Lissu amelalamikia watu wake kuzuiliwa kesi imesimamishwa kwa muda

Lissu amelalamikia watu wake kuzuiliwa kesi imesimamishwa kwa muda

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),. Tundu Lissu, inaendelea leo, Jumatatu Oktoba 06.2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam ambapo kwa mara ya kwanza Mahakama inatarajiwa kuanza kusikiliza ushahidi kutoka upande wa Jamhuri

Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa usikilizwaji wa ushahidi huo, mshtakiwa Lissu ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo ameomba Mahakama impatie ufafanuzi kuhusu masuala mawili aliyoyawasilisha Mahakama hapo leo, akisisitiza kwamba hoja hizo ziwekwe kwenye kumbukumbu za Mahakama kama inavyokuwa kwa hoja nyingine

Soma pia: Wawakilishi wa Marekani na New Zealand wazuiliwa kuingia kwenye kesi ya Tundu Lissu

Katika wasilisho lake, Lissu amesema kuwa Septemba 30 mwaka huu, Naibu Msajili wa Mahakama Livin Lyakinana amemwandikia barua kupitia Mkuu wa Gereza la Ukonga, barua hiyo ambayo aliipokea Alhamisi ya Oktoba 02.2025 ilimuelekeza awasilishe orodha ya watu 100 ambao angependa wahudhurie mwenendo wa kesi hiyo, wakiwemo Mawakili, viongozi wa chama chake, wanachama na ndugu zake

Anasema Mahakama kupitia barua hiyo ya Naibu Msajili ilielekeza kuwa orodha hiyo iwasilishwe ifikapo Oktoba 03.2025 kabla ya saa 12 jioni

Lissu ameendelea kueleza kuwa kutokana na mazingira ya yeye kuwa gerezani, alikuwa hana mawasiliano na Mawakili, ndugu wala viongozi wa chama, hata hivyo licha ya changamoto hizo alijitahidi kuandaa na kuwasilisha majina hayo ndani ya muda uliotolewa na Mahakama

Akizungumza mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wanaosikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Jaji Dastun Ndunguru, Lissu amedai kuwa baadhi ya watu aliowapendekeza kuhudhuria kesi hiyo wamezuiwa kuingia Mahakamani hapo akiwemo Dkt. Stephan kutoka Ujerumani na Dkt. Cathe kutoka Uingereza, ambao walikuwa wamefika kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo

Aidha, amedai kuwa baadhi ya wananchi waliokuwa nje ya Mahakama walipigwa na maafisa wa Jeshi la Polisi, jambo alilolielezea kama ukiukaji wa Haki za Kikatiba za wananchi kuhudhuria mwenendo wa kesi za wazi

Kesi imeahirishwa kwa muda wa dakika 30 kwa ajili ya kutolewa maelekezo na muongozo wa Mahakama.
 
Nahani title ingepaswa kuwa mkanganyiko wa ratiba ya kesi unaoonesha mwenendo wa kesi hadi tarehe ya hukumu jambo ambalo linaifanya kesi kuonesha iko controlled nje ya Mahakama
 
Kesi imeahirishwa kwa muda wa dakika 30 kwa ajili ya kutolewa maelekezo na muongozo wa Mahakama.
Majaji mpaka wakapige simu kwanza huku wanachekea chooni ndio waje kutoa maamuzi baada ya dakika 30, hakuna Mahakama hapo maigizo ni meengi sana
 
Back
Top Bottom