Pre GE2025 Lissu: Aliyemleta Abdul kunihonga anagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti na anamuunga mkono 'Mwenyekiti'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tanzania tunahitaji mtu kama TAL mtu ambaye uongo kwake mwiko, mtu ambaye hana bei ya kumnunua.
 
Miafrica minafiki Sana Trump kampeni zake nyeusi nyeusi nyeupe nyeupe na anashinda Lissu akiwaambia ukweli eti anakuwa mropokaji

Ngoja muone chadema inavyoenda kufa kifo kibaya kuliko hata udp
 
Kiongozi lazima awe mwajibikaji.

Wengine wanajiudhulu kabisa kisa matendo maovu wewe unazungumzia kusema tuu
We unadhani kuna wabunge wangapi na wanajua mangapi wenye acess na internet ya kuingia JF na kuropoka.

Au kuna watumishi wangapi wa umma wana-ona upuuzi unaondelea kwenye wizara zao na wanajua namna wanavyomulikwa.

Jerry akiwa meya wa Dar aliwahi sema kuhusu madawa ya kulevya, ‘ mimi jicho moja naona’ serikali macho yote aoni’ vitu vingine elewa.

Kiongozi wa chama anajukumu la kulinda imani ya chama chake mbele ya wananchi, mnyukano wa ndani upo. Iła vitu mbinu bila ya kuharibu reputation ya chama.

Kwetu kumekucha 👋
 
Wewe unatak rushwa iendelee kuchukukuliwa uko ndo uozo wa chama ndani uko nje unapaka mafuta lazima transparency ni muhimu kwenye siasa za chama hiyo sio jambo la kificha
 

Kama imani ya chama ni uhalifu na maovu Basi chama kinahaki zote kulinda uovu na uhalifu na wanaofanya mambo hayo.

Ninyi ndio mkiwa mahakimu au majaji mtalinda watawala ati kisa ni viongozi wa nchi.

Baadhi ya maoni ya wadau humu kama haya yanatoa picha tupo kwenye jamii ya aina gani.

Yaani ulinde maovu au muovu kisa mpo chama kimoja au dini Moja😂😂
 
Mbowe awe makini Sana kwani Lisu muda Siyo mrefu anakwenda kumwaga mboga, hasara itakuwa kwa Mbowe na CHADEMA kwa Ujumla , Lisu Hana chochote cha kupoteza maana hakuna chochote amewahi kunufaika nacho katika hizo biashara za chinichini hapo CHADEMA
SIASA NI KAMA DINI TU WATU WAKIKUAMINI HATA UCHAFUE VIPI HAWAKUSIKII YAANI WATU KWA MBOWE HATA USEME ANAKULA WATU HAWATA KUELEWA WATAMCHAGUA TU
 
Kama hii ni kweli basi anafanya kazi nzuri sana ya wapinzani wake wakuu. Kuna mambo ya wananchi na kuna mambo ya wanachama. Sio kila kitu unaongea in public. Kama mume wako ni kikojozi, kumtangaza hadharani hakutasaidia kitu.

Anapomuunganisha Wenje na Mbowe anatuambia kuwa ile rushwa ilikuwa na baraka za Mbowe. Kuwa Mbowe amekuwa analipwa na wakina "Abdul" miaka yote hii. Hizi ni tuhuma nzito sana. Ingawa wana tofauti zao lengo kuu linatakiwa kukiacha chama chake salama baada ya uchaguzi. Kama ni kweli anayosema kuhusu Wenje angemshughulikia baada ya uchaguzi. Kwa kumshutumu Mbowe kwa mafumbo anajiharibia kwa wale wenye imani nae. Kama ana ushahidi wa dhati kuwa Mbowe analipwa na CCM aseme wazi wazi ili wananchi wamjue na wampe adhabu atakayokuwa anastahili.

Anachofanya sasa ni kuleta mpasuko katika chama ambao itakuwa vigumu kuuziba. Mwisho wa siku faida itakuwa kwa CCM maana kuna watu wa CDM watakaoona bora wajikalie nyumbani kuliko kumpigia kura kama atagombea urais. Anachokifanya sio kizuri kwa mustakabali wa chama chake.

Scorched earth tactics hazijawahi kumuacha mtu salama. Ego yake inampeleka pabaya. Na akiwa Mwenyekiti tusubiri purge na witch hunt kubwa katika chama chake.

Yetu macho.

Amandla...
 
Lisu hata kama sio kiongozi mzuri lakini ndio Mwenye saport kubwa ya wananchi, na Mbowe anasapoti kubwa ya wajumbe aliowatengenezea mazingira washinde. Sasa ni either chama kibaki makao makuu au mkipeleke kwa wananchi uchaguzi ni wenu.
 
Wewe tunajua unaclmchukia Lissu sababu alimnyoosha Magufuli na wewe ni mfuasi wa Magufuli kindakindaki
 
Acheni aanike uovu na Wala rushwa bila kujali unafanywa na nani?. Ni either mumchague Mbowe chama kibaki ofisini au mumchague Lissu chama kiende kwa wananchi uchaguzi ni wenu.
 
Kuna wanasiasa wapumbavu pia na kuna siasa za kipumbavu pia wewe itakuwa unazungumzia wanasiasa wapumbavu na siasa za kipumbavu..maana katika siasa na wanasiasa wapumbavu ndiyo ufuata hiyo kanuni yako...nimesha gundua naongea na mtu mpumbavu pia
 
Probability of an event to occur is 0.95.
 
Endeeli kuvuana chupi tuone tupu zenu.

Wanasiasa ni washenzi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…