Pre GE2025 Lissu ashauriwe apunguze kutuhumu wenzie bila Ushahidi, anagharimu Chama chake kwa kucheza ngoma ya CCM bila kujijua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Upinzani ili uwe imara, unahitaji Siasa za kiaharakati Kwasababu ndizo zenye kubeba Hisia, na MTU pekee katika Hilo ni LISSU.

Siasa za mbowe, na genge lake, zinaifànya CDM ionekane ni TLP tu au CCM B
 
Kwanza nitangaze Mgongano wa Maslahi kwamba mimi pia ni Shabiki wa Lissu,
Mambo mawili hapa:
Kwanza, japo wewe ni shabiki wa lisu, lakini inaelekea humjui lisu ktk uhalisia wake. Lisu ni aina ya watu wasioshaurika. Yeye hujiona anajua kila kitu, na anajua kuliko watu wengine wote. Mtu wa aina hiyo huwezi kumshauri kitu chochote.
Pili, kwa kuwa wewe ni shabiki wake, nadhani wewe na washabiki wake wengine ndio mko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumshauri (kama atasikiliza ushauri wenu). Unataka nani amshauri kama siyo nyie washabiki wake? Unataka sisi tusiomshabikia ndio tumshauri?
Btw, hiyo mikosoo yake kwa chama chake ni mikakati ya kuelekea 2025, ambapo yeye tayari ameshajitangaza kuwa mgombea. Anajitafutia umaarufu ili muda ukifika apite kwa kishindo!
 
Tuwe wakweli tu, tatizo ni Mbowe, kwa mazingira yalivyo unaweza kuweka kikao cha kumjadili mwenyekiti kula rushwa? Inawezekana njia ya Lisu kuweka ukweli hadharani sio nzuri, lakini ndio njia pekee. Mbowe akubali tu wakati ukuta, apishe wengine kwa sasa.
isu anakwenda kuishia kama mrema! time will tell!
 
Kwanza nitangaze Mgongano wa Maslahi kwamba mimi pia ni Shabiki wa Lissu, naheshimu mchango wake katika kupigania mabadiliko ya nchi hii na natambua na kuheshimu gharama alizolipa kwa kwa kazi hiyo kwa ajili ya Taifa hili.

Ila siku za Karibuni ameanza kufanya Siasa fulani hivi za kutuhumu Viongozi wake hadharani masuala ya Rushwa bila ushahidi wa moja kwa moja jambo ambalo nadhani kisiasa lilipaswa kushughulikiwa katika Vikao vya ndani vya Chama.Ninajua Lissu anafahamu kuwa maneno yake yanaharibu taswira ya Viongozi wenzake na Chama chake ingawa yanamjenga yeye Binafsi.

Ninafahamu CCM kwa muda mrefu wanafanya jitihada za kumuondoa Mbowe bila mafanikio na ni kwasababu wanajua Nguvu ya Mbowe katika Uimara wa CHADEMA, na inaeleweka Propaganda nyingi wanaanzisha wao ikiwemo ya kuwagonganisha Lissu na Mbowe kutengeneza Mpasuko na kuisambaratisha CHADEMA.

Tukumbushane CCM imechokwa CHADEMA haijipangi ila tunahitaji Upinzani imara,kuanguka kwa CHADEMA ni hasara kwetu wote siyo kwa Lissu na Mbowe tu kwasababu ndiyo Voice ya Voiceless pekee iliyobaki.

Naomba walioko Karibu na Lissu wamshauri atumie Vikao vya ndani kuepuka kuimarisha Propaganda za CCM na kukidhoofisha Chama chake.

Yanga Bingwa.
 
Lissu alidai Abdul alienda nyumbani kwake na mmoja wa viongozi wa Chadema kutaka kumuhonga apunguze ukali kwa madam presso sasa anyamaze maana huyo aliyempekeka ni dhahiri mla rushwa.
 
Lisu ameamua kumwaga ugali
Anakwenda kupita kama Mrema na wengine....
Kuna wakati wa kusema ukweli na wakati wa kuusema ukweli faragha, maana unaangalia useme ukweli wapi! Mke wako akizini huwezi kusema hadharani kuwa Mke wangu amezini na fulani, utaoneka kichaa! Unasema faragha, then ikishindikana unajitoa kwake.
sasa Lisu anazamisha mtumbwi aliopanda! Atazama
 
Leo nimekuwa chawa kwa kuwa tu nimeandika ukweli usiopenda!??
CDM ikiendelea kulea watu namna yako, itatukimbiza wengi tunaoipenda,kuiamini na kuisaidia kuing'oa CCM.
My point ni: kuna wakati wa kusema ukweli hadharani na kuusema faragha!

