Lissu alivyomkaanga Mpelelezi Mkuu wa kesi yake

This is wastage of time, hakuna shahidi hapa, shahidi haju why yuko hapo on top of that hajui kesi inayoendelea and has no clue kuwa kujifanya afisa wa serikali ni jinai.
 
Huyo atakuwa kagushi identity. Subiri tu
Sema kama ni kweli serikali italizima hili jambo Leo Leo.

Ila kama mahamba ameshafariki na mahamba huyu ni mtumishi hewa lissu aweke cheti cha kifo na , force number na vyeti vya elimu.. hapo ngoma itakua NGUMU.

Hiii inaitwa shahidi batili kutoa Ushahidi batili kwenye kesi batili....
 
Lissu: Nimemtisha nani?

Shahidi Serikali.

Lissu; Ndio maana nikasema inawezekana tunazungumza na mtu ambaye ugonjwa wa akili upo.

Lissu: nilisema tune ya uchaguzi ni ya CCM inateuliwa na mwenyekiti wa CCM? NI KWELI

Shahidi: Ni kweli

Lissu; nilisema Tume yabuchaguzi imekuwa na tabia yabkuengua wagombea wa upinzani?

Lissu : Ni kweli. Nikasema Mheshimiwa Rais Samia ndio amekuwa akielekeza?

Shahidi: Ni kweli.


Hawa vidampa wa policcm hakika ni weupe kichwani.
 
Tatizo sasa hivi inabidi mtu achague sana maneno kutoa ushauri kwa sababu hao unaowashauri wao badala wachukue ushauri wautafakari wachukue ya maana wafanyie kazi na mabaya wayaache. Wao wanachokifanya ni tofauti kabisa. Matokeo yake sasa kila mtu anaogopa kutoa ushauri wa maana.

Haya yanayoendela mahakamani sio mageni na yalijitokeza hata kwenye kesi ya Mbowe mpaka baadhi ya mashahidi wakawa wanaomba poo kwenda kujisaidia katikati ya kesi kutokana na maswali magumu ya mawakili. Vipi tena hawakujifunza kwa yakliyojitokeza kwenye kesi ya Mbowe wanakuja kuleta tena kwenye kesi ya Lisu japo ni kesi tofauti. Kama kuna mtu anaamini kuwa wanaoabika pale mahakamani ni wale mashahidi tu anakosea sana kwa aibu ile inakwenda kwa serikali na watanzania wote kwa ujumla.

Naamini wizara ya sheria na hususan idara ya mahakama ina wasomi wazuri sana na wanaelewa mambo. Je huwa wanashauri vipi wanasiasa kwenye issue kama kesi ya Lisu. Je wanasiasa wetu nao wanajua kuwa siku hizi kuna mitandao kibao inatafsiri kila kitu kwa sekunde chache sana kwa hiyo kinachoendelea pale mahakamani kinafika duniani kwa lugha zote kwa dakika chache sana. Tukumbuke kuwa kuna balozi za nchi mbali mbali dunia zipo hapa kwetu na zinapeleka taarifa halisi kwao. Hivi hao wageni tunawaita washirika wenzetu kwenye maendeleo wanatuonaje kama taifa kwa haya yanayoendela nchini na hasa mahakamani? Aibu nyingine tunaweza kuziondoa tu kwa utashi wetu wenyewe sio mpaka washirika wenzetu watupe ultimatum.

Jamani hata kama hamtuhurumii sisi tunaoishi sasa hivi basi kihurumieni kizazi kijacho. Hivi kuna kiongozi yoyote amewahi kufikiri nje ya uanasiasa wake na madaraka yake ya sasa kuwa watoto wetu wote wataishije miaka michache tu ijayo wakati sisi hatupo. Je hii mbegu mbaya inayopandwa leo kwa kiburi cha siasa na madaraka ikiota ikamea vizuri wameshawahi kufikiri madhara yake yanaweza kuchukua miaka mingi kurekebishwa au inaweza kutokea kabisa kushindwa kurekebishika hivyo kusambaratisha taifa kwa ujumla. Hivi tunajifanya kabisa hatujui nini kilisamabaratisha baadhi ya mataifa duniani?

Hebu tukae chini kama watanzania tukiri pale tuliposea, tuwajibike tulipokosea, turekebishe pale tulipokosea. Kukiri kukosea na kuwajibika sio udhaifu bali ni njia yakujirekebisha na kurudi kwenye mwelekeo sahihi kama Taifa

Nikimnukuu Mhe. Mbatia; hebu tumtendee haki mama Tanzania.

Ni mtizamo tu.
 
Ni maeneo yote, mkuu 'Tindo',siyo serikalini pekee.
Wewe tazama fani ya ualimu inavyovurugwa.

Hii haina maana kuwa hakuna wenye uwezo mzuri huko, bali kwa kuwa kuwa na uwezo hakulipi; basi wote wanaamua kufuata uozo inaousambaza CCM, ili mradi tu waendelee kupata chochote.
Ufanisi wa taaluma siyo sifa tena ya kujivunia Tanzania.

Si unawaona akina Makonda, akina Wanu Hafidh Mchengerwa?
 
Tungekuwa na utaratibu wa kukaa chini na kutafakari kwa kina kama taifa, haya ndiyo yangetukalisha chini na kuyatafakari kwa kina bila ya papara na mihemko ya aina yoyote.

Tanzania imewekwa katika hali ngumu sana, tena wakati wenye mabadiliko makubwa duniani sasa hivi kiteknolojia.

Tutaujutia sana muda huu muhimu tulioupoteza.
 
Ndio maana nikasema huko serekalini. Yaani kuna watu wana uwezo duni ajabu.
 
Dah! Hatari sana mawakili wa serikali watakuwa walitamani kukimbia maana shahidi hali tete na ndiye aliyekuwa shujaa wao jana
Halafu huyo jamaa anajibu kwa dharau ile mbaya, maana anajua ni kesi yenye backup ya utawala. Ni basi tu wako mahakamani, lakini hajali maana anajua mahakama iniaagizwa kama yeye. Hata hao mawakili wa serekali wanajua kabisa huyo shahidi kwa Lisu hatoboi, ila wanapata ahueni kuwa ni kesi yenye mkono wa rais.

Najua kwa vyovyote hapo polisi wanajikaza ili walio chini yao wasiwadharau, na watakachofanya kwani hawamuwezi Lisu mahakamani, wataagizwa kumuumiza akiachiwa. Na huyo shahidi ni mmoja ya wana usalama wanaoratibu kundi la watu wasiojulikana.
 
Hizi kesi za kizushi zimeliumbua sana jeshi la polisi, kwa jinsi mashahidi hawa ambao ni askari polisi imedhihirisha kuwa jeshi la polisi ni moja ya taasisi ya serikali inayoajiri watu wenye upeo mdogo sana wa akili, form IV failures.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…