Lissu aonyeshe Uongozi katika suala la akina Halima Mdee na Wenzake,aachane na hayo mambo yake

Nimemuona Lissu anawashambulia sana akina Halima Mdee na wenzake badala ya kutengeneza Mazingira rafiki ya kurudisha wale Viongozi ambao CHADEMA imetumia muda wake mwingi kuwaandaa, na hasa ukichukulia toka wameisaliti hawajawahi kuisema vibaya Taasisi wala Viongozi wao.

Uongozi siyo Sheria tu mara nyingine ni hekima na busara na hapa ndiyo utaona Lissu anapungukiwa.Naongea hivi kwasababu kuna wakati nilisikia baadhi ya hao Wabunge 19 walikuwa wanataka kurudi kwenye Chama chao ila kwa Mazingira anayotengeneza Lissu siwaoni wakirudi na kiuhalisia wakienda CCM itakayopoteza ni CHADEMA.Huwezi kupuuza nguvu za akina Mdee,Bulaya,Matiko etc hasa ukichukulia wakitoka Bungeni hata kiuchumi watakuwa wameimarika kidogo.

Chama cha Siasa ni watu tunahitaji Wanachama hata kama wanatoka CCM ila wanakubali kufuata Misingi ya Chama tuwachukue kuimarisha Chama,katika hili Lissu anashindwa kuonyesha Uongozi anachokionyesha ni harakati na hasira.

Povu linaruhusiwa.
Kwamba afumbie macho? Kwanza huna logic, si kila kitu ni busara? Kiongozi ni maamuzi
Hao 19 kesi yao haikuisha ilikuwa paused na mwrnyekit aliepita. Mwenyeki wa sasa nataka taratibu zifuatwe na maelezo yanyooke

Watu design yako ya kufunika kilinda linda uzembe hamfai nchi hii
 
Mleta mada ana hoja ya msingi, kipindi hiki ikibidi hata kuungana na shetani ni kuungana naye ili kupamabana na adui. Wakina mdee bado wana ushawishi mkubwa sana hilo halipingiki, Ila tuachie muda ndio utakao ongea.
Usbawishi wa kina mdee si mkubwa tema kama hapo nyuma, after making the deal with the devil u.aarufu ukashuka na ushawish chamani bawana tena. It time waje nyumbani au waende walipo make deal
 
Kwamba afumbie macho? Kwanza huna logic, si kila kitu ni busara? Kiongozi ni maamuzi
Hao 19 kesi yao haikuisha ilikuwa paused na mwrnyekit aliepita. Mwenyeki wa sasa nataka taratibu zifuatwe na maelezo yanyooke

Watu design yako ya kufunika kilinda linda uzembe hamfai nchi hii
Na watu wa hivyo ndio wameifikisha nchi hii hapa ilipo.

Imefikia wakati sasa Tanzania imejengeka mindset kukiuka utaratibu kwenye kila jambo ndio ujanja, na kufuata utaratibu ni ushamba!
 
Mkuu
Nimemuona Lissu anawashambulia sana akina Halima Mdee na wenzake badala ya kutengeneza Mazingira rafiki ya kurudisha wale Viongozi ambao CHADEMA imetumia muda wake mwingi kuwaandaa, na hasa ukichukulia toka wameisaliti hawajawahi kuisema vibaya Taasisi wala Viongozi wao.

Uongozi siyo Sheria tu mara nyingine ni hekima na busara na hapa ndiyo utaona Lissu anapungukiwa.Naongea hivi kwasababu kuna wakati nilisikia baadhi ya hao Wabunge 19 walikuwa wanataka kurudi kwenye Chama chao ila kwa Mazingira anayotengeneza Lissu siwaoni wakirudi na kiuhalisia wakienda CCM itakayopoteza ni CHADEMA.Huwezi kupuuza nguvu za akina Mdee,Bulaya,Matiko etc hasa ukichukulia wakitoka Bungeni hata kiuchumi watakuwa wameimarika kidogo.

Chama cha Siasa ni watu tunahitaji Wanachama hata kama wanatoka CCM ila wanakubali kufuata Misingi ya Chama tuwachukue kuimarisha Chama,katika hili Lissu anashindwa kuonyesha Uongozi anachokionyesha ni harakati na hasira.

Povu linaruhusiwa.
Mkuu hakuna busara katika kukabiliana na usaliti uliothibitika.
 
Back
Top Bottom