Pre GE2025 Lissu anaipa ushindi CCM mapema sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CHADEMA IMEPOTEZA MVUTO SANA
 
Ungesikiliza hoja alizotoa Lissu usingeandika huu ushubwada wako,wewe ni chawa wa Mbowe bado unaomboleza
Mbowe kaacha wajinga wengi ndani ya chama lisu ana kazi kubwa sana , huwa naumia hasa napoona kuwa mtu kama ntobi alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa shinyanga, watu wenye kariba kama ya ntobi hawakujitokeza kipindi cha kampeni kwenye uchaguzi wa ndani lakini wamo wengi sana, lisu ana kazi kubwa kutoa elimu na kufanya reform ndani ya chama
 
Lisu awekeze zaidi Kwa vijana.
 

..mimi nayakubali sana mawazo yako tofauti na wengine wanaokushambulia.

..Kuhusu Tume Huru ya uchaguzi tujifunze wenzetu ambao wanayo lakini haijawapa matokeo mazuri wamekosea wapi.

..Mapungufu au ukosefu wa matokeo chanya Ghana, Malawi, Zambia, isitukatishe tamaa katika nia yetu ya kuunda Tume Huru ya uchaguzi.
 
..CCM ina mapesa mengi sana.

..kila mwezi wanapewa BILLION 3.2 kama ruzuku.

..wanaofaidika na fedha hizo ni Chawa wachache, miongoni mwa kundi kubwa la vijana masikini.

..kuna vijana wengi sana hawana ajira, na hawapati fursa zozote ndani ya CCM.
Unacho sema ni sahihi lakini hao asilimia kubwa ya vijana wasiyo pata chochote ndiyo wako kimbele kuwapigia CCM kura. Mimi nimeona kwenye uchaguzi wa mitaa wa mwaka huu vijana wengi sana wamepiga sura hasa wakilaani kuusu wabunge ambao waliwapigania 2015 halafu wakawauza. Kwahiyo wanaona upinzani nikichaka tu chakutafutia umaarufu ukishapata umaarufu unanunuliwa na ccm. Mimi kwa masikio yangu niliwasikia vijana watemeke navkinondoni wakiulaani upinzani kwa usaliti ulio wafanyia. Wakati viongozi wengi wa CCM ni jamaa zao wa karibu.
 

..unadhani kwanini hizo nchi hazijafanikiwa pamoja na kuwa na Tume Huru?
 

..CCM imeshindwa kutoa majibu kwa tatizo la ukosefu wa ajira na fursa kwa vijana.

..inawezekana kabisa kwamba vijana bado wana matumaini kuwa CCM itawafaa.

..lakini ukweli ni kwamba ya CCM ktk kuleta maendeleo haiendani na kasi ya ongezeko la vijana wanaohitaji msaada wa serikali.

..tukiendelea kwa mtindo na utaratibu huu wa CCM taifa linaweza kuingia katika matatizo makubwa.
 
..CCM ina mapesa mengi sana.

..kila mwezi wanapewa BILLION 3.2 kama ruzuku.

..wanaofaidika na fedha hizo ni Chawa wachache, miongoni mwa kundi kubwa la vijana masikini.

..kuna vijana wengi sana hawana ajira, na hawapati fursa zozote ndani ya CCM.
Ni kweli ccm wana hela nyingi,wana miradi,wana wafadhili na zingine wanaweza kuwa wanajichotea kwa sababu wako jikoni.lakini hii bado haijawapa kiburi cha kuacha kubembeleza na kushawishi watu wawaunge mkono.

Hata chadema wanapokea ruzuku,
Hata chadema wana wafadhili.

Je,lisu hanufaiki na hizo fedha?
Je ni kosa chama kutumia fedha zake kuwalipa watu wenye ushawishi kujiongezea watu na umaarufu?

Mi nafikiri chadema na wao wanatakiwa kubadilika,kutenga fungu la wasanii kwenye kila idara,wasanii,vyombo vya habari kote huko watu wako kazini,wanatafuta riziki na sio machawa kama tunavowaita!

