Ni kweli maana haiwezekani wabunge 30 waende wote Dubai ?nani alilipa gharama zao zote za wabunge wa Jamhuri ya Muungano .
Wakati kamati za kudumu za bunge la Muungano hazina idadi hiyo kubwa ya wabunge mfano LAAC, PAC, Miundo-mbinu, Mambo ya Nje na Ulinzi kwa kutaja kwa uchache ambao wajumbe chache ndiyo hutakiwa kuzama sana kuelewa miswada, miradi n.k Sana kundi lote hilo kuhamia Dubai ni harufu ya rushwa na kupewa milungula
TOKA MAKTABA :
Kamati ya Bunge ya LAAC imetembelea Mradi wa Machinjio ya Kisasa Ndembezi
View attachment 2662515
Kamati ya Bunge ya (LAAC) imetembelea Mradi wa Machinjio ya Kisasa Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga na kuuagiza Uongozi wa Manispaa hiyo kufanya jitihada za maksudi kuimarisha eneo la Masoko kwa kuongeza idadi ya mbuzi na ngombe wanaotakiwa kuchinjwa ili mradi uwe na tija.
Akizungumza mara baada ya Wajumbe wa LAAC, Makamu Mwenyekiti Mhe. Selemani Zedi akasema kamati inashauri licha ya kukamilika kwa mradi huo lakini idadi ya ngombe wanaotakiwa kuchinjwa haitoshi kulingana na uwezo wa machinjiyo hayo.
“Tumeona mradi umekamilika na umeanza kufanya kazi lakini tulichobaini ni kwamba mradi ni mkubwa lakini kwa sasa hakuna ngombe na mbuzi wa kutosha kufikia kiwango cha uzalishaji kilichopo.
Ameongeza kwamba lengo la miradi ya kimkakati ni kuzifanya halmashauri zijitegemee ziwe na vyanzo vya mapato hivyo kuutaka uongozi wa Manispaa ya Shinyanga kuongeza ubunifu ili mradi huo uwe na manufaa zaidi.
Spika afanya mabadiliko ya Wajumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI
View attachment 2662516
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko ya Wajumbe wote Ishirini na nne (24) wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kwa kuunda upya kamati hiyo na kuteua wajumbe Wapya Kumi na sita (16) ambao pia watakuwa ni wajumbe katika kamati nyingine za Kudumu za Bunge.
Mabadiliko haya yamelenga kuwawezesha Wabunge kujifunza na kujipatia uelewa na uzoefu zaidi katika kutekeleza shughuli mbalimbali za Kamati za Bunge ambapo Wabunge wote waliokuwa Wajumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI hapo awali, wamepangiwa Kamati zingine kwa nia ya kuboresha Utekelezaji wa majukumu ya kibunge.
Msingi wa Mabadiliko haya unatokana na Ibara ya 96 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inayolipa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kuunda Kamati za Bunge za namna mbalimbali kadri linavyoona inafaa kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake na Kanuni ya 116 (3) – (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 inampa Spika Mamlaka ya kuteua Wabunge ili wawe Wajumbe katika Kamati mbalimbali za Bunge ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya kuongeza, kubadilisha au hata kupunguza idadi ya Wajumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge.
