Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Nilitaka nimwambie hivi thanks.
Huyu Yehodaya ukweli anaujua lkn alishaamua kujitoa ufahamu.

Huyu yehodaya, ni mpiga kelele kama wale wapiga makofi na kuimba taarabu. Uwezo wake ni wachini sana na hana uwezo wa kuelewa kitu chochote zaidi ya kupiga filimbi. Ni jitu jinga jinga tu wala huna haja ya kusumbuka nalo.
 
Vidumu vya alizeti vikisimamiwa vizuri vinaweza kujenga lami, hospitali, shule, vituo vya afya na visima vya maji
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo

Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchuimi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti.hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja .Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?

Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe!!!

Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama Za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio
 
Suala ni Tanzania yetu na kesho yetu itakuwa vipi tukiruhusu sera ya majimbo.

Punguza unyonge wa kiakili ridhika na cha kwako ulichopewa na Mungu.
Kwani China ikoje? Marekani ikoje???
Jibu la swali lako ni kuwa Tanzania yetu ya kesho itakuwa na maendeleo ya uhakika na wana China viongozi wanaowajibika vizuri kwa maendeleo yao ya kweli.
 
Nyuzi za huyu mwamba huwa ana andika utafikiri anaishi sayari ya Pluto huko, Yaani anaonyesha kabisa uwezo wake wa kufikiria ni mdogo kama punje ya unga wa ngano [emoji23][emoji23]
 
US, UK, German, Kenya, South Africa, Nigeria zina majimbo tunazizidi nini.
Hizo zote walipigana wao kwa wao yaani Civil war wakaona ufumbuzi ni kuazisha serikali za majimbo

Google uone .Andika mfano Germany civil war au UK Civil war au USA civil war nk kenya hapo jirani walitwagana hasa ndio wakaja na huo mfumo .Afrika ya kusini wao kwa wao walitwangana hasa wakaja na huo mfumo msumbiji pia walitwangana wenyewe kwa weyewe wakaja na huo mfumo

Chadema wana copy na ku paste bila kujua chimuko lilikuwa nini

Nchi hizo zilikuwa fored sio hiari
 
Nimekujibu kwa kukwambia kuwa upinzani umejikita kupinga kila kitu hata mambo ambayo ni progressive.

Upinzani unafanya siasa hata katika masuala yasiyohitaji siasa.

Huko kwa bwege kiusalama kuna masuala mabaya sana yalifanyika na yakataka kuivunja kabisa Tanzania, siwezi kuyaandika humu jukwaani.
Kwa iyo Kama wanapinga kila kitu ndo wasipelekewe maendeleo pamoja na kwamba na wao wanalipa kodi???

Maendeleo ni fadhila au haki ya mtu kutokana na kulipa kodi???
 
USA wamepigana civil war, na yale majimbo ni Suluhu ya vita.

Ikitokea Afrika ikawa na wazo la kuungana na kuwa ni nchi moja mimi binafsi nitakuwa wa kwanza kuunga mkono Tanzania iwe ni jimbo mojawapo.
Kwani Tanzania kina Mkwawa , Kinjekitile hawakupigana vita??
 
Kwani China ikoje? Marekani ikoje???
Jibu la swali lako ni kuwa Tanzania yetu ya kesho itakuwa na maendeleo ya uhakika na wana China viongozi wanaowajibika vizuri kwa maendeleo yao ya kweli.
China na Marekani wanayo misingi ya sera ya majimbo, hawakuamka tu na kuwa na majimbo.

Sisi Tanzania tunategemeana sana na Nyerere hakuwa mjinga kusisitizia utaifa kwanza.
 
Vidumu vya alizeti vikisimamiwa vizuri vinaweza kujenga lami, hospitali, shule, vituo vya afya na visima vya maji
😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Nimekujibu kwa kukwambia kuwa upinzani umejikita kupinga kila kitu hata mambo ambayo ni progressive.

Upinzani unafanya siasa hata katika masuala yasiyohitaji siasa.

Huko kwa bwege kiusalama kuna masuala mabaya sana yalifanyika na yakataka kuivunja kabisa Tanzania, siwezi kuyaandika humu jukwaani.
Kauli za Mh. Za hivi juzi ni za kupigwa vita sana na mtanzania yeyote mwenye akili timamu.

Hawezi sema hatapeleka maendeleo kwa watakao chagua upinzani halafu wakati huo huo anakusanya mapato /kodi kutoka kwao.

Huo ni uonevu mkubwa na ndio mwanzo wa kuligawa taifa kuliko hata hiyo sera ya majimbo ambayo inaongelewa, tuwe wakweli daima.
 
Kwa iyo Kama wanapinga kila kitu ndo wasipelekewe maendeleo pamoja na kwamba na wao wanalipa kodi???

Maendeleo ni fadhila au haki ya mtu kutokana na kulipa kodi???

Maendeleo ni haki ya kila kona ya nchi lakini siasa zikizidi hata hayo maendeleo huwa yanaonekana ni ziada.
 
