliyechapisha hiyo video kwenye Jambo TV? NI kweli? Waeleze majaji maana ya neno kuchapisha au nikusomee?

Shahidi: Kosa ulikoshitakiwa ni la jinai sio kwa sheria hiyo.

Lissu: wewe si ndio umesema nilichapisha? Ngoja nikusomee: "kuchapisha ni distrbuting" waeleze majaji kwamba mimi ndoye sambaza

Shahidi:
Ni wewe.

Lissu: Transmitting: waambie majaji kama ni mimi ndiye transmit?

Shahidi: Ni wewe

Lissu: publishing ni dissemination, circulation. Waeleze majaji kama mimi niliye...

Shahidi: ni wewe.

Lissu waeleze majaji kama wewe ni mkurugenzi au mtumishi wa Jambo TV.

Shahidi: sina uhakika

Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mpiga picha qa Jambo TV

Waeleze majaji kama mimi ni password ya Jambo TV

Shahidi; su a uhakika

Lissu: wewe ndiye ulikiwa mpelelwzi wa Mambo yote ba huna uhakika? Tuendelee.

Ni kweli kwamba hiyo video mnaosema nilituhumiqa ilichukuliqa na shahidi P1

Shajidi: sio P1 sijajua.

Lissu ulisoma maelezo ya P1?

SHAHIDI; Nilisoma

Lissu: Ni kweli kwamba siku hiyo tulikuwa na camera 3 na camera moja aina ya Sony tulikuwa tunarusha mubashara kupitia channel ya YouTube ya Jambo TV.

Kwenye maelezo yake alisema tulipofika makao makuu ya polisi Dodoma ofisa wa polisi alitutaka tukabidi memory card kwa polisi.

Shahidi: ni kweli.

Lissu: kuna shahidi anaitwa P

Ni kweli kwamba yeye kwa kutumia camera ya Sony NX ndiyekuwa akipiga pocha na kurusha mubashara.

Ni kweli kwamba huyo P na wenzake wayatu ndio walisema kwamba wao ndio walikuwa wakifabya live streaming?

Shahidi: ni kweli.

Lissu: Ni kweli kwamba P alisema kwamba yeye ndiyehifadhi jayo mahudhui?

Shahidi: Ni kweli.

Lissu: uliyasoma maelezo ya George Bagyemu

Shahidi: nilisoma.

Lissu: huyo Bagyemu Deputy ZCO alisema hiyo video ilirekodiwa na kurushwa na wafanyakazi wa Jambo TV. Ni kweli

Shahidi: Ni kweli.

Lissu: Ni kweli kwamba hao P na P1 walipewa.maelekezo ya kurekodi mkutabo wangu na Mkurugenzi wa Jambo TV John Marwa na alipewa mwaliko na mkurugenzi wa habari wa Chadema.

Shahidi: Ni kweli.

Lissu: Nimekaa gerezani leo siku 490 mwaka na miezi minne kwa tuhuma kwamba jilichapisha video, wakati monyi mna ushahidi kwam a waliochapisha ni Jambo TV. Nina familia kama wewe, nina watoto niba ndugu hawa. Waeleze majaji huo ndio utendaji wa Jeshi la polisi?

Shahidi; Hao walichapisha P na P1 lakini walialikwa?

Lissu; mimi ndio nauliza maswali, nyamaza. Mlimuhoji mtu yoyote Chadema? Waelwze majaji kama mlimuhoji naibu Katibu mkuu, Golugwa? Mlimuhoji Makamu Mwenyekiti huyo hapo awaeleze Mkurugenzi wa habari ni nani?

Shahidi: Hao ni viongozi wa Chadema na wewe i kiongozi.

Lissu: Kwa hiyo mwenyekiti wa chama anawajibika kijinai na makosa yabayofanywa na viongozi wenzake? Waheshimiwa majaji shahidi ajibu swali langu.

Jaji Ndunguru: jibu swali.

Shahidi: Hawajibiki.

