Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Pole sana mkuu Huyu ni mpaka 2025 tukipewa uhai.Hivi huo ubinafsi ukabila na roho mbaya aliyonayo jiwe ni kwasababu ya serikali ya majimbo yapi. Ameikuta nchi inatawaliwa vizuri tu ameleta ukabila wa kupindukia ubinafsi hadi kiwanja cha Ndege cha kimataifa kijijini kwake, roho mbaya ya kuuwa watu na kuteka watu na kupoteza watu. Hakuna mtu ana roho mbaya kama jiwe tangu nizalowe sijawahi kuona mtu mbinafsi kama jiwe, aomdoke tu kwakweli aking’ang’ania ataingiza nchi kwenye machafuko
Ni zaidi ya uvivu kuna suala zima la utaifa mkuu Sijijui.Kwenye hili la majimbo wale wavivu wa kufanya kazi,wale waliozoea kuishi kwa kutegemea jasho la wengine lazima mpige kelele sana
Mkuu unataka Tanzania ya 2020 irudi kufanana na ile ya 1955!!.Acha ulofa na uwongo wako, kabla ya uhuru Tanganyika ilikuwa na majimbo 8... Jimbo la Kaskazini (mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga), jimbo la ziwa (Mwanza, Kagera, Mara na Shinyanga), jimbo la Pwani (dsm, Pwani, Morogoro) etc...viongozi wa majimbo na wilaya zake walikuwa wanateuliwa na gavana. Baada ya uhuru wakaondoa majimbo na kuleta mikoa, wilaya zikabaki vilevile. Sasa anayeteuwa wakuu wa mikoa na wilaya ni rais, kama alivyokuwa anafanya gavana wa kikoloni.
Majimbo yanaondoa dhana ya umoja na ukishapoteza umoja maana yake huna taifa.Kwa taarifa yako jimbo la Bwege (Kilwa) ndipo inapotokea gesi asilia ya Songo songo, wana misitu mingi sana, wana bahari yenye uvuvi mwingi sana, kuna mbuga kubwa ya Selous. Kwa ufupi ni kwamba lina utajiri mwingi sana, lakini tatizo ni mgawanyo. Mfano gesi ya songo songo limejengwa bomba inaenda Dar yote. Mapato ya mbuga ya Selous wanapata kiduuchuu, vilevile kwenye misitu ni the same. Meli kubwa za uvuvi zinakatia leseni huko Dar wizarani wakija kuvua Kilwa hawaguswi....
Vipi kuhusu balance of trade kati ya jimbo moja na jingine!?Hiki ndicho kitu kinachowatatiza, wrong concept....jimbo moja mfano jimbo la magharibi linaweza kuundwa na mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa. Sasa all resources kwenye hii mikoa 3 zinakwenda kwenye kapu la jimbo (pia kuna asilimia itaenda serikali kuu). Sasa kila jimbo litakuwa na bunge lake ambalo wabunge kutoka hiyo mikoa 3 watakuwa wanakutana na kujadili wamekusanya how much na wanapanga kufanya miradi gani ndani ya mikoa hiyo 3 na bajeti yake. Kumbuka kwamba kwenye bajeti yao pia watatarajia kupata pesa from serikali kuu plus grants au mikopo ambayo imedhaminiwa na serikali kuu. Kwa hiyo katika hiyo mikoa 3 kila mkoa utakuwa na mchango wake, mfano Kigoma wana ziwa Tanganyika, wana hifadhi ya Mahale, bandari na reli vitaimarishwa, ukienda Katavi wana misitu mingi sana, hifadhi ya Katavi, ardhi nzuri ya kilimo cha mahindi, mpunga, pamba etc, ukienda Rukwa pia wana resources zao, tena nyingi tuu. Haya jimbo lingine laweza kuwa jimbo la Kaskazini (mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga) hapa kila mkoa una rasilimali zake... Ukienda jimbo la nyanda za juu (Iringa, Mbeya, Njombe etc)...
Ni upuuzi mkubwa kuivunja nchi kwa kuigawa kimajimbo.Ni upuuzi kulazimisha mfumo wa mikoa na wilaya zooteee kushikiliwa Dar au Dodoma for about 60 years huku unachechemea na kila mwaka huna hata uwezo wa kuwa na pesa yako 100 %kuendesha nchi...
