Pre GE2025 Lissu anaipa ushindi CCM mapema sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Umesema vizuri sana kiongozi.
lisu amerejea yale yale,kwa hiyo na matokeo yake kwa asimia kubwa yatakuwa yale yale au mabaya zaidi ya yale Kwa sababu nguvu yao na ushawishi kiuhalisia imepungua kuliko wakati ule!

Haki itendeke ndio,lakini katika maisha haki haipatikani kilelemama.ndio maana hata lisu na wenzie kina sugu,lema,mbowe,mdee,msigwa na wengine waliposhinda ubunge aliipata haki yao lakini si kilelemama.alipambana(walipambana haswa!
Na huo ndio uhalisia katika maisha kwa ujumla sio katika siasa tu,haki inapambaniwa! Ukiwa mzubavu hupati kitu! Na huu ndio ukweli!
 
Hao vijana unaosema wako CCM ndio wale waliojipaka matope na kupita mbele ya raisi, au unazungumzia akina mwakani wanagalagala kwenye vumbi? hao vijana ni kama akina Lucas Mwashambwa ? Huko CCM Kuna vijana gani wenye kujenga hoja wakaeleweka labda
Kwa akili hizi ccm itatawala hata miaka 2000 ijayo. Kama ndo inadhani ipo hivyo basi pole sana nyumbu wewe.
 
Uhuru wa tume umeupima kwa vigezo gani, kutangazwa Lisu mshindi haiwezi kuhalalisha uhuru wa tume, inaweza ikawa hisani tu ili kuwafumba macho wananzengo.Haki ya kweli ya kiuchaguzi itapatikana kwa uwepo wa tume iliyo huru.
 
Ndio ccm kuna fursa kuanzia juu mpaka chini!
Fursa ambazo Dr.slaa aliziona akazifuata,sasa sijui utaniambia wewe umewahi kuwa mpinzani kuliko slaa?


Fursa ambazo msingwa ameziona kazifuata,sijui unataka kutuambia wewe umewahi kuwa mpinzani kuliko msigwa?

Fursa ambazo wasanii wanaziona wanazifuata,

Yaani ukiondoa hisia ukafungua macho kuuona uhalisia,utaona vijana wa chadema wanavotia huruma kimaisha na kuishia kuwatukana na kuwakashifu tu wanaonufaika na fedha za ccm.
Japo hawawezi kunufaika wote ila wengi.na hawanufaiki hivi hivi tu wanapewa kask(washawishi watu),maana mtaji wa kwanza wa ccm ni watu na watu inao ina wapata wapya kila siku!

Fedha ipo,haiwezi kuwa sawa na ya wale lakini ipo,Chadema nayo itoe fursa kwa vijana,hela za wafadhili na ruzuku wasile viongozi wa chama tu peke yao,mkate wa chama uliwe na wengi kama sio wote kila mmoja kwa hadhi, nafasi na kazi yake.
 
Uhuru wa tume umeupima kwa vigezo gani, kutangazwa Lisu mshindi haiwezi kuhalalisha uhuru wa tume, inaweza ikawa hisani tu ili kuwafumba macho wananzengo.Haki ya kweli ya kiuchaguzi itapatikana kwa uwepo wa tume iliyo huru.
Yaani chama fulani kimpe ushindi mshindwa wa chama kingine kwa hisani!
basi sawa,tuendelee hivi hivi!
 
..una hoja gani kuhusu Tume Huru ya uchaguzi?

..kwanini CCM haitaki kuunda Tume Huru ili uchaguzi uwe wa haki?
Hakuna tume huru duniani inayoweza kutenda haki,tume bora lazima iwe haiko huru.LAZIMA IDHITIWE TENA IDHITIWE HASWA NA SHERIA,ili isiwe huru kufanya lolote lililo kinyume na haki,maana ikiwa huru itakuwa imepewa haki ya kufanya vyovyote na isifanywe lolote maana iko huru kisheria!
Iabda hoja kwa mtazamo wangu iwe namna iyo tume inavopatikana!
 
mbona ccm 90% hawamkubali saa100 ni kumi tu nabado amekaza
 
naona ID za kimkakati tu huku unajitekenya alafu unacheka.
 
 

Attachments

  • 1edaac7a3e34dc7dbc36bb899a6e6430_1738702701936.mp4
    5.4 MB
Kwa akili hizi ccm itatawala hata miaka 2000 ijayo. Kama ndo inadhani ipo hivyo basi pole sana nyumbu wewe.
ndio inavyojionyesha kwani wewe huoni? kila mtu mama mama, sio mtu mzima, au vijana wote mnaimba chorus moja, wale waliojipaka matope si ni vijana wa CCM
 
Subira the princess Jipe muda uone kama huta muona ndugai akimpigia kampeni samia, ccm inapofikia wakati wa maslahi ya chama na kukilinda chama wako makini kuliko vyama vyote nchini,hawana uadui wa kudumu,na huo ndio ukamavu wa kisiasa,jipe muda utamuoana ndugai!
 
Ukimsikiliza Lisu ukiwa tungi nini? Kifupi masisiemu mmechangsnyikiwa na mtachsngsnyikiwa kweli kweli huyu TAL anajua kusimamia anachokiamini mambo hayatakua mepesi mjiandae kisaikolojia pia
 
Team Lisu walitukana sana, ndio maana huoni watu wakishtuka na hicho chama tena, walimuona kila mtu mjinga, isipokuwa wao.
Ngoja tuone.
 
Shida ndani ya CCM huanzia kwenye kura za maoni. Watu hukatika matabaka tabaka
 
Mama je wote Wana CCM wanamkubali?
 
Ukimsikiliza Lisu ukiwa tungi nini? Kifupi masisiemu mmechangsnyikiwa na mtachsngsnyikiwa kweli kweli huyu TAL anajua kusimamia anachokiamini mambo hayatakua mepesi mjiandae kisaikolojia pia
Moja ya shida ya wengi chadema ni hii,wanaamini kila anayeenda tofauti na mawazo yao au ya mwenyekiti wao ni ccm,wanakua hasira,matusi,kashfa na kuamini wanaweza hata kama wao ni wachache.
wakati ccm wanapambana kuwashawishi wanachama wapya hata wa chadema wawaunge mmkono,chadema wao wanapambana kuwatweza wanachama wa ccm badala ya kuwashawishi wajiunge nao!
Kisaikolojia iko hivi,mfano hapa jukwaani mtu anapomshambulia na kumkashifu Mwashambwa,anamfanya azidi kukipenda kile chama kinachompa heshima.wakati ungeweza kumuelimisha na kumshawisha akuelewe na akuunge mkono,maana kura yake hata kama ni moja ina thamani kubwa atakako ipeleka!

maana kazi ya kwanza ya ccm hata kabla ya yote kuelekea uchaguzi huwa NI KUTAFUTA KURA NYINGI ZA HALALI KWA NJIA YOYOTE.na kwa sehemu kubwa huwa wanazipata kwa hivyo hivo vitenge na kofia mnazozibeza.
Ila sisi twendelee hivi hivi..
 
Sikupoteza muda kusoma makala yote!
Lakini kwa kifupi hizo ulizoandika ni hoja dhaifu!
Achilia mbali hakuna utafiti uliofanya kuthibitisha kuwa vijana wengi ni CCM kwamba wanapata cho chote! Kipi wanachopata bila kuwa machawa kwanza?
Nadhani CCM ndiyo bado wanaishi wakati uliopita! Wanaamini kama wanavyovuruga uchaguzi miaka yote ili kuingia madarakani wataendelea hivyo hivyo!
Kwa nini mnavuruga uchaguzi ili muingie madarakani ni kwa sababu mnajua na ndivyo ilivyo CCM hakiaminiki kwa wapiga kura.
Nimalizie hapo kwa kukumbusha harakati za kuving'oa vyama vilivyokaa madarakani muda mrefu kwa hasara ya wananchi,ni Kuunganisha nguvu za wananchi.
 
Hata mama hatumpendi sisi sisiemu ila nani atamfunga paka kengere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…