Pre GE2025 Lissu anaipa ushindi CCM mapema sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tume huru tunayo au unazungumzia ipi mkuu?
Kwa hiyo Tume hii inayoshuhudi uenguaji na mauaji ya Wagombea wa Upinzani kila mara kwako ni sawa?? Sasa Mh Lissu alichosema hawako na hawatakuwa tayari kuwapeleka Vijana au Watoto wa Kitanzania kwenye uchaguzi utakaosimamiwa na tume zile zile wakauawe. Mauaji ya kila mara wakati wa uchaguzi sasa basi.
 
Shida ya Africa sio tume huru wala chaguzi huru bali kupata mifumo itakayo badili akili za waafrika waweze kuona fursa tele zinazowazunguka ili watatue shida zao.
Mambo ya uchaguzi ni matumizi mabaya tu ya fedha zetu
Wewe ni katika wachache wenye akili. Uongozi unapimwa hata kwako wewe binafsi. Uwezo wako, fikra yako, socialization, Lakini hata humu kwenye group unakuta mtu ni mbaguzi Lupita kiasi, matusi kupita kiasi, unaweza ukajifunza kuwa tuna watu wa namna gani ktk nchi. Watu hawa ndio tunategemea wounded dola, wakawe watumishi ktk ngazi tofauti, tutegemee Mimi kama sio umasikini. Wizi kwa Watanzania imekuwa ni biological trait. Mtu anajiibia hata yeye m wenyewe.
Uwongo ndio fashion, unadanganya mpaka mkeo, pesa umehonga ukiulizawa Majibu yake ni wewe jua imeisha tu, ukivyokula vilitokana na nini. Duu ni shida
Ila Sisi tuna utamaduni tofauti Lisu ajue, hatuwezi kuwa kama Kenya au Congo Lisu anakolinganisha. Afanye siasa kwa kuangalia utamaduni wa mtanzania. Akifanya siasa kama Kenya au Congo lazima afeli, Sisi ni watu wa Amani, ukitaja taja tu Congo au Kenya au Somalia inatosha Watanzania kukutosa hata kama ni masikini, Sisi kwetu cha muhimu ni Amani.
 
Mama je wote Wana CCM wanamkubali?
Hawezi kupendwa na wote lakini anaonesha kuwahitaji wote,anajipambanua kwa wote,wanadini,wanasiasa wenzie,wanamichezo,wasanii,mitaani mabonanza,mpaka chini ubalozini na hivyo vyote hakuna kiongozi wa upinzani aliyezuiliwa kuvifanya,viwe na umuhimu visiwe na umuhimu ila vinavuta watu upande wake! Na siasa kabla ya uchaguzi ni watu,mengine ni baada ya uchaguzi.

I'm signing out!
 

..uko upande mzuri kwasababu unazungumzia HAKI.

..pia umeweka msisitizo kuhusu namna Tume Huru inavyopatikana.
 
CCM wanachofanya kuhamasisha umma kushiriki katika michakato ya chaguzi si kwa ajili ya kupenda sana watu washiriki, bali ni katika kuhalalisha wizi wa kura wanaoufanya.

Kuna kituo mwaka 2020, kura za urais zilizidi mara mbili zaidi ya idadi ya wakazi wote wa huo mtaa.
Wapigakura halali kwenye daftari ni 130, lakini idadi ya kura za mgombea wa CCM ni 322.
 
Ukiwa "kigogo" ndani ya CCM halafu ukaenda kinyume nao, basi yatakukuta kama yaliyowahi kuwakuta wakina Kolimba, Abdu Jumbe, Mangula.
Unaweza kuKolimbwa.
Unaweza kubambikiwa kodi ya mabilioni kwenye biashara zako.
Unaweza kusingiziwa mambo mengi sana.
Tumeyaona.

CCM inapokuja kwenye swala la kulinda maslahi yao, wapo tayari kuwa zaidi ya shetani, na hilo ndilo linalowaogopesha watu wenye hoja za msingi huko CCM.
 
Bila mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi Tume ya uchaguzi imeshaipa CCM ushindi hata kabla kupigwa kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…