Unausema hadharani unajibomoa, unakigawa chama, is this akili njema?

Unajua kabisa kuwa kuna adui wako CCM and will bank on that kukubomoa.....unakomaa na kushupaza shingo eti unasema ukweli. Unatoboa mtumbwi uliopanda, UTAZAMA.

HAKUNA ANAYEPENDA RUSHWA, IKEMEWE KWA NGUVU LAKINI YOU HAVE TO CHOOSE THE SAFE WAY TO DO THAT! SIIPENDI RUSHWA LAKINI UKIIKEMEA HAPHARZADLY, UTAJIBOMOA Erythrocyte
 
Lissu alidai Abdul alienda nyumbani kwake na mmoja wa viongozi wa Chadema kutaka kumuhonga apunguze ukali kwa madam presso sasa anyamaze maana huyo aliyempekeka ni dhahiri mla rushwa.
Huyo kiongozi kwanini hamtaji anatoka tu hadharani na ngonjera? Mbona Abdul kamtaja? Anamaslahi gani kwa kumficha huyo kiongozi?! Upumbafu
 
My point ni: kuna wakati wa kusema ukweli hadharani na kuusema faragha!

Unausema hadharani unajibomoa, unakigawa chama, is this akili njema?

Unajua kabisa kuwa kuna adui wako CCM and will bank on that kukubomoa.....unakomaa na kushupaza shingo eti unasema ukweli. Unatoboa mtumbwi uliopanda, UTAZAMA.

HAKUNA ANAYEPENDA RUSHWA, IKEMEWE KWA NGUVU LAKINI YOU HAVE TO CHOOSE THE SAFE WAY TO DO THAT! SIIPENDI RUSHWA LAKINI UKIIKEMEA HAPHARZADLY, UTAJIBOMOA Erythrocyte
Huyu kama hajatumwa basi kaamua tukose wote yeye akimbilie Ubelgiji
 
Upinzani ili uwe imara, unahitaji Siasa za kiaharakati Kwasababu ndizo zenye kubeba Hisia, na MTU pekee katika Hilo ni LISSU.

Siasa za mbowe, na genge lake, zinaifànya CDM ionekane ni TLP tu au CCM B
Mbowe amewashika sana vijana njaa ,hata ukitokea uchafu hawakubali tofauti yao na vijana wa CCM ni rangi ya sare zao.

Kuna watu sijawahi sikia wanagombania nafasi ila miaka na miaka wapo pale pale tena hakuna Positive wanatotoa mfano Mrema.

Pia kuna vijana wanaojifanyachama ni mali ya baba yao kuna yule Ntobi na Martin hawa majamaa wana matusi na kashfa sana aisee.
 
Kwanza nitangaze Mgongano wa Maslahi kwamba mimi pia ni Shabiki wa Lissu, naheshimu mchango wake katika kupigania mabadiliko ya nchi hii na natambua na kuheshimu gharama alizolipa kwa kwa kazi hiyo kwa ajili ya Taifa hili.

Ila siku za Karibuni ameanza kufanya Siasa fulani hivi za kutuhumu Viongozi wake hadharani masuala ya Rushwa bila ushahidi wa moja kwa moja jambo ambalo nadhani kisiasa lilipaswa kushughulikiwa katika Vikao vya ndani vya Chama.Ninajua Lissu anafahamu kuwa maneno yake yanaharibu taswira ya Viongozi wenzake na Chama chake ingawa yanamjenga yeye Binafsi.

Ninafahamu CCM kwa muda mrefu wanafanya jitihada za kumuondoa Mbowe bila mafanikio na ni kwasababu wanajua Nguvu ya Mbowe katika Uimara wa CHADEMA, na inaeleweka Propaganda nyingi wanaanzisha wao ikiwemo ya kuwagonganisha Lissu na Mbowe kutengeneza Mpasuko na kuisambaratisha CHADEMA.

