Kwanza nitangaze Mgongano wa Maslahi kwamba mimi pia ni Shabiki wa Lissu, naheshimu mchango wake katika kupigania mabadiliko ya nchi hii na natambua na kuheshimu gharama alizolipa kwa kwa kazi hiyo kwa ajili ya Taifa hili.
Ila siku za Karibuni ameanza kufanya Siasa fulani hivi za kutuhumu Viongozi wake hadharani masuala ya Rushwa bila ushahidi wa moja kwa moja jambo ambalo nadhani kisiasa lilipaswa kushughulikiwa katika Vikao vya ndani vya Chama.Ninajua Lissu anafahamu kuwa maneno yake yanaharibu taswira ya Viongozi wenzake na Chama chake ingawa yanamjenga yeye Binafsi.
Ninafahamu CCM kwa muda mrefu wanafanya jitihada za kumuondoa Mbowe bila mafanikio na ni kwasababu wanajua Nguvu ya Mbowe katika Uimara wa CHADEMA, na inaeleweka Propaganda nyingi wanaanzisha wao ikiwemo ya kuwagonganisha Lissu na Mbowe kutengeneza Mpasuko na kuisambaratisha CHADEMA.
Tukumbushane CCM imechokwa CHADEMA haijipangi ila tunahitaji Upinzani imara,kuanguka kwa CHADEMA ni hasara kwetu wote siyo kwa Lissu na Mbowe tu kwasababu ndiyo Voice ya Voiceless pekee iliyobaki.
Naomba walioko Karibu na Lissu wamshauri atumie Vikao vya ndani kuepuka kuimarisha Propaganda za CCM na kukidhoofisha Chama chake.
Yanga Bingwa.
Lissu anafanya siasa za ukweli anajaribu kukiokoa chama kirudi kwenye misingi yake ya hapo awali kupinga vita ufisadi, rushwa, kudai katiba mpya, tume huru, chaguzi huru za haki ndani ya chama na nje ya chama.
Maridhiano:- aliyapinga na alijua ni uhuni baada ya mikutano miwili tu. Yakaendelea mwaka mzima ahadi za, ruzuku, asali, ubunge,uwaziri, anasema ilikuwa ni ujinga kuamini hivyo na kupewa nusu mkate kama Zanzibar. Wanajificha kufanya maridhiano kwa siri badala ya uwazi kushirkisha Watanzania wote na vyama vyote. Msidaganywe na kutiana ujinga. Mtu anayefiria hivyo ana akili au kuna jambo.
Mtoa mada jibu swali la Lissu.
Rushwa:- Lissu anasema:- Morogoro wamesimamisha wagombea 62 kati ya zaidi 200 kwa kukosa pesa lakini chaguzi za ndani kuna pesa nyingi sana. Lazima tukemee siasa chafu kwenye siasa za chadema. Kujipanga upya. Hoja ya msingi. Haki, demokrasia. Kuna uchafu, rushwa hata kwetu.
Ni pesa za kwetu, kama sio za kwetu ni za Nani?
Lissu anauliza. Mleta mada mpe majibu.
Lissu anaendelea tukampa tuzo ya maridhiano, ndio maana picha zake zimepachikwa kila sehemu.
Tubadilishe tactics, tusiwachekee CCM. Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi kwa gharama zozote zile. Huu uchaguzi umepita ttujipange upya.
Mwelekeo, agenda kuu ya chama iwe katiba mpya, tume huru. Huu ukimya unamsaidia Nani, kama hatuwezi kusemea haya tusemee nini. Anauliza Lissu.
Mbowe is not conviction politicians but businessman in politics. For him it is all about money. Toka jela stop ya kwanza ikulu, lowassa, sumaye.
Angekuwa zito angetukanwa. Magu hakutoa dau kubwa la kutosha ila naamini angefanya hivyo Mbowe angeshirikiana naye vizuri tu.
Lissu ni asset kubwa kwa Chama, mpeni uenyekiti. Muungeni mkono 100% muone Chadema itakavyo songa mbele haraka.