Valuhwanoswela
JF-Expert Member
- Jun 27, 2019
- 1,228
- 1,127
Rais ndo anatakiwa aombe radhi kwa Serkali yake kutuma wanaojulikana kumshambulia Lissu akiwa kazini akiwatumikia wananchi. Hakuna laana hapo maana ingekuwepo rusasi moja tu toka kwenye silaha ile ya kivita, ingemuondoa duniani. Risasi 16 mwilini kati ya 36 zilizopigwa na sharpshooters waliobobea na kuchaguliwa kwa makiniMambo yaliyomtokea Lissu mimi naona ni laana kutokana na kejeli dharau na matusi aliyomfanyia Rais Magufuli siku za mwanzo za utawala wake.
Rais Magufuli ni mtu mwenye imani ya Mungu. Kwa wale wenye kumbukumbu siku za mwanzo utawala wa Magufuli kuna viongozi wa CHADEMA walionesha uhasama mkubwa kwa Magufuli wakiongozwa na Lissu. Walichukia na hawakuamini kushindwa uchaguzi japo kwa kila dalili CCM ilionekana wangeshinda. Inaelekea Lissu mwenye imani kubwa na mabeberu wa kizungu baada ya kuhakikishiwa na wao wangeshinda hakuamini kushindwa.
Hapa ninakumbusha kauli ya kejeli na dharau ya Tundu Lissu nje ya Mahakama Kisutu mbele ya waandishi wa habari aliposema kwa kejeli na dharau huku akivuta mdomo '...katika nchi hii haijawahi kutokea rais wa hovyo kama Magufuli' kisha akasema 'narudia tena' akarudia maneno yake. Binafsi nilisikitika na kumuonea huruma lLssu.
Hivi leo binafsi naona yaliyompata Lissu kama laana kutokana na kumkejeli na kumdharau pia kumtusi kiongozi na mtu mwema anayependwa sana na wananchi. Badala ya Lissu kuendelea kutumika na ubeberu na hadi viongozi wa vyama vya mashoga arudi na kuomba msamaha.
Viongozi nchini mashuhuri kama Kinana wameomba radhi baada ya kumkosea Rais Magufuli ndio itakuwa Lissu?