Lissu; Hotuba yangu ilikuwa inahusu matatizo ya uchaguzi mkuu na matatizo yake?

Shahidi: ndio

Lissu: Naomba uwaleze majaji: kwa katiba hii mtu anahamasisha kuzuia uchaguzi anafanya kosa la uhaini.

Shahidi: katiba haijaanisha hilo.

Lissu: Unaifahamu kwamba unaifahamu sheria ya uchaguzi wa rais wabunge na madiwani. Waeleze majaji kama kwa Sheria hiyo inasema ni kosa la jinai kuzuia uchaguzi au kuhamasiaha watu kuvuruga uchaguzi



Shahidi: Sina uhakika sana.

Lissu: Mimi nina uhakika kwamba kwa Sheria hii kuhamasiaha kuvuruga uchaguzi sio kosa lolote? Wewe unasemaje?

Shahidi: wewe umesgitakiwa kwa uhaini.

Lissu: Kabla ya uhaini nimeshitakiwa kwa kuhamasisha kuvuruga uchaguzi.

Jana umeulizwa ukatumia sheria ya Penal code 39(2) d, waeleze waheshimiwa majaji kwamba uhaini ni oamoja na kivururuga uchaguzi.

Lissu: kwenye hayo uliyosoma kunaneno linaloeleza uchaguzi?

Shahidi: Lipo?

Lissu: nauliza tena, una akili timamu?

Shahidi: Ndio

Lissu: ACP. Hicho kifungu kinaeleza mtu anayetishia serikali, Bunge na mahakama. Mimi nilitishia serikali, bunge na mahakama?

Shahidi: wewe ulitishia serikali

Lissu: Nilitishia bunge? Nilitishia, mahakama?

Shahidi: hapana.

Lissu: Anasoma hati ya mashitaka.

Shahidi: Wewe ndio uliyepeleleza hayo maneno.

Lissu: Niambie maana ya serikali.

Shahidi: Ni mamlaka ina mihimili mikuu mitatu, mamlaka, mahakama na Bunge.

Lissu: naomba nimsomee Katiba ya Jamhuri ibara ya 151:1.

Kwenye hayo maelezo, wapi nilitaja Serikali ya Jamhuri ya Muungano?

Shahidi: umeyataja

Lissu: Shahidi una akili timamu?

Shahidi: Ndio.

Lissu; Nimetaja Serikali ya Mapinduzi ya Zanibar? Kuba mahali nimetaja halmashauri ya jiji la Dar es Salaam au jiji lolote? Au halmshauri youote?

Shahidi; umetaja.

Lissu: Waeleze majaji kama nimetaja jina la Rais Samia Suluhu Hassan

Shahidi: Hujataja

Waeleze majaji kama nilimtaja Makamu wa Rais wakati huo, Dk Philip Isidory Mpango na Waziri mkuu Kassima Majaliwa?

Shahidi hapana.

Lissu: Uchaguzi unasimamiwa na chombo gani?

Shahidi; Tume ya uchaguzi

Lissu: Nilitaja Tume ya uchaguzi?

Shahidi: ulitaja mambo ya uchaguzi

Lissu nilitaja Tume ya uchaguzi?

Shahidi; Hapana.



Lissu: Kwenye ushahidi wako kuna Inspekta anaitwa Andrew Churu aliyechukua ile hifadhi ya video na kuleta Dar es Salaam?

Shahidi; Ndio

Lissu: Waeleze majaji kama umesoma maelezobya Inspector Andrew Churu?

Shahidi: nimesoma

Lissu; maelezo Churu kwamba haonwafanyakazi wa Jambo TV ndio waliorekodi na kurusha ...

Shahidi: Ndio

Lissu: Umesoma maelezonya P?

Shahidi: Nimeyasoma.

Lissu: Anasoma maelezo ya P. Shahidi waeleze majaji, mnanitesea mimi nini ikiwa mna ushahidi wa waliofanya hayo makosa?

