Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

USA ilipigana civil war, ni nchi iliyojengwa kwa misingi ya ubaguzi wa rangi.

Huwezi ukayalinganisha majimbo yao na hizi ndoto za alinacha za Lissu.

..jambo la msingi ni kuwepo kwa utawala unaotenda HAKI kwa watu wote.

..waliokuwa wakitetea UTUMWA ndiyo waliosababisha civil war ya Wamarekani.
 
..mbona sasa hivi kuna mikoa na wilaya?

..Je, kuna mkoa au wilaya unanyanyapaa mkoa au wilaya nyingine?

..Kwa mfano, wilaya ya Kinondoni imewahi kunyanyapaa wilaya ya Ilala?

..Au mkoa wa Geita umewahi kunyanyapaa mkoa wa Shinyanga, au Simiyu?

..hata wakati wa mkoloni na mara baada ya uhuru majimbo hayakuwa na matatizo.

..wananchi waliweza kutoka jimbo moja kwenda lingine kutafuta fursa.

..pia wapo watumishi wa serikali walikuwa wakihamishwa toka jimbo moja kwenda lingine.
Sioni umuhimu kwa Tanzania ya 2020 kuwa na serikali ya majimbo.

Upo udhaifu mwingi wa mfumo huu lakini bado hauhalalishi maamuzi ya nchi kugawa kwenye majimbo.
 
Sioni umuhimu kwa Tanzania ya 2020 kuwa na serikali ya majimbo.

Upo udhaifu mwingi wa mfumo huu lakini bado hauhalalishi maamuzi ya nchi kugawa kwenye majimbo.

..huo ni mtizamo wako na una kila haki ya kuutetea.

..sisi wengine msimamo wetu ni kuwepo kwa mfumo wa majimbo na tuna haki ya kutetea hoja hiyo.

..mfumo wa majimbo utakomesha utaratibu mbaya ulioko sasa hivi wa serikali kuu kuhodhi kila kitu.
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.

Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?

Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.

Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.
Usisahau kodi hawakusanyi, na atuambie deni la taifa tunagawana vipi kwenye majimbo?
 
Mtampa nchi ya Facebook na twitter hii inayoitwa Tanzania inabidi msahau.
We jamaa hivi una kura ya veto? Kwamba kura yako moja ni sawa na kura milioni 15 eeh? Huyo babu yenu mwambieni ajiandae kukabidhi nchi kwa lissu sawa?
 
..huo ni mtizamo wako na una kila haki ya kuutetea.

..sisi wengine msimamo wetu ni kuwepo kwa mfumo wa majimbo na tuna haki ya kutetea hoja hiyo.

..mfumo wa majimbo utakomesha utaratibu mbaya ulioko sasa hivi wa serikali kuu kuhodhi kila kitu.
Ukimaliza tatizo la kuhodhi utagundua kuwa umezalisha tatizo jingine jipya la matumizi ya rasilimali chache zilizopo.

Majimbo ni muendelezo wa ubinafsi na choyo tu za baadhi ya watanzania.
 
We jamaa hivi una kura ya veto? Kwamba kura yako moja ni sawa na kura milioni 15 eeh? Huyo babu yenu mwambieni ajiandae kukabidhi nchi kwa lissu sawa?
Lissu akipata nusu ya kura alizopata Lowassa yatakuwa ni mafanikio makubwa kwake.
 
Ukimaliza tatizo la kuhodhi utagundua kuwa umezalisha tatizo jingine jipya la matumizi ya rasilimali chache zilizopo.

Majimbo ni muendelezo wa ubinafsi na choyo tu za baadhi ya watanzania.

..madaraka yote kuhodhiwa sehemu moja, na mtu mmoja, ndio uchoyo na ubinafsi.

..lazima wananchi wawe na ngazi ya kiutawala zaidi ya moja inayoweza kutatua shida zao.

..mfumo tulio nao sasa hivi, serikali kuu ikifeli, basi wananchi huko chini hawana namna.

..mfumo wa majimbo utawezesha kuwepo kwa ngazi zaidi ya moja za utawala zinazo-complement one another.
 
Concept ya majinbo ,ni kutolaliana kuwa mnachangia gharama za uendeshaji jimbo kwa mgawanyo sawa na hakuna eneo linamlalia mwenzie chake.

Jimbo hugawanywa kwa mikoa lakini kila mkoa chake chake sio kuwa singida ataponea pesa zitazoingizwa morogoro hata kama wako jimbo moja isipokuwa kwa ile miradi ya pamoja.

