Ningependa niweke wazi na Watanzania wakielewe, sijawahi kuomba kuwa mwenyekiti kwa mtu yeyote, mwaka 2004 nilikuwa Mwenyekiti baada ya wajumbe wa kamati kuu na wazee wa Chadema kunipendekeza kutokana na historia na commitment yangu ya chama.
Nilianza harakati za kuijenga Chadema baada ya kuona kinasinzia mwaka 2000, nikiwa na Dk. Wilbrod Slaa na wengine watatu, tulitoa magari yetu tukatembea nchi nzima kufanya mikutano. Nikaenda vyuo vikuu kutafuta wanafunzi walioonesha mwelekeo wa kuwa viongozi.
Credit: Mwanahalisi