Hivi mnadhani kwa kuwa chama tawala nyie mna hatimiliki ya akili za Watanzania? Kwamba sisi hatuelewi tunachoambiwa kuhusu majimbo yanayosemwa na kwamba tutapelekwa tu halutakuwa na vikao vya kuamua namna gani hayo majimbo yaendeshwe? Faida mojawapo ya majimbo tumeelezwa ni kuongozwa na Magavana wa kuchaguliwa, sasa hivi Wakuu wa mikoa na wilaya hawana tofauti na viongozi wa Kikoloni (Area commissioners) waliokuwa wanqogopwa kwa kukamata wananchi na kuwaweka ndani hata kwa makosa yasiyotajwa kwenye sheria.
Mmemsilkia Magufuli mwenyewe akisema wazi hata vitambulisho vya Machinga watu hawakupaswa kulazimishwa, lakini uliza mikoani Wakuu wa Wilaya ambao ni wateule wa Rais na Makada wa CCM wamewatendea nini Wananchi?
Ni watumishi wangapi wamekamatwa kwa amri ya maDc kwa kosa la kuchelewa kikao cha mkubwa, huku sheria ikimtaka DC kukamata na kuweka ndani masaa 24 kwa makosa ya jinai na uvunjifu wa amani pekee na si makosa ya Nidhamu? Tumechoshwa na umyanyasaji wa "Wakoloni" wenu weusi.