Ni kweli ajira ni tatizo ndio maana hata lisu ni msomi ila aliamua kujiajiri kwenye siasa na imemlipa sana leo ana maisha mazuri kupitia hizi hizi siasa.
Sasa kama viongozi wa chadema waliopita wangegomea chaguzi yeye na kina msigwa,heche,sugu,mdee,mbowe na wengine walionufaika tungewajua Leo kupitia siasa?

Chadema inatakiwa kubadilika,ccm wanatumia nyenzo zote walizonazo,wanaonesha hata kidogo walichoahidi na kutimiza au kuanza,wana ahidi kikubwa,wanajichanganya na wananchi na wanapiga hadi magoti kwa wananchi inapofikia swala la kuomba kura.

Nikupe tu mfano kwenye mji niliopo,ccm iliungana na serikali bega lwa bega kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.na hakukuwa na mwanachadema hata mmoja alieyehasisha watu kujiandikisha,hata lisu hakufanya hivyo.
Je,unahisi hao watu walijiandijisha ccm watakubali kuwapoteza kirahisi?

Chadema iache siasa za matamko na mtusi,ishuke chini kwa wananchi.
Hakuna kura za huruma,kura zinatafutwa.
 
Upo sahihi mtumishi kabisa ila kwa sasa vijana ambalo ndiyo kundi kubwa limekosa mvuto kwenye upinzanni kwasababu wameona wenzao wanatekwa wanauwawa halafu mtu uliye mpigania apate ubunge au udiwani kesho yake anapata nafasi alafu anahama chama anarudi ccm. Mimi sikuzani kuwa kumbe hii ilikuwa trick kali sana yakuwavunja moyo wananchi.
 

..una hoja nzuri maridadi kwelikweli, isipokuwa katika maeneo machache.

..lakini nakuomba udadisi ni kitu gani kimepelekea Lissu na wenzake waone ni bora kususia uchaguzi.

..pia nakuomba utafakari kwanini Tume za Jaji Nyalali, Jaji Kisanga, Jaji Bomani, Jaji Warioba, na Prof.Mukandala, zote ripoti zake zimeshauri tubadilishe mifumo yetu ya uchaguzi na tuunde Tume Huru.

..mwisho, nakuomba ushauri hatua gani zichukuliwe ili uchaguzi wetu uwe wa HAKI zaidi, na usilalamikiwe na wagombea wa vyama vya upinzani.
 
Hao vijana unaosema wako CCM ndio wale waliojipaka matope na kupita mbele ya raisi, au unazungumzia akina mwakani wanagalagala kwenye vumbi? hao vijana ni kama akina Lucas Mwashambwa ? Huko CCM Kuna vijana gani wenye kujenga hoja wakaeleweka labda
 

..Nawaamini vijana wa Tanzania.

..muda si mrefu wataelewa kwamba chanzo cha matatizo yao ni CCM.

.
 
Ndo akili zenu zilipoishia huko CCM.

Eti CCM kuna fursa za vijana! Fursa gani?

Au unanadhani hatuoni hao vijana wanaorubiniwa huko wanavyopigika mitaani kwa kukosa ajira? Mnavyowatumia kama toilet paper kuwajaza kwenye mikutano kwa posho mnazoiba kwenye hamlashauri ndo fursa?

Kama huko Ccm kungekuwa na fursa vijana wangelia kukosa ajira?

Eti Chama chake kina watu wengi hamkubali? Wapi kwenye chaguzi huru na haki mtu anakubaliwa kwa asilimia 100%?

Kama hawamkubali kwenye chama chake wekeni hiyo Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya tuone kwa jinsi gani watanzania hawamkubali.
 
Hongera sana mkuu. Umejitahidi sana kumjibu asiye na uelewa wa mambo kwa busara.
 
Unajua kwanini hizo tume zote hazijafanikiwa kufanikisha kuipata tume huru?
Ni kwa sababu Nguvu ya mamba ni maji,wao wanapiga mbizi nchi kavu.

90% ya mabadiliko ya kisheria na katiba yanafanywa na wabunge ndani ya bunge.

Walio wengi bungeni na wenye nguvu ndio wenye maamuzi.

Kwahiyo njia ya kupata yote hayo ni kuwa wengi bungeni.njia ya kuwa wengi bungeni ni kuungana(imesha-prove) na lisu ashatangaza hadharani kuikataa ndio maana nasema ameipa ushindi ccm!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…