Asante sana kwa ufafanuzi kaka, wangejiuliza kwa sasa hiyo mikoa inajiendeshaje ikiwa mapato yote yanapelekwa serikali kuu ndipo wanaanza kuomba na kubembeleza kwa boss wao na mpka apende kuwapa. Serikali ya majimbo itawasaidia wananchi kumiliki mapato yao ambayo yatajenga majimbo yao pia kuunda serikali inayoongoza kwa weledi.Usilazimishe Kutokuelewa Kwa Maksudi, unazidi kuudhihirisha ujuha wako.
Je, unayajua Majimbo yatakavyokua na mikoa itakayoyaunda hayo majimbo?
Hiyo singida uisemayo itakua katika jimbo la kati litakalojumuisha mikoa ya MOROGORO, DODOMA SINGIDA NA TABORA. haya hapo umasikini unatokea wapi ikiwa kuna vyanzo vingi vya mapato katk mikoa hiyo.
Mnakera hata kama mnalipwa, wengi ni mambumbumbu. Yaani weupe vichwani.
Tuambie issue ya utaifa ipoje kwasasa,issue ya utaifa ipoje kenya,issue ya utaifa ipoje US?Ni zaidi ya uvivu kuna suala zima la utaifa mkuu Sijijui.
Majimbo pia yanatokana na fikra za kichoyo na kibinafsi.
US, Kenya huwezi kufananisha na TZ.Tuambie issue ya utaifa ipoje kwasasa,issue ya utaifa ipoje kenya,issue ya utaifa ipoje US?
Small mind, mfumo tuliyonayo wa Unitary System of Government kwa akili zako unafikiri Tanzania ndiyo iliuanzisha si na wenyewe tuliukopi tu kwa wengine.Suluhisho la hasira zako haliwezi kuwa sera ya majimbo ya kukopi na kupesti kutoka nchi nyingine.
Nchi huwa haifanyiwi majaribio kwa sera zisizokuwa na msingi wa asili, watu wataumia.
Nyerere akawa mjanja akahakikisha baada ya kuuwa uchifu anawapa vyeo serikalini kama kuwapooza wasijione wameshushwa thamani.Kama Taifa tusingeabolish Uchifu leo tungekuwa na vijiserikali vingiii ambavyo vingekuwa na maoni tofauti tofauti na huenda hili la majimbo lingewezekana... Maana haya huja ku hamornize co-existance kunapokuwa na more than one group of unified interest. Haina tofauti na kuwa na serikali ya mseto.
Majimbo kwa sasa sioni mantiki yake. Hakuna mpasuko wa kitaifa, wachanga wamewekeza kwa wagogo na Wahehe wanafanya kazi na wasukuma wajita wako na wabondei. Kwa namna fulani kwa sasa watanzania ni wamoja.
Kwa rasilimali chache zilizopo zikielekezwa Mbeya wapo wasukuma wanaonufaika zikielekezwa mwanza wapo wagogo na wazaramo wanaonufaika zikiwekwa DSM wako wachaga na wabena wananufaika.
Kuondoa chuki, tamaa, sioni kwann watu watake rasilimali zao pekee ziwanufaishe wao pekee ikiwa tumeamua kuwa wamoja!?! Kuna dhana ya majimbo tajiri kuyasaidia masikini ..hili haliwezekani.. pesa haijawahi kujaa hata siku moja na matatizo hayakomi... Ingekuwa ni rahisi kusingekuwa na majimbo masikini USA.
Mie nadhani haya ni mawazo ya kuweka mbali kabisa kwa mustakabali wa Taifa. Kama haridhiki na muundo wa jamhuri yetu, tuangazie hapo na tulete mapendekezo ya maboresho. Sio turudi tena kuanza kujigawa .. Maumivu ya kichwa huanza taratibu hiki tunachokililia kitatuchoma tutashangaa.
Kuna watu wanaizungumzia Kenya Kenya zilikuwemo serikali za kikabila.. na zinalinda interest za kikabila. Ziliachwa na zikakua sasa hapo hawana namna zaidi ya kuzitambua kwao serikali ya kijimbo ni solutions maana nchi msingi wake ni Umimi. Mkikuyu hataki kutawaliwa na Mkisii, Mluhya hataki kuwaliwa na Mkamba. Hakuna namna zaidi ya kuwaachaa wajitawale chini ya mwamvuli mmoja wa Kenya..
