Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.
Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.
Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?
Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.
Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.
Mkuu sio hivyo tu,unapozungumzia watu wa majimbo kujiamulia mambo yao wenyewe ni kudanganya watu.
Chukulia mfano Lissu mwenyewe alipokuwa mbunge,lini alitoa mawazo ya wapiga kura wake bungeni?
Chukulia mfano wa mwenyekiti wake kumpokea Lowassa 2015,lini Chadema ilikaa na kuamua? Haikuwa gia kubadilishia angani?
Chukulia mfano wa fedha za makato ya wabunge wenu,lini mlikaa na kubadilisha matumizi kutoka maandalizi ya uchaguzi,mpaka leo mnatembeza bakuli,huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja wa kuhoji maswala ya msingi kama;-
Michango ilifikia kiasi gani?
Nani aliidhimisha matumizi?
Kama hayo mnashindwa kuyatatua,itakuwaje kwenye majimbo?
HOJA YA PILI NI UKABILA WA MOJA KWA MOJA.
Huu ni ukweli kwa kuwa hakuna jimbo litakalo ajiri mtu kutoka jimbo lingine,kwa sababu za wazi,kwanza mtu wa kuja anaweza kuhujumu juhudi za maendeleo,pili mtu wa kuja ataathiri ajira za wazawa wa jimbo.
ELIMU.
Hili pia litajitokeza kwa sababu hakuna jimbo litakalo kubali kugharamia elimu ya mtu wa jimbo lingine,na kuacha mtu wa jimbo lake.
Mlolongo huu utakwenda kwa kila secta.
UCHOYO.
Majimbo masikini yatakuwa masikini zaidi,kwa sababu kila jimbo litakataa kusaidia maendeleo ya jimbo lingine.
UASI WA MAJIMBO TAJIRI.
Majimbo tajiri yatajiona ni bora kuliko mengine,mwisho wa siku yataona majimbo masikini yanawapotezea muda,hivyo kuomba jimbo tajiri lijitegemee,(liasi na kuwa nchi).