Kwa mujibu wa waraka Na.5/2016 wa Mhe. Spika kwa Wabunge wote wa Tarehe 7 Oktoba, 2016, Mabadiliko haya yataanza kutekelezwa mara moja kuanzia mwezi huu Oktoba, 2016 ambapo Wajumbe husika watakutana kwa ajili ya kufanya Uchaguzi wa Viongozi wao na kuandaa Ajenda za Vikao vya Kamati. Orodha ya wajumbe wapya 16 wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI na orodha ya wajumbe 24 waliobadilishwa kutoka kamati hiyo na Kamati mpya ni kama ifuatavyo:-
ORODHA YA WAJUMBE WAPYA WA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI
__________________________________________
NA. | JINA | KAMATI YAKE NYINGINE |
1. | Mhe. Asha Abdullah Juma, MB | Pia ni Mjumbe wa Katiba na Sheria |
2. | Mhe. Daniel Edward Mtuka, MB | Pia ni Mjumbe wa Sheria Ndogo |
3. | Mhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile, MB | Pia ni Mjumbe wa Huduma na Maendeleo ya Jamii |
4. | Mhe. Dkt. Hadji Hussein Mponda, MB | Pia ni Mjumbe wa PAC |
5. | Mhe. Dkt. Jasmine Tiisekwa Bunga, MB | Pia ni Mjumbe wa Huduma na Maendeleo ya Jamii |
6. | Mhe. Gibson Blasius Meiseyeki, MB | Pia ni Mjumbe wa Katiba na Sheria |
7. | Mhe. Joseph Kizito Mhagama, MB | Pia ni Mjumbe wa Katiba na Sheria |
8. | Mhe. Juliana Daniel Shonza, MB | Pia ni Mjumbe wa Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama |
9. | Mhe. Kemirembe Julius Lwota, MB | Pia ni Mjumbe wa Ardhi, Maliasili na Utalii |
10. | Mhe. Lucia Ursula Michael Mlowe, MB | Pia ni Mjumbe wa Huduma na Maendeleo ya Jamii |
11. | Mhe. Mary Deo Muro, MB | Pia ni Mjumbe wa Miundombinu |
12. | Mhe. Martha Mlata, MB | Pia ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira |
13. | Mhe. Masoud Abdalla Salim, MB | Pia ni Mjumbe wa Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama |
14. | Mhe. Oscar Rwegasira Mukasa, MB | Pia ni Mjumbe wa Nishati na Madini |
15. | Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, MB | Pia ni Mjumbe wa Viwanda , Biashara na Mazingira |
16. | Mhe. Yussuf Kaiza Makame, MB | Pia ni Mjumbe wa Nishati na Madini |
ORODHA YA WALIOKUWA WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA
UKIMWI NA KAMATI WALIZOHAMISHIWA
NAMBA | JINA | KAMATI
ALIYOHAMISHIWA |
| Mhe.Hassna Sudi Katunda Mwilima,Mb | Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama | |
| Mhe.Constantine John Kanyasu,Mb | Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) | |
| Mhe. Muhammed Amour Muhammed,Mb | Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) | |
| Mhe. Sixtus Raphael Mapunda,Mb | Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) | |
| Mhe.Juma Kombo Hamad,Mb | Katiba na Sheria | |
| Mhe. Mattar Ali Salum,Mb | Kilimo, Mifugo na Maji | |
| Mhe.Savelina Sylvanus Mwijage,Mb | Huduma na Maendeleo ya Jamii | |
| Mhe. Khalifa Mohammed Issa,Mb | Utawala na Serikali za Mitaa | |
| Mhe.Abdallah Haji Ali,Mb | Hesabu za Serikali(PAC) | |
| Mhe. Waitara Mwita Mwikabe,Mb | Utawala na Seikali za Mitaa | |
| Mhe. Khamis Yahya Machano,Mb | Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama | |
| Mhe.Sikudhani Yasini Chikambo,Mb | Huduma na Maendeleo ya Jamii | |
| Mhe. Zuberi Mohamedi Kuchauka,Mb | Miundombinu | |
| Mhe. Mgeni Jadi Kadika,Mb | Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) | |
| Mhe. Hussein Nassor Amar,Mb | Huduma na Maendeleo ya Jamii | |
| Mhe.Richard Philip Mbogo,Mb | Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) | |
| Mhe. Grace Victor Tendega,Mb | Huduma na Maendeleo ya Jamii | |
| Mhe. Elibariki Emmanuel kingu,Mb | Sheria Ndogo | |
| Mhe. John Peter Kadutu,Mb | Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) | |