Akiongea na waandishi wa habari, leo ndugu Tundu Lissu ameelezea kirefu taarifa za njama za kumuengua kugombea kupitia kumfungulia mashitaka mapya ya papo kwa papo pindi akienda kusikiliza mashauri yake ya zamani.
Lissu amesema taarifa za uhakika walizo nazo kutoka katika vyanzo vya taarifa ndani ya serikali ni kuwa, mpango uliosukwa ni kuwa tarehe 26 imechaguliwa makusudi kwa sababu tarehe hiyo ndiyo tarehe pia ambayo kama kuna mapingamizi huko NEC ya kugombea, basi mgombeaji anapaswa awepo kuyajibu. Hata hivyo kwa upande wa Lissu tarehe hiyohiyo amepangiwa awepo mahakamani kuendelea na mashauri yake. Lissu amesema taarifa walizonazo ni kuwa akifika mahakamani atasomewa mashitaka mengine mapya ya papo kwa papo, kunyimwa dhamana kisha kesi kuahirishwa tarehe ya kutajwa na kisha kunyimwa dhamana ili asiweze kwenda NEC kujibu mapingamizi yoyote yatakayoibuliwa na hivyo kuwa kuondolewa katika kugombea!
Lissu amesema, kuwa kesi za jinai ni kesi za hadhara ambapo umma unaruhusiwa kwenda kuzisikiliza, hivyo anawataka wananchi wa Dar na mikoa ya jirani wahudurie mahakamani siku hiyo!
Pamoja na shauri lake kutajwa tarehe hiyo, Lissu hajawwka wazi msimamo wake kuwa Je atakwenda yeye binafsi au hatakwenda, lakini kwa jibu alilolitoa kwa mwandishi wa habari ameonyesha kuwa Jambo la kugombea ambayo ni haki yake ya kikatiba analipa kipaumbele zaidi.
Kwa habari zaidi tazama video hii: