Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
Nimemuona Lissu anawashambulia sana akina Halima Mdee na wenzake badala ya kutengeneza Mazingira rafiki ya kurudisha wale Viongozi ambao CHADEMA imetumia muda wake mwingi kuwaandaa, na hasa ukichukulia toka wameisaliti hawajawahi kuisema vibaya Taasisi wala Viongozi wao.
Uongozi siyo Sheria tu mara nyingine ni hekima na busara na hapa ndiyo utaona Lissu anapungukiwa.Naongea hivi kwasababu kuna wakati nilisikia baadhi ya hao Wabunge 19 walikuwa wanataka kurudi kwenye Chama chao ila kwa Mazingira anayotengeneza Lissu siwaoni wakirudi na kiuhalisia wakienda CCM itakayopoteza ni CHADEMA.Huwezi kupuuza nguvu za akina Mdee,Bulaya,Matiko etc hasa ukichukulia wakitoka Bungeni hata kiuchumi watakuwa wameimarika kidogo.
Chama cha Siasa ni watu tunahitaji Wanachama hata kama wanatoka CCM ila wanakubali kufuata Misingi ya Chama tuwachukue kuimarisha Chama,katika hili Lissu anashindwa kuonyesha Uongozi anachokionyesha ni harakati na hasira.
Povu linaruhusiwa.