chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Lissu ni mwanasiasa anaye shine/anayeng'aa pale panapokuwa na Siasa za mapambano, Siasa hizo zilikuwepo enzi ya jiwe, yule Mzee wa Chato.
Kwa Sasa ni SSH, hana Siasa hizo za piga nikupige. Ndio maana baada ya ujio wa Lissu, ndani ya muda mfupi "amechuja" na umaarufu wake umechuja kwa asilimia 80.
Aina hii ya Siasa aliwahi kuijadili Mbowe akiwa nje ya nchi, Mbowe alisema anawafahamu watanzania kwa muda mrefu, kwamba Siasa zao ni tofauti na Siasa za Kenya, Kenya Wana Siasa za mapambano, kuandamana, mikutano, hawaogopi. Nadhani Lissu anahitaji kuisoma upya jamii ya watanzania na kucheza ndani ya engo ya saikolojia ya watanzania.
Mbowe alikamatwa ndani ya vuguvugu la katiba mpya, hakuna Cha Mnyika, Heche, Wala nani aliyeandamana. Watu wako bize na mambo yao.
Mbowe alikuwa sahihi alipofanya mabadiliko ya mbinu kwa kuingia katika mjadala na Serikali.
Na ndio watanzania tulivyo, tangu ukoloni, Nyerere alitusoma akajua hawa ni watu wa kwenda nao taratibu, na ni wazi aliona hakuna wa kuandamana Wala kuingia katika vita kupigania Uhuru, kama ilivyokuwa kwa MAU MAU Kenya, Nyerere Kaa mezani, Uhuru ukaja.
Pia Lissu kama kiongozi awe anaangalia muda gani anaongea angalau watu wammisi, watu wamemsikiliza Twitter mpaka wakachoka, kiongozi angalia timing ya kuongea, kaa kimya, ulisema unaongea watu wanashtuka, au kuwa na hamu. Sasa akina maria sarungi wakishavuta Hela za mabeberu, kujustify retirement, wanakimbia kwa Lissu, Lissu anaongea masaa kadhaa, anachuja.
Nadhani Kila nchi Ina set up ya kisaikolojia ambayo wanasiasa wanatakiwa kuisoma na kuifanyia uchambuzi, na pengine hata Kila Jimbo, Tarime na Mkunazini Zanzibar haziwezi kuwa sawa.
Wasalaam.