China na Marekani wanayo misingi ya sera ya majimbo, hawakuamka tu na kuwa na majimbo.

Sisi Tanzania tunategemeana sana na Nyerere hakuwa mjinga kusisitizia utaifa kwanza.
Nani kakwambia sie tutatamka tu bila kuweka misingi???
Mbona huyo Nyerere pia aliandika kitabu akisema tujisahihishe??? Wewe ni nani hutaki kujisahihisha?
 
Maendeleo ni haki ya kila kona ya nchi lakini siasa zikizidi hata hayo maendeleo huwa yanaonekana ni ziada.
Nani kakwambia maendeleo ni ziada??? Wewe jamaa una elimu gani kwanza??? Maana tuanzie hapa, Naona kama Kuna kilaza aliyetukuka anayejidhalilisha tu
 
China na Marekani wanayo misingi ya sera ya majimbo, hawakuamka tu na kuwa na majimbo.

Sisi Tanzania tunategemeana sana na Nyerere hakuwa mjinga kusisitizia utaifa kwanza.
Kung'ang'ana na ujinga unao gharimu taifa eti kisa alianzialsha nyerere ni ujinga mkubwa zaid

Unatakiwa kujua enzi za nyerere hali ilikuwaje na sasa hali ikoje , mifumo ya nyerere kwa sasa haina nafasi maana ni mzigo mkubwa sana na ni ya kikolon sana
Mkoa mmoja una lundo la viongozi na wote wanatumia gharama kubwa za uendeshaji.
 
Kwani Tanzania kina Mkwawa , Kinjekitile hawakupigana vita??
Wakati wa uhuru vita zilikuwa zimeshakuwa ni historia. Nyerere alijenga nchi kwa kutumia dhana ya kuwaunganisha watu.

Akavunja kabisa uchifu kwa kuwaona machifu ukuu wa mikoa na uwaziri ili tuongee lugha ya utanzania.

Ukirudisha majimbo unarudisha hulka ya watu kujitambulisha kimaeneo badala ya kujitambulisha kama watanzania.
 
Kung'ang'ana na ujinga unao gharimu taifa eti kisa alianzialsha nyerere ni ujinga mkubwa zaid

Unatakiwa kujua enzi za nyerere hali ilikuwaje na sasa hali ikoje , mifumo ya nyerere kwa sasa haina nafasi maana ni mzigo mkubwa sana na ni ya kikolon sana
Mkoa mmoja una lundo la viongozi na wote wanatumia gharama kubwa za uendeshaji.

Hiyo hali ya sasa ina misingi ya zamani isiyokwepeka.

Msidanganywe na kina Tundu Lissu, mtakuja kulia kilio cha mbwa mdomo juu.
 
Wakati wa uhuru vita zilikuwa zimeshakuwa ni historia. Nyerere alijenga nchi kwa kutumia dhana ya kuwaunganisha watu.

Akavunja kabisa uchifu kwa kuwaona machifu ukuu wa mikoa na uwaziri ili tuongee lugha ya utanzania.

Ukirudisha majimbo unarudisha hulka ya watu kujitambulisha kimaeneo badala ya kujitambulisha kama watanzania.
Kwa iyo Nani kakwambia kurudisha majimbo ni kurudisha uchifu???? Hicho kichwa chako unafugia nywele tu???

Daaaah kweli dunia kuna vilaza 😂😂😀😂😀
 
Hiyo hali ya sasa ina misingi ya zamani isiyokwepeka.

Msidanganywe na kina Tundu Lissu, mtakuja kulia kilio cha mbwa mdomo juu.
Mbona Marekani hawaliii, Mbona Ujerumani hawalii???

Mbona kwa mfumo huu Tanzania ndo tunalia??? Wananchi wa kahama wanalalamika wana migodi ila hata barabara Nzuri na shule bora hamna???

Wananchi wa LINDI na Mtwara wanalia wana zao linaloongoza kwa kuingiza fedha za kigeni( korosho) , mbaazi na gesi Ila mikoa yao ina umasikini wa kutisha???!

Sasa kwa nini vilio vipo Tanzania na mfumo wetu wa mikoa???
 
Nigeria kuna ukabila uliojengwa kwa msingi wa majimbo yao. Wanajitambulisha kwa ukabila wao.

Sera ya majimbo itaigawa nchi.
Si kweli nigeria hakuna ukabila kwa kiwango unacho dai nimeishi huko tatizo lililopo ningeria kwa sababu hata tanzania kuna ukabila tena mkubwa tu

Nigeria makabila makubwa ni yoruba , wahausa na wa igbo hayo ndio makabila yaliyo dominate karibu 65% ya wa nigeria wote hivyo ukabila uliopo huko ni sawa tu na ule wa wasukuma na wachaga na wanyakyusa kwa hapa tanzania

Nigeria hakuna ukabila kama wa rwanda au kenya msiwe mnaongea vitu ambavyo hamvijui
 
Back
Top Bottom