Lissu atoa msimamo rasmi dhidi ya Rais Samia, Zitto Kabwe, Katiba Mpya na ACT Wazalendo

Kuna haja watanzania tukapiga kura kuamua wenyewe tunaitaka au hatuitaki katiba mpya maana kuna watu sasa wanataka kuwa wasemaje wetu..
 
Katika sheria za Tanzania, kuna sehemu yoyote inayotamka hivi; kwamba "... mchakato ni lazima upate baraka za Mh Rais wa JMT"?, au huu ni ujinga tu unaotumika kupotosha watu?

Nimetumia uzoefu wa 2010 mchakato ulianzishwa/ ulipata baraka za Mh Rais Mstaafu Mzee JK Kikwete.

Na amini aliongozwa na sheria na si akili zake.

Wakati huo msimamo wangu ulikuwa ni ama serikali tatu au moja.
 
Umekomaa kiasi cha mtu kudhani na kufikiri kuwa labda unakijua hata hicho ulichokikomalia, kumbe masikini huna lolote ulijualo au umeamua kujifyatua kwa makusudi hizo akili ili nia yako ovu ya kupotosha ukweli ifanikiwe. Sasa na kuambia hivi, HUWEZI!

Ni ushauri tu kuwa, unapo - argue juu ya jambo fulani, jitahidi uwe na ufahamu na uelewa kuhusu jambo hilo

FACT #1 ya UKAWA na BLK;

Kama hujui chanzo cha kuundwa kwa UKAWA, acha tukulishe kumbukumbu

Kwamba, UKAWA ni kifupisho cha maneno "UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI". Chanzo cha kuundwa kwa umoja huu ni mtafaruku uliotokea ndani ya BLK ambapo CCM kwa nguvu ya uwingi wao waliipindua RASIMU YA WARIOBA iliyotokana na MAONI YA WANANCHI nchi nzima na kiujanja ujanja wakaingiza rasimu yao

Kuona hivi, waliokuwa upande wa Tume ya WARIOBA na wananchi, wakakataa kuubariki unajisi huo. Wakatoka nje na kuwaacha waliotaka kupitisha haramu waendelee na uharamu. Nafsi zikawasuta, wakaona aibu na wao hao wakaweka mpira kwapani na mchezo mzima ukaisha hapo

FACT #2 ya UKAWA na BLK;

Kama huna kumbukumbu na ufahamu, ni kwamba, kiuhalisia CCM ndiyo waliovuruga mchakato wote wa kupata katiba mpya mwaka 2014 because of their self dangerous political desires of remaining into power by whatever means possible kama tu ambavyo wanaendelea kukomaa hadi sasa kupitia huyu mama yenu Hangaya

However, walikuwa na uwezo wa kuendelea mpaka wapate haramu yao kwa sababu hata bila UKAWA kuwepo ndani ya BLK, bado CCM walikuwa na majority kupitisha hiyo katiba.

Ndo kusema basi kuwa, UKAWA hawakuwazuia CCM na vibaraka wao kufanya lolote na chochote walichotaka. UKAWA, simply refuted to participate in endorsing something which was illegal..!!

Hivyo kama ni kukwama kwa mchakato wa kupata katiba mpya mwaka 2014, watu sahihi wa kuulizwa ni CCM kwanini hawakusonga mbele kumalizia mchakato haramu kwa kuifanyia endorsement katiba haramu. Waulize waligwaya na kuogopa nini.!??
 
Wanasiasa ni watu wapuuzi sana, kwa sasa Mimi sitetei uwepo wa katiba wala nini

Kwa sababu kipimdi kile cha katiba ya Walioba, waliingiza siasa zao na Lissu akiwepo, badala ya katiba kuzungumzwa kama suala la kitaifa, walilibeba kuwa la kisiasa utadhani ni mashindano ya Chadema na CCM wakidhani kwamba, chadema ama CCM watakaozidiwa hoja za kisiasa katika katiba waonekane mambumbumbu kitu ambacho haikuwa hivyo

Machakato wa Katiba ni lazima ubebe sura ya kitaifa

Namuasa Mh Raisi wetu, hata atakapoamua mchakato wa katiba uwepo, asitupelekee wanasiasa ktk bunge hilo la katiba,

Wachambuliwe watanzania waungwana ambao watachambua katiba yetu bila mwelekeo wa kisiasa, kama ilivyokuwa tume ya madini, basii!

