Pre GE2025 Lissu: Aliyeshika chupa ya damu nikipelekwa Nairobi ni Msigwa (sio Mbowe)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona hizi habari za chadema zimeshika kasi humu... kwani kunanin
Ni chama kikubwa cha kitaifa . Lazima kipite kwenye moto kabla ya kukikabidhi nchi.

Tunataka katiba mpya. Tukiwa na Katiba mbovu kama iliyopo tutakuja kuwa na Kunguni badala ya Chawa wa sasa.

Rais akiwa ndiye mwenyekiti wa Chama na amiri jeshi mkuu mambo hayaweza kwenda zaidi ya kisifia siafia mpaka vitu vya kipuuzi
 
😂 😂 😂
Kwani Mbowe alishwahi kusema yeye ndio aliyeshika CHUPA?
Halafu harakati za Lissu sasa hivi anazifanya kwa kivuli cha chama gani?
Hebu wana JF muwe na Fikra pevu basi.

..Abduli na Maza ake wako kazini.

..ukiona kiongozi wa Cdm anashambuliwa sana na Ccm ujue yuko site anafanya kazi.
 
Ni swala la muda tu, ccm wataipasua chadema

Sidhani kama wataweza.

Labda wamhadae Mbowe na mambo ya maridhiano, na yeye ahadaike. CCM haina dhamira ya maridhiano wala dhamira njema na Taifa hili. Kilicho muhimu kwao ni kuhodhi madaraka. Kungine kote ni hadaa tupu. Wanawahadaa wananchi, wanavihadaa vyama vya siasa, wanawahadaa mataifa wafadhili, wanawahadaa viongozi wa dini, wanayoyanena vinywani mwao, hayamo katika dhamira zao. Ndiyo maana utawasikia wanasema wanapiga vita rushwa lakini CCM ndiyo walaji wakubwa wa rushwa. Utawasikia wanapiga vita ufisadi lakini ndiyo majizi wakubwa. Utawasikia wakisema watu watendewe haki lakini ndiyo wadhulumaji wakubwa wa haki za watu.

Hatua ya kwanza ya kupiga hatua Taifa hili ni siku ile watu watakapoondokana na ukoloni wa CCM.
 
Unajuwa mtu akiwa anatafuta talaka, kwanza anatafuta huruma na malalamiko mengi kama alikuwa anateswa sana wakati utakuta amekaa kwenye ndoa miaka 20 leo ndio anakumbuka talaka ndio haya ya Lissu na Chadema, hakuna haja ya kutafuta huruma hutaki chama unasema tu au unataka kugombania nafasi ya juu gombania chama kitaamua hii ndio democracy.
 
Kwa hiyo mtu yoyote uko Chadema akiwa tofauti na fikra za Mbowe anakuwa hataki chama anaoneshwa mlango wa kuondoka?
 
Itakuwa na maana kubwa iwapo ukiwa wewe sii chademaphobia🤔
 
na bado atatajwa tena mwingine aliyezibeba zile nguo zilizoloa damu
 
Acha uongo tulimsikia akiongea
Hakuna mahali alisema sio Mbowe alie beba chupa. After all alikuwa ame zima
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kwani Mbowe alishwahi kusema yeye ndio aliyeshika CHUPA?
Halafu harakati za Lissu sasa hivi anazifanya kwa kivuli cha chama gani?
Hebu wana JF muwe na Fikra pevu basi.

Hata ukisema alichokijenga kwa jasho na damu utakuwa hujakosea mwana jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…