Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Huenda upo usahihi.

Ila utakuwa usahihi zaidi ukitoa ushahidi wa wewe kuwahi kuelezwa na huyo mwingine au mamlaka yake yoyote nyingine maswala haya:
-Mandege yalinunuliwa kwa Mchakato gani na nani alipewa kiasi gani hadi yamefika hapa?
-Ma-stieglers,SGR na Kipanda juu cha UBUNGO (Sio Fly Over)
Kama ni Fedha za ndani zinajenga,
Deni la Nje limeongezekaje?

Zimekwenda wapi hizo Pesa?

-Mapato ya Tanzanite yalikuwa yakikaguliwa awali,
Kabla huyu Mtu wako hakuwa Dereva,
Sasahivi Mkaguzi Mkuu hatii Pua huko,
Umejiuliza kwa nini?

Au Kunya anye Kuku?
Bata🤔

Tuanzie hapo Kama huwa Akili yako inaweza kuchakata Hoja kwa Hoja.
 

Mtu wa hovyo kweli kweli wewe. Kama mataifa hayo ukiyoyataja yana mfumo tofauti katika majimbo yao, kwani ni lazima tufanye kama wao??

Kuna kitu kimoja hujui - kuwa viwango katika kila jambo. Unaweza kupima ubaya na uzuri. Tujaribu mfumo wetu pekee (kama ulivo muungano) na tujaribu hilo - mfumo wa sasa umeshindwa kuendeleza maeneo kadhaa ya nchi!!
 
Majimbo madhara yake ni makubwa na ya muda mrefu.

Kodi anayolipa mtu wa Mtwara ndivyo inayojenga meli ziwa Victoria.

Kodi anayolipa mkulima wa Kahama Kagera ndio inapanua bandari ya Tanga.

Kodi anayolipa mkulima wa mahindi Ruvuma ndio imejenga kilio kikubwa cha mabasi Dodoma.

Hiyo ndio maana ya umoja wa nchi na ndio kusudio la waasisi wa taifa.

Tukipata tunatumia kwa faida ya wote na tukikosa tunalala njaa wote.

Kauli ya rais lengo lake ni kuwafanya wanasiasa wakukumbuka jukumu lao la msingi kwamba ni kushughulika na shida za watu kuliko kuzama kwenye siasa za kususa na kutoka nje ya jengo la bunge.
 

Sera ya majimbo msingi wake ni fikra za uchoyo na ubinafsi.

Kidole kimoja hajivunji chawa, kuamini kwamba jimbo moja moja linaweza kutimiza mikakati mikubwa ya kimaendeleo ni sawa na kukiamini kidole kimoja.
 

..serikali za majimbo zitasaidia kutatua shida wa wananchi kwa wakati, bila kuchelewa.

..pia zitaongeza uwajibikaji wa viongozi kwani watakuwa wamepatikana kutokana na wananchi.

..kuhusu masuala ya kodi, kodi za serikali kuu, na kutakuwa na kodi za mamlaka za majimbo.

..kodi za serikali kuu zitatekeleza miradi ya maendeleo ya serikali kuu maeneo mbalimbali ya nchi.

..Kwa mfano, sgr ni mradi wa serikali kuu hivyo utagharimiwa kwa fedha zitakazotokana na kodi za serikali kuu.

..kodi za mamlaka za majimbo zitagharamia miradi ya maendeleo na huduma za kijamii ktk jimbo husika.

..Kwa mfano, miradi ya masoko ya kisasa, ujenzi wa madarasa, ujenzi wa majosho, etc inaweza kuwa chini ya serikali za majimbo.

..maeneo ambayo yatakuwa yamepungukiwa yatachangiwa na serikali kuu kama ambavyo inafanyika sasa hivi.

..Serikali za majimbo zitaondoa mlundikano wa madaraka na majukumu ktk ngazi ya serikali kuu na kuyashusha madaraka chini kwa wananchi.