Tundu, zito, nape, msukuma, mbowe, n.k, tupa kulee wote
 

Asiyetaka katiba mpya sasa ila baadaye anapata wapi uhalali wa kuwazuia wanaoitaka sasa?
 

Wanasisasa wao ni ulaji tu. Bunge la JMT na lile SMZ walitikiwa watoe wawakilishi kama makundi mengine wakaingia wote humo.

Hilo huwezi kumsikia Lissu wa Msigwa kuliongelea wakamua wavute mafao ya pande zote huku na huku.
 
Kuna haja watanzania tukapiga kura kuamua wenyewe tunaitaka au hatuitaki katiba mpya maana kuna watu sasa wanataka kuwa wasemaje wetu..

Kura iwe ile ya utaratibu wa mwaka 1947 kusimama nyuma ya unachokichagua
 
Nafanje ili niweze kuona hiyo attachment?nisaidieni!
 
Zile sauti za "Mbowe sio gaidi" mpaka DPP akaweka mpira kwapani zilisikika toka Namtumbo au?
Maridhiona sio kelele za mitandaoni. Mbona hizo kelele hazishindi chaguzi, hazibadilishi Katiba wala hazileti Tume Huru?

Hizo kelele hazikufanikiwa hata kuleta maandamano ya UKUTA sembuse vitu vikubwa kama Katiba?

Mtadanganyana na kupotezeana usingizi sana huko Space..
 
For sure watanzania wengi tunataka katiba mpya ikiwamo mimi, lakini si kwa njia za mikato au za kupeana hisani na watu ambao wanajidai wanajali maslahi yetu kumbe wapo kuzingatia yao kwanza na kutumia agenda hii njema kujihakikishia wao watakuwa wafaidika wakwanza.
 
Wakati wa CDM ya DR Slaa umuweke Mbowe jela miezi 8 thubutu yake? Utaanzia wapi kwanza. Kidogo kidogo watamkubali JPM kwamba Maguvu na ukichaa wake vilihitajika kuonesha serikali iko.
Ukiwa na dhamira njema hata ukali unapata nguvu, but when you are not straight nani atakubali ukali wako? Ukali lazima uwe na justifications;

JPM had, kwasababu alibeba agenda ya kitaifa hata kama ana weaknesses zake lakini he had moral authority so as Dr. Slaa is, mbele ya jamii kubwa ya Tanzania kwakua waligusa interests za wengi.

Msiseme tu ooh mkali, jaribu wewe kuwa alafu uwe corrupt uone nchi itakavyosambaratika!
 

Na kiongozi yeyote anaye shindwa kujua wengi ni wapi na niendenao vipi jua huyo keshashindwa ni suala la muda tu.

Natamani sana makundi mbalimbali ya kijamii yangelichukua mfano wa bongo fleva katika kudai haki zao.

Mbona kingeeleweka tu.
 
Chadema hadi sasa hawajaweka hadharani msimamo wao…Uchaguzi wa 2025 kama Msimamo wa Serikali utakuwa twende kwny uchaguzi huo bila ya Katiba mpya watashiriki au wataususia?
 
Hili haliepukiki kwani Wamachinga, Mfumuko wa Bei, Wasio na Ajira, Waliokosa Mkopo wa Elimu ya juu, Wanaosumbuliwa ktk kupata Mafao yao yaani mambo yapo mengi kwa hiyo hili ni jeshi kamili lililokosa Kamanda.

Mama na Chama changu tuwemakini na upepo unavyovuma kabla madhara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…