Lakini hata hivyo inapokuja kuwa head of state bado unaona clashes.. kwa sababu kila moja ataka kuwa mkubwa. Hii sio approach bora kwa matarajio ya muda mrefu ya taifa imara na lenye umoja. Tusijitumbukize huko.. dhambi ya kujitenga hauishii hapo kwenye majimbo... Huko mbele watu wataulizana we ni wa ukoo gani.
Asubuhi Njema.
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Small mind, mfumo tuliyonayo wa Unitary System of Government kwa akili zako unafikiri Tanzania ndiyo iliuanzisha si na wenyewe tuliukopi tu kwa wengine.
Kuna ushahidi kwamba hakuna mfumo ambao ni 100% Foolproof, lakini mfumo wa Federation kwa nchi inayotaka ijiletee usawa na maendeleo ya haraka na kukwepa kutawaliwa kidikteta ni mfumo bora zaidi.Big mind tambua kuwa ukiuvunja huu mfumo madhara yake ni ya miaka mingi ijayo.
Umejengwa kwenye dhana ya umoja yaani usisi na sio umimi.
Federation kwa Nigeria haijawaacha salama. Huko mashariki wa-Igbo wanadai kuonewa na wa Hausa pamoja na yoruba.Kuna ushahidi kwamba hakuna mfumo ambao ni 100% Foolproof, lakini mfumo wa Federation kwa nchi inayotaka ijiletee usawa na maendeleo ya haraka na kukwepa kutawaliwa kidikteta ni mfumo bora zaidi.
Nigeria baada ya uhuru 1960 walikuwa na mfumo wa Unitary System of Government kama huu tuliyonao lakini ulisababisha ukabila hadi wakapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe na baada ya vita 1970 wakaanzisha mfumo wa Federation waliyonayo hadi leo bila shida.
Wewe ni mjinga (Ignorant) hujui kitu. Unafahamu Nigeria kabla ya kuundwa kwa Federal Government kitu gani kilitokea.Federation kwa Nigeria haijawaacha salama. Huko mashariki wa-Igbo wanadai kuonewa na wa Hausa pamoja na yoruba.
Federation ni rahisi sana kuibuka makundi ya wasomi watakaocheza na sentiments za majimbo yao na kuanzisha akili za kujitenga kwa maana ya kujimega kwa nia ya kujitegemea.
Unaweza ukatatua tatizo la ukiritimba wa serikali ukaanzisha tatizo la watu kukuza asili zao na kujiona ni bora kuliko wengine.
Tumia lugha za kistaarabu punguza jazba. Federation kwa nchi ya Nyerere haiwezi kufanikiwa, msingi wetu wa taifa ni umoja.Wewe ni mjinga (Ignorant) hujui kitu. Unafahamu Nigeria kabla ya kuundwa kwa Federal Government kitu gani kilitokea.
Nenda usome ukishaelewa ndio urudi tena hapa kwa sababu inaonekana hujui ni kwa nini Nigeria waliamua kuachana na Unitary System of Government na ku-adopt Federal System of Government.
Nyie mnabisha nini wakati hapa Tanzania tu sasa hivi kuna manung'uniko mengi kuwa Magufuli anapendelea sana eneo anakotoka, wateule wake wengi wa kwenye maeneo nyeti lazima watoke huko.
Miradi mingi pia anajaribu kupeleka kwao na wengine wakibomolewa nyumba zao huko anawakingia kifua wasibomolewe haya yote yanafanyika wakati sio utawala wa majimbo.
Ukishakuwa na majimbo ndio utaufahamu uwezo halisi wa hayo majimbo katika kuweza kujitegemea.
Hivi sasa wakati tunao mfumo wa ushirikiano huwezi ukaiona tofauti kati ya kanda za nchi hii.
Ukiwa na majimbo ndio itaiona tofauti ya jimbo la pwani lenye bandari kubwa na jimbo la kati kina Singida na Dodoma wenye ukame mwaka mzima.
Majimbo ni mtego mbaya sana kwa utaifa wa Tanzania.