Shahid: Kazi yangu ni kuthibitisha kosa

Lissu kama hayo wameyasema waliyofanya na polisi wenzako, mnanitesea nini?

Shahidi: wewe ndio umesema hujateswa.

Lissu: Mwaka mmoja na zaidi niko gerezani.



Lissu: Turudi kwenye PGO 1 aya ya 25.

Upelelezi wa makosa unapaswa kufuata sheria. Makosa ni matendo yaliyotajwa na sheria. Swali: Penal code 39 inataja kuvuruga uchaguzi?

Shahidi: Ni kutishia serikalj sio kuvuruga uchaguzi. PGO kila askari polisi ana wajibu kuheshimu haki na uhuru wa wananchi kwa.mujibu wa katiba na sheria za nchi. Kweli?

Shahidi: Ni kweli

Lissu: Haki yangu ya Katiba, ibara ya 15:1.

Waeleze waheshimiwa majaji kwamba ku a mahali popote katika maelezo yako polisi uliheshimu uhuru wangu?

Shahidi; Wewe ulihojiwa na askari wengine

Lissu; hao wengine nilishamalizana nao nakuuliza wewe. Kosa nimeshaeleza mengine hakuna lolote.

Shahidi: Hakuna.

Lissu: Anasoma Ibara ya Ibara 19(1) ya Katiba ya Jamhuiri ya Muungano inayohusu Uhuru wa maoni, mawazo. Mlizingatia uhuru wangu wa mawazo kwenye kazi zangu? Ibara 20 Uhuru wa kukutana na watu wengine kwa uhuru na kutoa maoni yake hadharani kwa amani.

Chama changu kiliitisha mkutano wa watia nia, wakaitisha waandishi wa habari kuna p P1. Mwemyekiti akahutubia. Mlizingatia uhurubwangu wa kukutana a kutoa maoni?

Shahidi: wewe uliitisha Serikali

Lissu: Nimemtisha nani?

Shahidi Serikali.

Lissu; Ndio maana nikasema inawezekana tunazungumza na mtu ambaye ugonjwa wa akili upo.

Lissu: nilisema tune ya uchaguzi ni ya CCM inateuliwa na mwenyekiti wa CCM? NI KWELI

Shahidi: Ni kweli

Lissu; nilisema Tume yabuchaguzi imekuwa na tabia yabkuengua wagombea wa upinzani?

Shahidi: Ni kweli. Nikasema Mheshimiwa Rais Samia ndio amekuwa akielekeza?

Shahidi: Ni kweli.

Jaji Ndunguru ameahirisha kesi hadi saa 8: 10 mchana.
Polisi wanatia Aibu sana...kwa hali hii ndio maana maskini ndio wanafungwa tu kwa kukosa mawakili wabobevu.....
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Leo Agosti 12, 2026

Kesi ya uhaini dhidi ya Mhe. Lissu inaendelea katika Mahakama Kuu ya Dar es salaam ambapo Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross Examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba.

Jana tuliishia part 231 so leo tunaendelea na

Part 232.

Imepigwa high court.

Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.

Mtuhumiwa nae ameingia japo leo Askari Magereza wamemzonga sana ili asisalimiane na watu.

Mtuhumiwa yani Mhe. Lissu amechukua nafasi yake, na shahidi Amini Mahamba amekaa katika kizimba tayari.

Karani anaita kesi kwa namba yake : JAMUHURI dhidi ya TUNDU LISSU

Mawakili wa serikali wanaongozwa na AJUAYE, Katuga, Job Mrema , Cuthbert Mbilingi na Winniwa Kasalla.

Majaji wanamuuliza mtuhumiwa kama yupo tayari…

Mhe. Lissu anaomba kufanya consultation toka kwa Mawakili wake/researchers

Majaji wanamruhusu

Mawakili wake Nashon Nkungu Na Sisty Aloyce wanainuka na kusogea kizimbani kumconsult Mhe. Tundu Lissu wanateka Kama dakika tano hivi kisha wanarudi kukaa kwenye viti vyao.