Ukiunda jimbo ni kuwa mfano umeunda jimbo lenye mikoa miwili wa singida na kilimanjaro usidhani hapo kuwa pesa za utalii za kilimanjaro zitaenda singida .Haiwezekani .kodi kila mkoa unakusanya zake asilimia fulani ndio wanapeleka mfuko wa jimbo hawapeleki zote kwa ajili ya kugharimia gharama za uendeshaji wa jimbo. Lakini hakuna mkoa ambao utabeba mkoa mwingine kwa pesa zake kila mmoja anajibeba mweyewe.
hebu nitafutie katiba ya kenya tujifunze wao majimbo wanayaendeshaje,maana sijwasikia wanalalamikia serikali za majimbo kwamba zinawaletea umaskini
 
hebu nitafutie katiba ya kenya tujifunze wao majimbo wanayaendeshaje,maana sijwasikia wanalalamikia serikali za majimbo kwamba zinawaletea umaskini
Kwa hiyo Lisu kulazwa Kenya imekuwa nongwa hata katiba tunatakiwa ku copy na ku paste ya Kenya alikolazwa mheshimiwa mgombea Lisu!!!!! Na majimbo tu copy Kenya ha ha ha ha
 
Kwa huu mfumo wa Lissu, Singida itakuwa pamoja na mikoa gani kuunda jimbo moja?
 
Kwa hiyo Lisu kulazwa Kenya imekuwa nongwa hata katiba tunatakiwa ku copy na ku paste ya Kenya alikolazwa mheshimiwa mgombea Lisu!!!!! Na majimbo tu copy Kenya ha ha ha ha
duuh sikujua kama najadili na mtu anayeelewa masuala, kumbe najadili na mtu wa kuendekeza vijimambo!!!, kwanza mimi nilikuwa hata nimesahau kwamba lisu alilazwa nairobi, akili yangu ilizama kwenye mjadala, wa wanaounga mkono majimbo na wanaoipinga. ndio maana nikamkumbuka jirani yetu kenya yeye ana majimbo lakini hata siku moja sijasikia jimbo linalalamika halina mapato ya kutosha kulinganisha na jimbo fulani, the same goes to USA. tunapojadili masuala ya nchi ni vyema tukaexhaust kila kitu ili tunapokuja na jibu liwe la kusaidia nchi na si ushabikishabiki tu, wengine sisi hatuko kwenye politiki tuko kwenye masuala ya nchi, ndiyo maana Mwalimu Nyerere aliwaaambia waandishi tujadili masuala sio kuja na mswali mepesi
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.

Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?

Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.

Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.
Mkuu sio hivyo tu,unapozungumzia watu wa majimbo kujiamulia mambo yao wenyewe ni kudanganya watu.
Chukulia mfano Lissu mwenyewe alipokuwa mbunge,lini alitoa mawazo ya wapiga kura wake bungeni?
Chukulia mfano wa mwenyekiti wake kumpokea Lowassa 2015,lini Chadema ilikaa na kuamua? Haikuwa gia kubadilishia angani?
Chukulia mfano wa fedha za makato ya wabunge wenu,lini mlikaa na kubadilisha matumizi kutoka maandalizi ya uchaguzi,mpaka leo mnatembeza bakuli,huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja wa kuhoji maswala ya msingi kama;-
Michango ilifikia kiasi gani?
Nani aliidhimisha matumizi?
Kama hayo mnashindwa kuyatatua,itakuwaje kwenye majimbo?

HOJA YA PILI NI UKABILA WA MOJA KWA MOJA.
Huu ni ukweli kwa kuwa hakuna jimbo litakalo ajiri mtu kutoka jimbo lingine,kwa sababu za wazi,kwanza mtu wa kuja anaweza kuhujumu juhudi za maendeleo,pili mtu wa kuja ataathiri ajira za wazawa wa jimbo.
ELIMU.
Hili pia litajitokeza kwa sababu hakuna jimbo litakalo kubali kugharamia elimu ya mtu wa jimbo lingine,na kuacha mtu wa jimbo lake.
Mlolongo huu utakwenda kwa kila secta.
UCHOYO.
Majimbo masikini yatakuwa masikini zaidi,kwa sababu kila jimbo litakataa kusaidia maendeleo ya jimbo lingine.
UASI WA MAJIMBO TAJIRI.
Majimbo tajiri yatajiona ni bora kuliko mengine,mwisho wa siku yataona majimbo masikini yanawapotezea muda,hivyo kuomba jimbo tajiri lijitegemee,(liasi na kuwa nchi).
 
Back
Top Bottom