Mister mimi
Member
- Apr 29, 2018
- 89
- 106
Kwanza,kwenye chama chake tu kuna watu zaidi ya 40% hawamkubali,hiyo imethibitika kwenye uchaguzi mkuu wa chama,hata kama atapambana kuwarudisha, hutawarudisha wote.wengine atakua nao ila hawatakua upande wake abadani,na huo ndio ukweli akubali ukatae!
Hoja ya kugomea uchaguzi na kutangaza kuzuia uchaguzi mapema hivi ni dalili ya uoga na kukubali kushindwa mapema sana,yani umetupa taulo hata kabla hujaingia ulingoni.maana kama hoja ni katiba na tume tu inabidi utuambie kwanza wakati ulipokua mbunge ulitangazwa mshindi kupitia katiba na tume za namna gani?
Je kama tume zilikua hazitendi haki,je na wewe ulipokua mbunge ubunge uliupata kinyume na haki? Tambua kuwa sibezi hitaji la katiba na tume bora yenye kujisimamia.ila kususia uchaguzi kwa hoja hiyo ni kichaka cheupe sana ikiwa viongozi wengi tu ukiwemo wewe mwenyewe ulitangazwa mshindi na tume hizo hizo tunazozilalamikia.
Vijana wengi saizi ni ccm tena CCM haswa,kwanini vijana wengi wanakua CCM,kwa sababu wanajionea ukiwa CCM kuna chochote kitu unapata,japo hili hutakubaliana nalo ila haitabadilisha ukweli.vijana saizi wanataka hela,na wanaelewa vyama vyote vina hela.wanaona vijana wenzao waliopo CCM wanavyopata hela na fursa,sasa yeye aendelee kufanya siasa za kuchangisha wanachama bila kuwaeleza fungu la ruzuku lime limefanya kazi gani! Ujinga una mwisho(sisemi kwa ubaya bali hoja).
Siasa ni watu na CCM inatafuta watu usiku na mchana,majumbani,makanisani,misikitini,michezoni.popote palipo na watu CCM ipo na ina watu wake hapo.na yote inayofanya CCM hakuna chama kinazuiliwa kufanya.nyinyi endeleeni kujifungia ofisini mkitoka mnatangaza migomo na kuwatukana wahamasishaji na washawishi wa ccm kuwa ni machawa.haya! Machawa hao hao wanasepa na kijiji! Mkija kushtuka kuwa mliokuwa mkiwabeza na kuwakashifu kumbe wana umuhimu, kumekucha!
Lingine niwambie CHADEMA kuwa wasiishi wakati uliopita,maana katika wakati huu wapenzi wao wengi iliokuwa nao chaguzi mbili mpaka tatu zilizopita,wengi wao wamevujwa mioyo sana na mienendo ya viongozi wao wa juu tatika hizo chaguzi,na ukweli wengi wamejiunga au wamehamia ccm na wengine kuchukia na kuachana kabisa na siasa.
Na kosa lingine analofanya mwenyekiti mpya CHADEMA ni kutangaza hadharani hahitaji muungano na chama kingine.anaamini yeye ndio yeye na anaweza peke yake,wakati hata ccm wanapambana kuungwa mkono na vyama vingine yeye anagoma.yaani unafanya siasa halafu hutaki watu wakuunge mkono.
CCM ukiona hawamtaki mtu ujue huyo mtu hawaungi mkono na amegoma kubadilika au kushawishika.
Na katika hili CCM wameweza sana,wamewekeza sana katika watu,wapo karibu sana na watu,kutoka ngazi ya taifa hadi ubalozi wa nyumba kumi,na inawalipa!
Huu ndio ukweli japo ni mchungu.
Sisi CHADEMA tuendelee kujifungia ofisini, tukitoka tunaita waandishi wa habari,tunakashifu vyama,viongozi wa nchi,wa dini,wa taasisi,wasanii na wote wanaoiunga mkono CCM kana kwamba wanachofanya ni ni kosa kikatiba.,
Tuendelee kutafuta kuhurumiwa huku tunatangaza migomo na fujo kisha tunaomba michango mwisho tunagawana posho za ruzuku, tupanda V8 zetu nyumbani kutulia na familia zetu tukiendelea kufuatilia maoni ya wanachama wetu mitandaoni.wakati ccm wako mtaa kwa mtaa nyumba kwa nyumba wakihamasisha watu kujiandikisha na kuwaunga mkono!
Na hakika wanawapata! Maana
Siasa ni sanaa na sanaa ni kazi! Naona wengi wapo kazini kushawishi,wachache wanatia huruma kukashifu na kutukana(timing mbovu kabisa).
Muda ambao unatakiwa kuji-brand unampaisha mshindani kwa kumtajataja kila ulipo.
Mgonjwa hakatai dawa, akikataa dawa ujue hali ni mbaya!
Mida!