NB:

..Kauli ya Raisi ni ya KIBAGUZI na inapaswa kukemewa na kila anayependa umoja wa nchi yetu.
 
Kila Jimbo linajitegemea ndio maana Kuna majimbo Marekani yenye umaskini wa kufa mtu na yako mengine matajiri kupita maelezo
Tanzania hakuna majimbo lakini maisha ya kongwa , bahi, geita na kawe au kinondoni yanadanana? Mbona wengine hata maji ya Bomba hawajawahi huyaona tangu dunia kuomba?ni sababu ya majimbo au sera mbovu za Ccm?
 

Wewe kila siku huwa unaongea ujinga tu sijui unatatizo gani Kwani garama za kuendeshea hiyo mikoa zinatoka wapi mbona unataka kuwaambukiza wengine ujinga wako.

Kwahiyo kuna jimbo la singida ulilisikia lini hilo jimbo au jimbo la kati ni singida peke yake, na mikoa mingine hiyo huioni kama Dodoma. Acha kupotosha watu wamechoka na huu umasikini unachangiwa na viongozi kuwa na immune na kufanya ufisadi kwa sababu pesa zote zinakuwa chini ya mtu mmoja kila siku nitawajengea atajenga yeye Kwani pesa si za wananchi. Acha kila jimbo litumie rasilimali zake kuna ubaya gani sioni jimbo lisilo na rasilimali.
 

Hivi huo ubinafsi ukabila na roho mbaya aliyonayo jiwe ni kwasababu ya serikali ya majimbo yapi. Ameikuta nchi inatawaliwa vizuri tu ameleta ukabila wa kupindukia ubinafsi hadi kiwanja cha Ndege cha kimataifa kijijini kwake, roho mbaya ya kuuwa watu na kuteka watu na kupoteza watu. Hakuna mtu ana roho mbaya kama jiwe tangu nizalowe sijawahi kuona mtu mbinafsi kama jiwe, aomdoke tu kwakweli aking’ang’ania ataingiza nchi kwenye machafuko
 
Kwenye hili la majimbo wale wavivu wa kufanya kazi,wale waliozoea kuishi kwa kutegemea jasho la wengine lazima mpige kelele sana
 
Wote mnaopinga hii hoja hakuna hata mmoja anayetoa sababu zenye mashiko. Msingi wenu mkubwa wa kupinga ni kwa kuwa tuu Lissu katamka full stop. Ingekuwa jambo hili liko kwenye sera ya ccm wote mngekaa kimya kwa sababu kwenye hoja nyingi ninyi lumumba huwa mnaenda na movement ya upepo. Wengi wanadhani sera ya majimbo kaleta Lissu lakini msichojua ni kwamba ipo tokea Slaa akiwa katibu mkuu, ni sera ya zamani tuu.
 
Kitu wanachokiogopa kuliko vyote, na ambacho Lissu kakusema sana ni viongozi wa majimbo (wakuu wa majimbo, wakuu wa wilaya na Ma DED) watachaguliwa na wananchi kwenye majimbo yao na pale watakapoboronga watawajibushwa huko huko. Sasa wanaogopa kwamba kutakuwa hakuna mgao wa vyeo vya bure vya ki siasa.
 
Acha ulofa na uwongo wako, kabla ya uhuru Tanganyika ilikuwa na majimbo 8... Jimbo la Kaskazini (mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga), jimbo la ziwa (Mwanza, Kagera, Mara na Shinyanga), jimbo la Pwani (dsm, Pwani, Morogoro) etc...viongozi wa majimbo na wilaya zake walikuwa wanateuliwa na gavana. Baada ya uhuru wakaondoa majimbo na kuleta mikoa, wilaya zikabaki vilevile. Sasa anayeteuwa wakuu wa mikoa na wilaya ni rais, kama alivyokuwa anafanya gavana wa kikoloni.
 