Jaji anamkumbusha Shahidi kuwa bado yupo chin ya kiapo.

Mhe. Lissu anaruhusiwa aanze kumuhoji Shahidi.

Anamwambia leo hana maswali mengi sana

Anamuuliza kama alidhamiria kuwa maelezo yake aliyotoa alidhamiria yaaminiwe kama ushahidi wa kweli.

ACP Amin Mahamba anajibu kwamba ndio alidhamiria

Mhe. Lissu : Ulidhamiria kuwa maelezo yako uliyotoa kule Polisi yawe ushahidi Mahakamani?

Lissu anasema “IM TYING UP THE LOOSE ENDS”

Anamuuliza kuhusu wale mashahidi waliofichwa waliotolewa mikoani.

Mhe. Lissu : Swala la kwanza eneno hilo; unakumbuka ulisema kwamba hawa mashahidi waliofichwa ni watu waliokamatwa na Polisi ni KWELI walikutwa wakipanga njama?

ACP Amin Mahamba : sio tu kupanga niama, na kuhamasisha

Mhe. Lissu: Walipokamatwa walikiri Polisi kupanga kufanya njama na vurugu Uchaguzi na kadhalika ni kweli??

ACP Amin Mahamba : Hayo yalikuwa ni makosa ya jinai.

Mhe. Lissu: Wakakiri kwa maandshi?

ACP Amin Mahamba : Sahihi.

Mhe. Lissu: Waleleze Majaji hizo tuhuma za kijinai mlizowakamatia ziliishia wapi?

ACP Amin Mahamba : Waheshimiwa rejea maelezo yangu ya siku ya kwanza, kuwa baaada ya watu hao kukamatwa tuliitisha jalada, tukasoma tukapitia.

Mhe. Lissu: Umeelewa swali langu shahidi?
Nimesema sitaki unipotezee muda, nataka kutumia nusu saa.

Katuga anainuka

Kabla hajasema chochote Mhe. Lissu anamwambia kaa,

Katuga anasema si jukumu la Mhe. Lissu kumwambia akae chini.

Mhe. Lissu anakubali na kumueleza Shahidi kuwa akiuliza swal anataka jibu sio hotuba

Mhe. Lissu anauliza kuwa hizo tuhuma za kupanga njama ziliishia wapi?

ACP Amin Mahamba : Baada ya kupitia majalada…

Mhe. Lissu: kweli kuwa mliwafutia kesi wote?

ACP Amin Mahamba : sahihi

Mhe. Lissu : Tuanze na DSM… 29/10.. kulitokea vurugu zilizoua watu 182

ACP Amin Mahamba: Mimi sio msemaji wa Jeshi la Polisi, hizo ni taarifa nyeti.

Kwa mujibu wa Tume ya Jaji Chande watu 182 waliuwawa DSM.

ACP Amin Mahamba : si kweli

Mhe. Lissu: Katika wale watu waliokamatwa wapo wa kutoka Arusha

ACP Amin Mahamba : Kweli

Mhe. Lissu: Walikiri kupanga uhalifu, kupiga watu nk na Mkawaachia,?

ACP Amin Mahamba : Kimya

Mhe.Lissu : Siku ya uchaguzi 29, kwa mujibu wa Tume ya Jaji Chande, waliuwawa watu 53 Arusha, watu ambao mlikuwa mnajua walichopanga mkawaachia, wakaenda kutekeleza hayo.?

ACP Amin Mahamba : Aaah, eeh

Mhe. Lissu : Twende Mbeya, kuna watu mlikwakamata Mbeya, walisema wanapanga kufanya vurugu kwenye Uchaguzi, watapiga watu mawe wakakiri halafu mkawafutia mashtaka kweli si kweli.

ACP Amin Mahamba : KWELI

Mhe. Lissu : Arusha, Dar es Salaam, Mbeya jumla ya watu waliouawa ni 315.