Tukumbushane CCM imechokwa CHADEMA haijipangi ila tunahitaji Upinzani imara,kuanguka kwa CHADEMA ni hasara kwetu wote siyo kwa Lissu na Mbowe tu kwasababu ndiyo Voice ya Voiceless pekee iliyobaki.

Naomba walioko Karibu na Lissu wamshauri atumie Vikao vya ndani kuepuka kuimarisha Propaganda za CCM na kukidhoofisha Chama chake.

Yanga Bingwa.
Aliekwambia kua ccm imechokwa nani ??
 
Upinzani ili uwe imara, unahitaji Siasa za kiaharakati Kwasababu ndizo zenye kubeba Hisia, na MTU pekee katika Hilo ni LISSU.

Siasa za mbowe, na genge lake, zinaifànya CDM ionekane ni TLP tu au CCM B
Una akili Carlo
 
Mambo mawili hapa:
Kwanza, japo wewe ni shabiki wa lisu, lakini inaelekea humjui lisu ktk uhalisia wake. Lisu ni aina ya watu wasioshaurika. Yeye hujiona anajua kila kitu, na anajua kuliko watu wengine wote. Mtu wa aina hiyo huwezi kumshauri kitu chochote.
Pili, kwa kuwa wewe ni shabiki wake, nadhani wewe na washabiki wake wengine ndio mko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumshauri (kama atasikiliza ushauri wenu). Unataka nani amshauri kama siyo nyie washabiki wake? Unataka sisi tusiomshabikia ndio tumshauri?
Btw, hiyo mikosoo yake kwa chama chake ni mikakati ya kuelekea 2025, ambapo yeye tayari ameshajitangaza kuwa mgombea. Anajitafutia umaarufu ili muda ukifika apite kwa kishindo!
Utumbo huu tuchanganye na mboga gani za majani
 
Anakwenda kupita kama Mrema na wengine....
Kuna wakati wa kusema ukweli na wakati wa kuusema ukweli faragha, maana unaangalia useme ukweli wapi! Mke wako akizini huwezi kusema hadharani kuwa Mke wangu amezini na fulani, utaoneka kichaa! Unasema faragha, then ikishindikana unajitoa kwake.
sasa Lisu anazamisha mtumbwi aliopanda! Atazama
Kumbe wewe ni chawa wa mbowe?
Hata akiharibu unamsifia tu?
Uhai wa cdm kwasasa ni Lissu pekee.

Hakuna hotuba inafuatiliwa kama ya Lissu.
Hata ccm wenyewe wanaogopa Lissu akihutubia
 
Una ushahidi, uweke hadharani...it seems wewe ID hii ndiwe Lisu! 😀 😀 😀 😀
Usipokuwa muumini wa ukweli, msimamo wako ni rahisi kuyumba. Kwani kuna ulazima gani wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti tena kwa muda aliokaa madarakani? Nasisitiza kwa sasa Mbowe ndio tatizo halisi ndani ya cdm. Sipingi unachoamini, lakini taasisi inayotegemea kiongozi king'ang'anizi wa madaraka aina ya Mbowe ni ngumu pia kupata mafanikio.
 
My point ni: kuna wakati wa kusema ukweli hadharani na kuusema faragha!

Unausema hadharani unajibomoa, unakigawa chama, is this akili njema?

Unajua kabisa kuwa kuna adui wako CCM and will bank on that kukubomoa.....unakomaa na kushupaza shingo eti unasema ukweli. Unatoboa mtumbwi uliopanda, UTAZAMA.

HAKUNA ANAYEPENDA RUSHWA, IKEMEWE KWA NGUVU LAKINI YOU HAVE TO CHOOSE THE SAFE WAY TO DO THAT! SIIPENDI RUSHWA LAKINI UKIIKEMEA HAPHARZADLY, UTAJIBOMOA Erythrocyte
Ukiona ukweli unasemwa hadharani, ujue humo ndani ukweli haupewi nafasi, hasa ukweli huo unapotaka kuusema uwe sio unaotakiwa na mwenyekiti.

Naona unalazimisha kuwa Lisu anaweza kuwa kama Mrema, kwanini usione kama anaweza kuwa kama Maalim Seif aliopoondoka CUF na kwenda ACT, hadi leo CUF imekuwa mahututi? Ni hivi, muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti umeshapita, tena alitangaza mwenyewe ikifika 2023/24 ataachia uenyekiti. Ni vyema kwa sasa ungehoji anatekeleza hiyo ahadi yake? Au kwa ID hii ww ndio Mbowe?
 
