ze future
JF-Expert Member
- Jan 2, 2020
- 204
- 303
Kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Mhe. Rais John Pombe Magufuli na ndugu Tundu Lissu kwa kuteuliwa na vyama vyao(CCM na CHADEMA) kuwa wagombea urais katika uchaguzi huu wa mwezi Oktoba, Niende kwenye hoja ya hapo juu ya kuwa Bwana Lissu bila kupinga atashinda sana mioyo ya watu wengi kwa kuwa na historia yake ya kupigwa risasi na mpaka sasa kuwa mgombea uraisi wa nchi lakini Mhe. Rais John Pombe Magufuli atashinda kura za watu wengi kwa juhudi alizozifanya katika kipindi chake cha uongozi.