Eleze kama kuna Mkuu wa Polisi, au DC, alichukuliwa hatua kwa uzembe wa maafa haya?

ACP Amin Mahamba : Sina hakika kama kuna aliechukuliwa hatua

Part 233 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Part 233

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba.

Mhe. Lissu : Eleza kama hao waliosema watafanya vurugu, mkawaachia na wakaenda kweli kufanya vurugu kama kuna hata mmoja mliemchukulia hatua?

ACP Amin Mahamba : Kimya

Mhe. Lissu : Kimya maana yake hamkuchukua hatua

ACP Amin Mahamba ; Hapana, nimeona unakumywa maji

Mhe. Lissu : Ninakunywa kahawa

Mhe. Lissu : Mkoa wa Mwanza 29/10 kwa mujibu wa ripori ya jaji chande waliuawa watu 90, eleza kama Mwanza ina RPC?

ACP Amin Mahamba : Yupo

Mhe. Lissu : Yule ambaye yupo kwenye vyombo vya habari kila siku hata gerezani namsikia? Anaitwa Mutafungwa

ACP Amin Mahamba : ndio

Mhe. Lissu : Kwa Mikoa minne watu 405 kwa mujibu wa taarifa ya Chande, kuna aliyechukuliwa hatua?

ACP Amin Mahamba: Sina taarifa

Mhe. Lissu : Kwa Mikoa 7, ni Songea tu mlipopewa taarifa kuwa watafanya vurugu?

ACP Amin Mahamba : Ndio lakini waliachiwa kwa mujibu wa taratibu ya sheria

Mhe. Lissu : Waeleze Majaji kama Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao hawakuripoti wamechukuliwa hatua kwa maafa yalitokea???

ACP Amin Mahamba : Sina uhakika

Mhe. Lissu : Mara ya mwisho watu waliuawa na vyombo kiasi kikubwa hivyo ni mwaka 1905 kwenye Vita ya Majimaji.

Mhe. Lissu anaendelea kueleza awamu zote watu hawakuuawa kiasi iko kama ndani ya wiki 1 ya Samia wameuawa watu wengi

Mhe. Lissu anaelekea kwenye Ushahidi wa video, kwenye ushahidi wako kuhusiana na video, ulisema wewe na timu yako baada ya wewe kupanga timu zako 3, Je video mliyoangalia ilikuwa mtandaoni au ilikuwa kwenye memory card? Au ile iliyokuwa kwenye flash.??

ACP Amin Mahamba; Tuliangalia ile ya kwenye mtandao, Youtube

Mhe. Lissu; Nitakuwa sahihi kusema hamkuangalia ile video ya kwenye flash wala ya kwenye mamory card??

ACP Amin Mahamba ; Hizo hatukuangalia

Mhe. Lissu: Nitakuwa sahihi kusema pengine flash na memory card huenda hazina hata hizo video?

ACP Amin Mahamba ; sio kweli

Mhe. Lissu: umejuaje wakati hujaangalia?

Waeleze Majaji unajuaje kilichokuwa kwenye flash disk wakati hukua.???

ACP Amin Mahamba anakwepa

Mhe. Lissu anarudia

Shahidi umejuaje?

ACP Amin Mahamba: Wenzangu KAAYA na mwenzie walipakua hizo video na kuziweka kwenye flash.

Mhe. Lissu anarudia, swali langu wewe unajuaje kama zipo wakati hujaziona?

ACP Amin Mahamba: najibu kitaalamu sasa,

Mhe. Lissu anamkatiza jibu swal langu

ACP Amin Mahamba : Ngoja nijibu basi, nimefahamu kupitia taarifa ya mchunguzi

Mhe: Lissu: Hiyo taarifa ipo Mahakamani kama kielelezo???

