PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo Ijumaa Julai 3, 2026, ambapo anatarajiwa kuchuana na jopo la mawakili wa Serikali kwa hoja za kisheria wakati wa usikilizwaji wa shauri lililofunguliwa dhidi yake na Jamhuri, kuhusiana na kesi ya uhaini inayomkabili.
Jamhuri ilifungua shauri hilo la maombi ya mapitio Februari 24, 2026, ikipinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, kuikatalia maombi yake ya kutaka iruhusiwe kuwasilisha ushahidi wa nyongeza katika kesi ya uhaini inayomkabili mwanasiasa huyo.
Soma: Rufaa ya Jamhuri katika kesi ya Lissu kusikilizwa leo (Julai 3, 2026) baada ya shauri la msingi kusimama kwa zaidi ya miezi minne
Shauri hilo la mapitio namba 7203216/2026 limepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani litakaloketi Dar es Salaam, linaloongozwa na Jaji Augustine Mwarija, Majaji wengine ni Zainabu Muruke na Amour Khamis.