Kwa mabeberu 🤣😳🤣😳
 
Sahihi kabisa. Pia serikali kuu itakuwa na uwezo wa kuchukua mikopo mikubwa ili kufanikisha miradi mikubwa kwenye majimbo mfano ujenzi wa mabwawa ya umeme, kuvuta maji ziwa Victoria kuleta Tabora au Singida, ujenzi wa Railway za kisasa etc. So majimbo Kuna asilimia ya mapato yake yataenda serikali kuu ili ku services hiyo mikopo lakini pia kuongezea kwenye bajeti za majimbo mengine.
 
Kwa taarifa yako jimbo la Bwege (Kilwa) ndipo inapotokea gesi asilia ya Songo songo, wana misitu mingi sana, wana bahari yenye uvuvi mwingi sana, kuna mbuga kubwa ya Selous. Kwa ufupi ni kwamba lina utajiri mwingi sana, lakini tatizo ni mgawanyo. Mfano gesi ya songo songo limejengwa bomba inaenda Dar yote. Mapato ya mbuga ya Selous wanapata kiduuchuu, vilevile kwenye misitu ni the same. Meli kubwa za uvuvi zinakatia leseni huko Dar wizarani wakija kuvua Kilwa hawaguswi....
 
Hiki ndicho kitu kinachowatatiza, wrong concept....jimbo moja mfano jimbo la magharibi linaweza kuundwa na mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa. Sasa all resources kwenye hii mikoa 3 zinakwenda kwenye kapu la jimbo (pia kuna asilimia itaenda serikali kuu). Sasa kila jimbo litakuwa na bunge lake ambalo wabunge kutoka hiyo mikoa 3 watakuwa wanakutana na kujadili wamekusanya how much na wanapanga kufanya miradi gani ndani ya mikoa hiyo 3 na bajeti yake. Kumbuka kwamba kwenye bajeti yao pia watatarajia kupata pesa from serikali kuu plus grants au mikopo ambayo imedhaminiwa na serikali kuu. Kwa hiyo katika hiyo mikoa 3 kila mkoa utakuwa na mchango wake, mfano Kigoma wana ziwa Tanganyika, wana hifadhi ya Mahale, bandari na reli vitaimarishwa, ukienda Katavi wana misitu mingi sana, hifadhi ya Katavi, ardhi nzuri ya kilimo cha mahindi, mpunga, pamba etc, ukienda Rukwa pia wana resources zao, tena nyingi tuu. Haya jimbo lingine laweza kuwa jimbo la Kaskazini (mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga) hapa kila mkoa una rasilimali zake... Ukienda jimbo la nyanda za juu (Iringa, Mbeya, Njombe etc)...
 
Suluhisho la hasira zako haliwezi kuwa sera ya majimbo ya kukopi na kupesti kutoka nchi nyingine.

Nchi huwa haifanyiwi majaribio kwa sera zisizokuwa na msingi wa asili, watu wataumia.
Ni upuuzi kulazimisha mfumo wa mikoa na wilaya zooteee kushikiliwa Dar au Dodoma for about 60 years huku unachechemea na kila mwaka huna hata uwezo wa kuwa na pesa yako 100 %kuendesha nchi...
 
Mbona unafoka sana?
Kumbuka kuwa magavana wa majimbo ni viongozi wa kuchaguliwa na wananchi wa eneo husika.Are we togather?
Hawataki hilo maana watashindwa kuhongana u DC, DAS etc
 
Ukishakuwa na majimbo ndio utaufahamu uwezo halisi wa hayo majimbo katika kuweza kujitegemea.

Hivi sasa wakati tunao mfumo wa ushirikiano huwezi ukaiona tofauti kati ya kanda za nchi hii.

Ukiwa na majimbo ndio itaiona tofauti ya jimbo la pwani lenye bandari kubwa na jimbo la kati kina Singida na Dodoma wenye ukame mwaka mzima.

Majimbo ni mtego mbaya sana kwa utaifa wa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…