ACP Amin Mahamba : Kimya

Mhe. Lissu anasema mimi nachojua taarifa ilikataliwa hapa mahakamani sababu haikuandaliwa na mtaalamu

Mhe. Lissu: Mpaka sasa wewe ni Shahidi wa 16, na nyie wote hakuna hata mmoja aliyewasilisha ushahidi wa video, taarifa ya uchunguzi wala nyaraka yoyote hakuna.

Mhe. Lissu: Nyaraka zote zilizoingia Mahakamani ni ushahidi wangu,
Mpaka sasa hakuna kilelezeo chochote zaidi ya story kwenye kesi hii.

ACP Amin Mahamba : sina kumbukumbu

Mhe. Lissu: Mkutano wangu ulizungumzia Katiba Mpya?

ACP Amin Mahamba anakataa

Mhe.Lissu : Waeleze Majaji kama unafahamu madai ya Katiba Mpya na mfumo huru wa uchaguzi ni madai yaliyopo kwa miaka 35 hapa Tanzania.

ACP Amin Mahamba : sifahamu

Mhe. Lissu; Eleza kama unafahamu au hufahamu kuwa Tume ya Jaji Nyalali, ilipendekeza itungwe Katiba mpya itakapofikia 1993?

ACP Amin Mahamba : Sijawah kuipitia

Mhe. Lissu: Eleza kama mapendekezo hayo yalikataliwa na Mwinyi?

ACP Amin Mahamba : Sifahamu

Mhe’s Lissu: Mkapa aliunda tume iliyoongozwa na Jaji Kisanga na ikapendekeza kuwe na Katiba mpya halafu Mkapa akasema hadharan mimi sikuwatuma waangalie maswala ya Katiba mpya, unafahamu au hufahamu???

ACP Amin Mahamba : Sifahamu

Part 234 itaendelea kwenye post inayofuata

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Part 234

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba

Mhe. Lissu: Kama unafahamu au hufahamu Tume iliundwa pia ya Mark Boman.. kuangalia utaratubu wa Katiba nayo ikapendekeza kuwe na Katiba mpya na Serikali ya Mkapa na ccm yake ikakataa????

ACP Amin Mahamba : Sifahamu

Mhe. Lissu: Kama hufahamu au unafahamu Kikwete aliunda Tume ya Mabadilio ya Katiba (ya Warioba) ambayo sio tu ilipendekeza Katiba mpya bali pia iliandaa Rasimu halafu Serikali ikakataa???

ACP Amin Mahamba; Sijawah kupitia

Mhe. Lissu: Eleza kama unafahamu au hufahamu tunafanya Uchaguzi Mkuu kila baada ya mikaa 5???

ACP Amin Mahamba : sahihi

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu au hufahamu katika kila Uchaguzi mkuu wa vyamana vingi Watazamaji wa Kimataifa na Kikanda, Jumuiya ya Ulaya, COMMON WEALTH, Marekani., Canada, Japan, AU, SADC, Jumuiya ya Afrika kila Uchaguzi Mkuu wamependekeza kuwa Serikali itungwe Katiba mpya na mfumo mpya wa Uchaguzi ili kuondoa matatizo mengi ya kiuchaguzi???

ACP Amin Mahamba : Sifahamu

Mhe. Lissu Tumeambiwa kila baada ya miaka 5 na ccm imekataa, Eleza kama unafahamu ilani ya ccm ilikuwa na ahadi ya Katiba mara baada ya uchaguzi 2015 na 2020.

ACP Amin Mahamba anajibu haraka SIFAHAMU hata kabla swali halijaisha.

Watu Wanacheka 😀😀😀😀

Mhe. Lissu : Samia alisema Katiba haiweki ugali mezani, unafahamu?

ACP Amin Mahamba ; Sifahamu

Mhe. Lissu: Kwasababu ya kukataa huku kila Uchaguzi mkuu lazima uendane ma maujaji ya Watanzania???

