Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
Ni mjinga pekee ndiyo anaweza kuunderestimate Nguvu ya Mbowe ndani ya CHADEMA, Namshauri Lissu awamu hii akubali amekosea hesabu zake za kisiasa na ni wazi hatamuweza Mbowe atashindwa ila anaweza kurekebisha Makosa baada ya awamu hii kama kweli bado atakuwa anahitaji kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kipindi Mbowe anang'atuka.
Siasa ni sayansi siyo porojo au maneno makali pekee,Kiukweli kwa jinsi Mbowe alivyoijenga CHADEMA na kuweka Mizizi huwezi kukurupuka na kuona Mbowe si lolote si chochote ndani ya CHADEMA ukategemea kushinda haitakuwa rahisi, ni muhimu kutambua na kuheshimu hiyo nguvu yake na kuangalia namna ya kuiingiza katika timu yako ya Kampeni.
Kwahiyo kama Lissu atakuwa anahitaji kuwa Mwenyekiti aachane kabisa na hayo mambo yake ya kumtukana,kumdhalilisha,kumtweza,kumfedhehesha nk amlete Karibu amuombe amsaidie kufikia azma yake hiyo.
Na Kampeni ni Field siyo Mitandaoni pekee,Lissu aingie front Vijijini kama Mbowe akajenge Chama huko atengeneze Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa kutosha huku kwenye Uchaguzi wa Taifa awe anamalizia tu Uchaguzi.
Haya ni maoni na mawazo yangu tu ila kama ataendelea kuwasikiliza hao akina Msigwa,Lema na Heche basi ni juu yake waendelee tu kumshambulia Mbowe kwa Mikutano,Interviews na Mitandao watapata Kiti.
Ni Mtazamo tu masela msijenge Chuki,Povu linaruhusiwa kabisa.