Kwanza nitangaze Mgongano wa Maslahi kwamba mimi pia ni Shabiki wa Lissu, naheshimu mchango wake katika kupigania mabadiliko ya nchi hii na natambua na kuheshimu gharama alizolipa kwa kwa kazi hiyo kwa ajili ya Taifa hili.

Ila siku za Karibuni ameanza kufanya Siasa fulani hivi za kutuhumu Viongozi wake hadharani masuala ya Rushwa bila ushahidi wa moja kwa moja jambo ambalo nadhani kisiasa lilipaswa kushughulikiwa katika Vikao vya ndani vya Chama.Ninajua Lissu anafahamu kuwa maneno yake yanaharibu taswira ya Viongozi wenzake na Chama chake ingawa yanamjenga yeye Binafsi.

Ninafahamu CCM kwa muda mrefu wanafanya jitihada za kumuondoa Mbowe bila mafanikio na ni kwasababu wanajua Nguvu ya Mbowe katika Uimara wa CHADEMA, na inaeleweka Propaganda nyingi wanaanzisha wao ikiwemo ya kuwagonganisha Lissu na Mbowe kutengeneza Mpasuko na kuisambaratisha CHADEMA.

Tukumbushane CCM imechokwa CHADEMA haijipangi ila tunahitaji Upinzani imara,kuanguka kwa CHADEMA ni hasara kwetu wote siyo kwa Lissu na Mbowe tu kwasababu ndiyo Voice ya Voiceless pekee iliyobaki.

Naomba walioko Karibu na Lissu wamshauri atumie Vikao vya ndani kuepuka kuimarisha Propaganda za CCM na kukidhoofisha Chama chake.

Yanga Bingwa.
Lissu anafanya siasa za ukweli anajaribu kukiokoa chama kirudi kwenye misingi yake ya hapo awali kupinga vita ufisadi, rushwa, kudai katiba mpya, tume huru, chaguzi huru za haki ndani ya chama na nje ya chama.

Maridhiano:- aliyapinga na alijua ni uhuni baada ya mikutano miwili tu. Yakaendelea mwaka mzima ahadi za, ruzuku, asali, ubunge,uwaziri, anasema ilikuwa ni ujinga kuamini hivyo na kupewa nusu mkate kama Zanzibar. Wanajificha kufanya maridhiano kwa siri badala ya uwazi kushirkisha Watanzania wote na vyama vyote. Msidaganywe na kutiana ujinga. Mtu anayefiria hivyo ana akili au kuna jambo.

Mtoa mada jibu swali la Lissu.

Rushwa:- Lissu anasema:- Morogoro wamesimamisha wagombea 62 kati ya zaidi 200 kwa kukosa pesa lakini chaguzi za ndani kuna pesa nyingi sana. Lazima tukemee siasa chafu kwenye siasa za chadema. Kujipanga upya. Hoja ya msingi. Haki, demokrasia. Kuna uchafu, rushwa hata kwetu.
Ni pesa za kwetu, kama sio za kwetu ni za Nani?

Lissu anauliza. Mleta mada mpe majibu.

Lissu anaendelea tukampa tuzo ya maridhiano, ndio maana picha zake zimepachikwa kila sehemu.

Tubadilishe tactics, tusiwachekee CCM. Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi kwa gharama zozote zile. Huu uchaguzi umepita ttujipange upya.

Mwelekeo, agenda kuu ya chama iwe katiba mpya, tume huru. Huu ukimya unamsaidia Nani, kama hatuwezi kusemea haya tusemee nini. Anauliza Lissu.

Mbowe is not conviction politicians but businessman in politics. For him it is all about money. Toka jela stop ya kwanza ikulu, lowassa, sumaye.

Angekuwa zito angetukanwa. Magu hakutoa dau kubwa la kutosha ila naamini angefanya hivyo Mbowe angeshirikiana naye vizuri tu.

Lissu ni asset kubwa kwa Chama, mpeni uenyekiti. Muungeni mkono 100% muone Chadema itakavyo songa mbele haraka.
 
Back
Top Bottom