ACP Amin Mahamba -Sina uhakika na hilo

Mhe. Lissu: Eleza Kama baada ya maujaji ya Oktoba 29 mlichukua hatua ya kuniuliza haya maneno yana maana gani, unaposema mtakinukisha una maana gani au haya maneno ya uasi yana maana gani?

ACP Amin Mahamba : Hapana

Mhe. Lissu; Hamkutafuta ufafanuzi wa hayo maneno yangu?

ACP Amin Mahamba : Hukuwa tayari

Mhe. Lissu: Ningekuwa mjinga kiasi gani kujibu nikiwa kwenye pingu?

Mhe. Lissu: Nitakuwa sahihi kusema kuwa No reforms, No election ilikuwa sahihi kwa mazingira yale???

ACP Amin Mahamba : sio sahihi

Mhe. Lissu: Kwa mujibu wa tume ya jaji Chande Ghasia za oktoba 2025 zimetokana na changamoto mbalimbali ambazo hazikutatuliwa, anazisoma kama madai ya katiba mpya.

Waeleze majaji kwamba huo ni msimamo sahihi?

ACP Amin Mahamba ;Unakosea

Mhe. Lissu: kwahiyo hata Jaji Chande alikosea?

Lissu anamsomea sababu kama zilivyo kwenye hotuba ya Jaji Chande.

ACP Amin Mahamba: Sikupata nafasi ya kupitia

Mhe. Lissu: Hayo mnayodai ni makosa yangu, waeleza Majaji kama unafahamu au hufahamu kuwa 13/2/2026, Kikosi kazi cha Kamati ya Umoja wa Mataifa, Kikosi kazi cha Haki za Binadamu, kinachoshughulikia watu wanaokamatwa bure arbitrary detention) kimetoa taarifa na taarifa hiyo inasema kukamatwa kwangu na kushtakiwa huku ni kukuka haki za binadamu na wakapendekeza nilipwe fidia???

ACP Amin Mahamba : sijawah kufahamu

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu au hufahamu mwezi ulipoita 10 july, kamati ya Mawaziri wanaowakilisha nchi za Jumuiya ya Madola imetoa taarifa inayoitaka Serikali ya Tanzania kuniachilia huru bila mashart yoyote ndan ya siku 30 kuanzia 10 july na wakaeleza watatake appropriate action isipofanyika hilo…???

ACP Amin Mahamba : Sifahamu

Mhe. Lissu: Kama Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, Mawaziri kabisa sio wale WANAHARAKATI msiowapenda wanasema aachiliwe ndani ya siku 30 vinginevyo tutawashughulikia, huyu mtu anayepiganiwa na Taasisi hizi ni mtu mbaya anayetakiwa kunyongwa hadi afe?

ACP Amin Mahamba ;Sina uhakika

Mhe. Lissu anamaliza maswali na kukaa chini

Kimya kinaendelea mahakamani kwa muda kidogo

Part 235 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba Nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Part 234

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba

Mhe. Lissu: Kama unafahamu au hufahamu Tume iliundwa pia ya Mark Boman.. kuangalia utaratubu wa Katiba nayo ikapendekeza kuwe na Katiba mpya na Serikali ya Mkapa na ccm yake ikakataa????

ACP Amin Mahamba : Sifahamu

Mhe. Lissu: Kama hufahamu au unafahamu Kikwete aliunda Tume ya Mabadilio ya Katiba (ya Warioba) ambayo sio tu ilipendekeza Katiba mpya bali pia iliandaa Rasimu halafu Serikali ikakataa???

ACP Amin Mahamba; Sijawah kupitia

Mhe. Lissu: Eleza kama unafahamu au hufahamu tunafanya Uchaguzi Mkuu kila baada ya mikaa 5???

ACP Amin Mahamba : sahihi

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu au hufahamu katika kila Uchaguzi mkuu wa vyamana vingi Watazamaji wa Kimataifa na Kikanda, Jumuiya ya Ulaya, COMMON WEALTH, Marekani., Canada, Japan, AU, SADC, Jumuiya ya Afrika kila Uchaguzi Mkuu wamependekeza kuwa Serikali itungwe Katiba mpya na mfumo mpya wa Uchaguzi ili kuondoa matatizo mengi ya kiuchaguzi???

