Lissu anapigania Mambo ya msingi kuliko hata Dudu Baya. Lakini angalia akili za wabongo wengi. Hopelessly

Lissu anapigania Mambo ya msingi kuliko hata Dudu Baya. Lakini angalia akili za wabongo wengi. Hopelessly

Hapa ndio umeongea points sana tujiwekeee sheria za kukataa lakini sio kumshambulia mtu
Sasa sheria za kwenye makaratasi zipo ila hazijaweza kusaidia na hakuna aliyewahi kutilia mkazo ndio maana Dudubaya akaamua kujitokeza na kulisimamia hilo
 
Mjadala wa Lisu upo lakini unapotezwa.
Angalia trend ya watu huko mitandaoni utaelewa
Kwa sasa la Dudubaya linatrend, ndio nimekuambia misimamo ya Lisu ni marathon, hilo la Dudubaya ni sprint. Haiwezakani watu wajadili la Lisu tu, lazima watajadili na mengine boss wangu.
 
Shida ya watu kama kina lisu wanabadikika wakipata wanachokitaka ila dudu hatobadilika anatupa nguvu ya kulinda bikra zetu
 
Mkuu Mtibeli, naomba nikupinge kidogo.

Kwanza, umaarufu wa jambo si kipimo cha akili za jamii wala umuhimu wa jambo. Mtu anaweza kujadili Dudu Baya leo kwa sababu ni burudani, na kesho akafuatilia kesi ya Lissu. Hayo hayapingani.

Pili, nadhani unalinganisha mambo mawili yaliyo kwenye mazingira tofauti. Suala la Dudu Baya wananchi wanaweza kuliathiri moja kwa moja kwa kumfuatilia, kumuunga mkono, kumkosoa au hata kuchangia. Lakini kesi ya Lissu iko kwenye mchakato wa mahakama; wananchi wanaweza kudai haki na kufuatilia, lakini uamuzi wa mwisho uko kwenye mhimili wa Mahakama.

Tatu, kusema watu wanachanga kwa Dudu Baya hakuthibitishi kwamba hawajali Lissu. Kunathibitisha tu kwamba wameamua kutumia muda au fedha zao kwenye jambo hilo. Trending si referendum ya akili za Watanzania.Halafu ni asilimia ngapi ya waTanzania wanafuatiliwa jambo Hilo la dudu baya?

Kwa hiyo mkuu, kama lengo ni kubadilisha fikra za Watanzania, tujadii kwa nini haki, utawala wa sheria na kesi ya Lissu ni muhimu, badala ya kutumia umaarufu wa Dudu Baya kama ushahidi kwamba Watanzania hawana akili.

Umaarufu wa Dudu Baya ni ushahidi wa umaarufu wake; si ushahidi wa ujinga wa Watanzania.
Hoja ya mtibeli ni dhaifu sana. Ukizingatia tafsiri halisi ya dhana "kuunga mkono" Lissu anaungwa mkono na Watanzania wengi kuliko Dudubaya. Unaweza kuunga mkono juhudi za mtu bila kelele. Lissu anaungwa mkono na watu wengi ambao wapo kimya for obvious reasons lakini wapo naye sana tu. Dudubaya akipitishwa njia anayopitia Lissu ndo utajua kwamba wanaomuunga mkono siyo wengi kwa kiwango kinachodhaniwa. Kushabikiwa kwa kelele nyingi hakumaanishi una wafuasi wengi.
 
Huko mbali, wengine hata kufuatilia muenendo wa case hawana huko mda, ndio kwanza utasikia, atajua yeye na chadema yake.
Raia wa hii nchi ni Maiti zinazotembea. Khaaah
Hawa usije kujaribu kuwapambania ni wajinga sana.
 
Wabongo wanasikitisha sana. Ni kama maroboti. Juzi Majezi feki kesho Nandy kavaa vibaya na Leo Dudu na Linda mgongo wako. Na watu hawashtuki.
Huo ndo mkakati wa ccm... Kuwafanya WaTanganyika wengi (wote ikiwezekana) kuwa propaganda bots.
 
Sasa sheria za kwenye makaratasi zipo ila hazijaweza kusaidia na hakuna aliyewahi kutilia mkazo ndio maana Dudubaya akaamua kujitokeza na kulisimamia hilo
Kazi ya kusimamia sheria ya nani ilo nalo tatizo kama taasisi inaweka sheria unashindwa kusimamia
 
Nakubaliana na Dudubaya kwa kile anachopigania ila kwa hii TZ!!
Inawezeakana ata uyo Dudubaya amepangwa ili kufifisha kufatilia mambo ya mcngi anayopigania Lissu..
 
