Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katika sheria za Tanzania, kuna sehemu yoyote inayotamka hivi; kwamba "... mchakato ni lazima upate baraka za Mh Rais wa JMT"?, au huu ni ujinga tu unaotumika kupotosha watu?
Umekomaa kiasi cha mtu kudhani na kufikiri kuwa labda unakijua hata hicho ulichokikomalia, kumbe masikini huna lolote ulijualo au umeamua kujifyatua kwa makusudi hizo akili ili nia yako ovu ya kupotosha ukweli ifanikiwe. Sasa na kuambia hivi, HUWEZI!Hao wanaolialia na katiba mpya si ndiyo walifyatuka bunge la katiba pamoja na akina Prof Lipumbu wakaenda kuanzisha UKAWA huku wakigomea makubaliano ya wengi ndani ya bunge la katiba? Sasa wanahangaika na nini tena hawa akina Lissu! Wacha katiba ya sasa iendelee, sitaki kusikia tena katiba mpya! Mmesikia?
.
Fisadi KuuHe is talking too much, anaenda kuwa irrelevant soon huyu Lissu
Hivi hiyo katiba mpya ni kwaajili ya HAO walioamua KUTAFUTA Kwa mbinu zao binafsi au ni Kwa watanzania wote?
Kama Kuna watu wanataka katiba mpya na wengine hawataki basi wote Wana haki Sawa.
Issue ya wasiojulikana wapo nchi zote na malengo Yao ni kuondoa SUMU mbaya pamoja na wapika SUMU ili waliowengi wasiangamie Kwa SUMU.
Wanasiasa ni watu wapuuzi sana, kwa sasa Mimi sitetei uwepo wa katiba wala nini
Kwa sababu kipimdi kile cha katiba ya Walioba, waliingiza siasa zao na Lissu akiwepo, badala ya katiba kuzungumzwa kama suala la kitaifa, walilibeba kuwa la kisiasa utadhani ni mashindano ya Chadema na CCM wakidhani kwamba, chadema ama CCM watakaozidiwa hoja za kisiasa katika katiba waonekane mambumbumbu kitu ambacho haikuwa hivyo
Machakato wa Katiba ni lazima ubebe sura ya kitaifa
Namuasa Mh Raisi wetu, hata atakapoamua mchakato wa katiba uwepo, asitupelekee wanasiasa ktk bunge hilo la katiba,
Wachambuliwe watanzania waungwana ambao watachambua katiba yetu bila mwelekeo wa kisiasa, kama ilivyokuwa tume ya madini, basii!
Tundu, zito, nape, msukuma, mbowe, n.k, tupa kulee wote
Kuna haja watanzania tukapiga kura kuamua wenyewe tunaitaka au hatuitaki katiba mpya maana kuna watu sasa wanataka kuwa wasemaje wetu..
Nafanje ili niweze kuona hiyo attachment?nisaidieni!Wanabodi, sehemu ya mazungumzo ya fuatayo ni msimamo wa Lissu dhidi ya watu husika na mambo tajwa hapo juu.
Mengi amewahi kuonya ama kuyaweka bayana na yakajiri, alikuwa wa kwanza kusema wazi wazi Magufuli ni dikteta na Rais wa ajabu, akasema kuhusu watu wasiojulikana na mauaji ya MKIRU,yalijiri!!
Zaidi msikilize Lissu mwenyewe kwenye kiambatbishi!
View attachment 2163100
Maridhiona sio kelele za mitandaoni. Mbona hizo kelele hazishindi chaguzi, hazibadilishi Katiba wala hazileti Tume Huru?Zile sauti za "Mbowe sio gaidi" mpaka DPP akaweka mpira kwapani zilisikika toka Namtumbo au?
For sure watanzania wengi tunataka katiba mpya ikiwamo mimi, lakini si kwa njia za mikato au za kupeana hisani na watu ambao wanajidai wanajali maslahi yetu kumbe wapo kuzingatia yao kwanza na kutumia agenda hii njema kujihakikishia wao watakuwa wafaidika wakwanza.Sasa kama Watanzania hawataki katiba mpya kazi ya Warioba kukusanya maoni alipewa ya nini ..... na wale waliotoa hayo maoni walitoka wapi kama Watanzania hawaitaki katiba mpya. Na kama handiyo mawazo yako mbona huyatumii hayo majibu yako kwenye Tume huru anayotaka kutuletea Maza kupitia Kikosi kazi chake (SHAMBA LAKE)....!!?
Kaporwa au kutokuporwa ndio kuwa irrelevant huko. Angekuwa relevant unafikiri angeporwa?
Ukiwa na dhamira njema hata ukali unapata nguvu, but when you are not straight nani atakubali ukali wako? Ukali lazima uwe na justifications;Wakati wa CDM ya DR Slaa umuweke Mbowe jela miezi 8 thubutu yake? Utaanzia wapi kwanza. Kidogo kidogo watamkubali JPM kwamba Maguvu na ukichaa wake vilihitajika kuonesha serikali iko.
Unaongea ukiwa wapi Bawacha? Ni muda wenu huu wa Space..Hilo neno relevant unalitumia ili uonekane umeenda shule, lakini sioni hata kama unajua unachoongea
Ukiwa na dhamira njema hata ukali unapata nguvu, but when you are not straight nani atakubali ukali wako? Ukali lazima uwe na justifications; JPM had, kwasababu alibeba agenda ya kitaifa hata kama ana weaknesses zake lakini he had moral authoritu mbele ya jamii kubwa ya Tanzania kwakua aligusa interests za wengi.
Unaongea ukiwa wapi Bawacha? Ni muda wenu huu wa Space..
Sawa ChibaPunguza utoto dogo.
Hili haliepukiki kwani Wamachinga, Mfumuko wa Bei, Wasio na Ajira, Waliokosa Mkopo wa Elimu ya juu, Wanaosumbuliwa ktk kupata Mafao yao yaani mambo yapo mengi kwa hiyo hili ni jeshi kamili lililokosa Kamanda.Kwa nini Lissu na CDM waachiwe ionekane Katiba mpya ni agenda yao na si ya Watanzania wote? Wakati kimsingi mchakato lazima upate baraka za Mh Rais wa JMT.
Kuhusu katiba mpya ni bora maamuzi yakafanyika mapema maana muda si rafiki tena na katiba haiepukiki.
Katiba ni kitu muhimu kwa afya ya Taifa hili, haita kuwa busara ije kupatikana kipindi joto limeshakuwa kubwa na penginepo lisilo weza kuwa controlled. Kwa nini muwape hawa vibaraka wa Wazungu cha kuongea huko duniani? Makabrasha ya katiba mpya yako yanapigwa vumbi itisheni kura ya maoni.
Sababu za Marehemu JPM kusema mchakato wa katiba na uweka pembeni haziishi leo tena. Kwa mfano Wamachinga walioipokea hiyo kauli ya JPM kwa mikono miwili leo Lissu akiwafuata akawaambia Katiba mpya ni muhimu hawatamuelewa vizuri na kumbeba juujuu?
So Katiba mpya haiepukiki tengenezeni utaratibu mchakato uanze muda hauko upande wenu.