ACP Amin Mahamba : Sifahamu

Mhe. Lissu Tumeambiwa kila baada ya miaka 5 na ccm imekataa, Eleza kama unafahamu ilani ya ccm ilikuwa na ahadi ya Katiba mara baada ya uchaguzi 2015 na 2020.

ACP Amin Mahamba anajibu haraka SIFAHAMU hata kabla swali halijaisha.

Watu Wanacheka 😀😀😀😀

Mhe. Lissu : Samia alisema Katiba haiweki ugali mezani, unafahamu?

ACP Amin Mahamba ; Sifahamu

Mhe. Lissu: Kwasababu ya kukataa huku kila Uchaguzi mkuu lazima uendane ma maujaji ya Watanzania???

ACP Amin Mahamba -Sina uhakika na hilo

Mhe. Lissu: Eleza Kama baada ya maujaji ya Oktoba 29 mlichukua hatua ya kuniuliza haya maneno yana maana gani, unaposema mtakinukisha una maana gani au haya maneno ya uasi yana maana gani?

ACP Amin Mahamba : Hapana

Mhe. Lissu; Hamkutafuta ufafanuzi wa hayo maneno yangu?

ACP Amin Mahamba : Hukuwa tayari

Mhe. Lissu: Ningekuwa mjinga kiasi gani kujibu nikiwa kwenye pingu?

Mhe. Lissu: Nitakuwa sahihi kusema kuwa No reforms, No election ilikuwa sahihi kwa mazingira yale???

ACP Amin Mahamba : sio sahihi

Mhe. Lissu: Kwa mujibu wa tume ya jaji Chande Ghasia za oktoba 2025 zimetokana na changamoto mbalimbali ambazo hazikutatuliwa, anazisoma kama madai ya katiba mpya.

Waeleze majaji kwamba huo ni msimamo sahihi?

ACP Amin Mahamba ;Unakosea

Mhe. Lissu: kwahiyo hata Jaji Chande alikosea?

Lissu anamsomea sababu kama zilivyo kwenye hotuba ya Jaji Chande.

ACP Amin Mahamba: Sikupata nafasi ya kupitia

Mhe. Lissu: Hayo mnayodai ni makosa yangu, waeleza Majaji kama unafahamu au hufahamu kuwa 13/2/2026, Kikosi kazi cha Kamati ya Umoja wa Mataifa, Kikosi kazi cha Haki za Binadamu, kinachoshughulikia watu wanaokamatwa bure arbitrary detention) kimetoa taarifa na taarifa hiyo inasema kukamatwa kwangu na kushtakiwa huku ni kukuka haki za binadamu na wakapendekeza nilipwe fidia???

ACP Amin Mahamba : sijawah kufahamu

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu au hufahamu mwezi ulipoita 10 july, kamati ya Mawaziri wanaowakilisha nchi za Jumuiya ya Madola imetoa taarifa inayoitaka Serikali ya Tanzania kuniachilia huru bila mashart yoyote ndan ya siku 30 kuanzia 10 july na wakaeleza watatake appropriate action isipofanyika hilo…???

ACP Amin Mahamba : Sifahamu

Mhe. Lissu: Kama Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, Mawaziri kabisa sio wale WANAHARAKATI msiowapenda wanasema aachiliwe ndani ya siku 30 vinginevyo tutawashughulikia, huyu mtu anayepiganiwa na Taasisi hizi ni mtu mbaya anayetakiwa kunyongwa hadi afe?

ACP Amin Mahamba ;Sina uhakika

Mhe. Lissu anamaliza maswali na kukaa chini

Kimya kinaendelea mahakamani kwa muda kidogo

Part 235 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba Nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
Ahsante mkuu
 
Back
Top Bottom