Uchaguzi 2020 Lissu aonya juu ya mkakati wa nia ovu ya kumuengua baada ya watawala kupagawa kwa kimbunga chake mikoani, asema hilo halitofanikiwa

Yaani mwaka huu kuna kuna Bundi huko CCM. Wagombea wao hadi sasa hawajui hatima yao. Na muda unazidi kuyoyoma. Hii hali ilikuwa ikiwakuta wapinzani miaka ya nyuma. This time kibao kimebadilika.

Kuna mvutano mkubwa kuliko ule wa kusimamishwa kwa Membe. Mwisho wa siku wataamua kuwasimamisha walioshinda kula kutoka kwa wenye njaa!
 
Wajaribu, wathubutu, tutawafundisha adabu, watajuta!
Sema ujasiri wa watanzania upo kwenye keyboard.

Tanzania ingekuwa na watu jasiri serious kama John Heche, Tundu Lisu. HALIMA MDEE , John Mnyika na wengine kama hao angalau 1000, utawala wa kimabavu wa ccm ungeshafika kikomo miaka 10 iliyopita.

Nchi hii ujinga umetamalaki, raia hawajui haki zao za msingi na wanaojaribu kuwaelimisha kuhusu haki zao wanaonekana wasaliti.
Serikali ikitimiza wajibu wake kama kujenga barabara na miundombinu mingine , wananchi wengi kutokana na ujinga wao wanahisi wanafanyiwa upendeleo.

Baadhi ya watanzania ni sawa na mtu ambaye anatoa hela kwenye ATM halafu anaishukuru ATM kwa kumpa pesa ambazo ni zake.
 
2022 atakuwa mtu wa kawaida tu akipishana na mawakili wengine, kisutu na mahakama zingine hana hata baunsa
 
Lissu the great!!

Naogopa sana CCM wasije wakamponza Jaji wetu wa uchaguzi!!

Suala la kumwengua Lissu kwa sababu zisizo za kisheria linaweza kuwa na madhara makubwa kwa nchi.

Kuhusu huyu kada wa CCM Nape kwenye tweet kusema ati " kwenye siasa ukiwa tunaongea peke yako na wengine wapo kimya jiandae kuna jambo kubwa laja juu yako"

Hapa nafikiri alikuwa anampiga dongo Mwenyekiti wake aliyeongea miaka 5 peke yake...

Huu ni muda wa wengine nao kuongea....wananchi wana shauku kujua na kusikia toka kwa kina Lissu sasa!!

Kwenye mchezo huu wa siasa usiwe na hasira...ni lazima kujikaza!!

Go Lissu Gooooo!!
 
Huyu jamaa anashida kichwani maana alituambia Magu ameanza kutoa rushwa mapema leo anasemaje
Wewe una akili timamu kweli?

Kwa hiyo kuna rushwa za kucheleweshwa na rushwa za mapema,

Basically alichosema Lisu ni kwamba Magufuli kutoa pesa wakati ameshavaa kofia ya kugombea urais ni sawa na kutoa rushwa.
 
Hata hivyo tuko pazuri mno.
 
Na iweje bodi ya mikopo ya elimu ya juu tanzania kuanza kupokea pesa za wahitaji kabla ya matokeo? au ufaulu ni lazima kwa wote? ila tofauti ni vigezo vinginevyo? kunako hasi , chanya haikosekani!!
Mkuu naona umepiga msumari kuliko! Tusubiri jibu.
 
Sheria ilimaanisha baada ya kuteuliwa na chama chako usianze kampeni kabla Tume haijakupitisha.Lissu anacheza na akili zenu ambazo siku zote hazitaki kufikiri.
Mkuu najua unajua ulichokiandika siyo sahihi. Chama chako kikikupitisha na NEC (tume ya taifa ya uchaguzi) ikawa haijakupitisha bado, hapo wewe hata ukiongea unaongea na wanachama wako tu. Ndiyo maana sheria inamtambua mtu kuwa ni mgombea pale tu akishateuliwa na NEC. Tarehe ya uteuzi ni tarehe 25 August. Kama kwa mfano kampeni zingekua zimepangwa kuanza tr 1 September, mtu ambaye ameshateuliwa na tume akianza kampeni kabla ya tr 1 September atakua ameanza kampeni kabla.
 
Yaani kumchagua lisu tumepotea sana wanachadema
Lisu ana akili nyingi sana lakini hana hekima kabisa
..afadhali ya nyarandu mara mia kuliko lisu
Naomba msinifokee maoni yangu tu..
Mkuu mbna wewe umeshatufokea? Baada ya hapo tuambie wapi amekosa hekima?
 
Puguza upayukaji, wote walielezea malengo yao baada ya kuchukua fomu, wapo walioahidi ubwabwa, hata jpm alisema ya kwake
 
Nilikuwa kijijini juzi. Kati ya watu 100 wanaomjua lissu ni watatu, hawezi kuwa Raisi
 
Again nakuambia, kukutana na watu siyo lazima uhutubie Mkutano wa hadhara.Ukifuatilia mikutano ya Lissu haina tofauti na kampeni anasimama kila eneo anahutubia siyo kwenye Ofisi za chama pekee.

Yes tumetekeleza na hatuna uoga wowote na maigizo yananyofanywa. Nyinyi mnasema kila siku mnamuhitaji huyu bwana ili asimamie utawala sheria lakini cha ajabu ameanza kuzivunja hizo sheria kabla hata hajaanza kuzisimamia.
 
Ni wivu tu. Watu wanamfata fata. Na ndio maana akisimamishwa barabarani hafanyi mkutano anawasalimia tu. Akifika ofisi ya chama ndio anaongea na wananchi kuhusu vidonda na operesheni zake ambazo nyie mnaponda.
 
Yani unavyoongea Kama unazijua sheria za uchaguzi? , Sio kutujazia saver tu hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…