Sikupi 'like' pamoja na kwamba ninakubaliana na uliyo eleza kwenye mistari ya kwanza kabisa huko juu.Burundi wameuwana miaka na miaka kuna mabadiliko gani?
Uganda wameuwana mbona M7 amefanya uganda 🇺🇬 kuwa mali ya familia?
Rwanda wameuwana mbona hata kauhuru uliko nako chini ya ccm Rwanda hakuna?
Dubai, Qtaar, Denmark, Malaysia,Indonesia waliuana lini mpaka wakapata hayo maendeleo walio nayo?
Tatizo la nchi hii sio ccm bali tatizo la nchi hii ni mfumo mzima wa jamii yetu kiufupi jamii ya kiafrika ni jamii iliyo jaa upumbavu mwingi.
Sasa inashangaza kutaka kupata viongozi bora kutoka ndani ya jamii ya wapumbavu.
Nataka nikuhakikishie hata leo ikatokea ccm ikatoka madarakani kikaingia chama kingine hakuna kitakacho badilika chochote ndani ya nchi hii.
Sikubaliani na wewe hata mara moja kwa maoni uliyo maliza nayo kwenye mistari yako ya mwisho; na ndiyo yaliyonipa msukumo wa kukujibu hapa.
"Viongozi bora" wamo ndani ya jamii unayoiita wewe ya "wapumbavu".
Na ili kusisitiza wewe ni mtu wa aina gani, huo mstari wako wa mwisho sijui kama kweli ulitaka kuuweka kama ulivyo uweka hapo. Pengine hii ni ishara tu ya kukuelezea mwenyewe kunakokuhusu mwenyewe; ndani ya himaya ya hao wapumbavu wa CCM.
Nchi hii pamoja na umaskini wetu tumekuwa na wakati wa heshima sana kama taifa. Tumeshiriki kikamilifu katika ukombozi wa mataifa yaliyokuwa chini ya ukoloni kwa heshima kubwa.
Tumejenga umoja kati yetu, mshikamano uliotufanya kuwa mfano kwa mataifa chungu nzima; halafu leo unakuja hapa na kutoa dharau za kipuuzipuuzi kwa vile mmevuruga yote yaliyowekwa na waasisi wa nchi hii?
Hao hawakuwa waTanzania. Hawakuwa viongozi wa kuheshimika?
Tutawapata viongozi watakao tusukuma mbele kama taifa, na waTanzania sina shaka yoyote wataijenga nchi yao na kujiletea maendeleo wao wenyewe. Kama hayo mataifa uliyo yataja hapo, ya waarabu na hao wengineo. Leo unamwona Mwarabu kuwa mtu wa maana zaidi kuliko mtu mweusi?
Nenda kawaambie hao waliokutuma (akina Samia na Genge lake) kuja kuwadharau waTanzania hapa kwamba siku zao zinahesabika. In fact, umetumia mifano ya Museveni na Kagame; kwa sababu huko ndiko Samia anakochota uzoefu na kudhani atafanikiwa kutufanya mifugo yake kama hao wenzake.
Hatafanikiwa.