Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu amegoma kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili (kutokana na ratiba ya leo) hadi hapo hoja yake aliyoiwasilisha Mahakamani hapo itakapotolewa uamuzi na jopo la Majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru Baada ya Majaji kuingia kwenye chumba namba moja kwa ajili ya kuanza kusikiliza kesi hiyo kwa mujibu wa ratiba ya leo, Jumanne Septemba 16.2025.
Lissu amewaeleza Majaji hao kuwa alipoingia kwenye chumba cha Mahakama hajawakuta wafuasi wake na kwamba amepata taarifa kuwa wamegoma kutokana na baadhi ya wanachama wenzao kuzuiliwa kuingia Mahakamani na maafisa wa Jeshi la Polisi.
Kutokana na hoja hiyo, Lissu ameomba Mahakama kutoa muongozo wake wa haraka na kuhoji inawezekanaje ZCO anaawafukuza watu Mahakamani na Mahakama iko kimya?, pia amesema Majaji pekee ndio wenye mamlaka ya kutoa amri yoyote Mahakamani sasa inawezekanaje mtu mwingine anatoa amri ndani ya viunga vya Mahakama, amri ambazo pia zinakinzana na sheria na taratibu?
Baada ya kuwasilisha hoja hiyo, Lissu aliieleza Mahakama kuwa hawezi kuendelea na kesi hadi suala hilo litolewe muongozo na Mahakama, na kwamba hadi wafuasi wake waruhusiwe kuingia Mahakamani.
Baada ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga aliiomba Mahakama kuendelea ratiba ya usikilizwaji wa kesi kutokana na kwamba suala analowasilisha Lissu halina uhalisia, lakini pia Katuga amesema wafuasi hao walikuwepo kwenye chumba cha Mahakama na wametoka muda mfupi kabla ya kesi kuanza .
Sambamba na hilo Wakili Katuga amesema baadhi ya watu wako Mahakamani na wanasikiliza kesi bila kikwazo, (hata hivyo watu hao CHADEMA wanadai kuwa si wanachama wao bali ni askari waliovaa kiraia) Ikimbukwe kuwa katika uwasilishaji wa hoja yake Lissu alibainisha kuwa kesi hiyo ni ya wazi, na kwamba kinachofanyika sasa hakina uhalisia wa uwazi wa Mahakama Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru wanaosikiliza kesi hiyo, wameahirisha kesi hiyo kwa muda hadi saa tano watakaporejea kutoa 'uamuzi.