Kazi ya kusimamia sheria ya nani ilo nalo tatizo kama taasisi inaweka sheria unashindwa kusimamia
Sheria zipo shida inakuja kwa jamii yote.
Kama hujaenda kumshitaki shoga wasimamizi wa sheria wataanzia wapi na watajuaje kuwa mtaani kwako kuna shoga?
 
Dudu baya ni project anafanya siyo bure kuna michezo tunachezewa, huwezi kuwa na akili timamu upoteze muda kwa ule ujinga
 
TUNDU LISSU ANAPIGANIA MAMBO YA MSINGI KULIKO HATA DUDU BAYA. LAKINI ANGALIA AKILI ZA WABONGO WENGI HOPELESSLY.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Ukitaka kujua akili za watu angalia yale wanayoyashabikia na kuyapigania. Hiyo itakupa picha upo na watu wa aina gani.

Tundu Lisu ni moja ya wapiganaji wa level za juu katika nchi hii ambapo mambo anayoyapigania yanagusa maisha ya watu moja kwa moja, kila familia, kila ukoo. Mtu yeyote.

Lisu anapigania haki mpaka za viongozi waliopo madarakani, usalama wa taifa, polisi, wanajeshi,magereza, watumishi wa umma na Watanzania wote.

Lisu anapigania HAKI, anataka jamii yehye kufuata sheria, yenye kutii sheria, yenye kuheshimu haki za binadamu.

Lisu hataki watu waonewe. Yeye huo ndio wimbo wake.

Kwa level ya elimu na kiwango cha maarifa alichonacho. Lisu angeweza kula na State, dola akakaa zake kimya maisha yakendelea. Na serikali ingemfaidi. Lakini yeye akachagua njia ngumu.

Dudu baya yeye kaja na Kupinga Ushoga. Kama nilivyosema yuko sawa.
Lakini mshtuko wangu upo hapa,
Uungwaji mkono kwa Dudu baya ni mkubwa sana.

Kila mtu YBWYB kila mtu Linda mgongo wako. Imefikia hatua watu wanachanga kwaajili ya Dudubaya.

Mpaka watu wanachapa Tsheti. Imagine.
Mpaka watu wanatukana basata.

Mpaka wasemaji wa timu za mipira nao. Wanamuunga mkono.
Yaani ni makundi mengi sana.

Lakini upande wa Lisu anayetetea Haki na mambo mengi na makubwa zaidi pamepoa.

Lisu anatetea haki sio tuu za wenye HAKI bali mpaka haki za waliokosea.
Kwamba huyu ni muuaji lakini naye anahaki zake. Yaani mnyonge mnyongeni lakini haki zake mpeni. Mnyongeni kwa kufuata taratibu.

Fikiria watu walivyokuwa wanatekwa alafu kila makundi ya watu wawe wanapiga kelele.

Embu angalia picha ikivuja ya uchi watu watakavyoishabikia. Wanajua kabisa ni uovu. Lakini wanashabikia.

Fikiria suala la Engonga yule aliyevujisha video za uchi. Angalia vijana wanavyompenda. Licha ya kuwa ule ulikuwa udhalilishaji. Unaweza ukaona upo kwenye jamii ya aina gani.

Fikiria ongezeko la single mothers ambapo ni matokeo ya ngono zembe na zinaa.
Unapinga Single mothers alafu upande wa pili wanaume wanajisifu kutia mimba wanawake hovyohovyo.

Jamii yetu inahitaji kubadilishwa kifikra ambapo ndio kazi kubwa kuliko kazi yoyote duniani.
Ni rahisi kubadilisha uchumi lakini ni ngumu sana kubadilisha fikra.

Kubadilisha mfumo wa utamaduni.

Watu kupambana na chanzo badala ya kupambana na matokeo.

Mimi nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Kahama, Shinyanga
Kwanza nikupe kongole mkuu🤝 leo sikuwa na hamu ya kureply chochote lakini kwa andiko hili umepiga point nzito nzito zote! hongera mkuu. Mimi nawewe tuko pamoja kumuunga mkono TAL Forever! Ni mwamba kweli kweli sio madem wengine kina bashite na wenzie wenye kufanana nae
 
Kwanza nikupe kongole mkuu🤝 leo sikuwa na hamu ya kureply chochote lakini kwa andiko hili umepiga point nzito nzito zote! hongera mkuu. Mimi nawewe tuko pamoja kumuunga mkono TAL Forever! Ni mwamba kweli kweli sio madem wengine kina bashite na wenzie wenye kufanana nae

Naam Mkuu
 
Back
Top Bottom