Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mgombea wa Uenyekiti CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, amewasili Mlimani City akiwa ndani ya gari alilopigiwa risasi na watu wasiojulikana mjiji Dodoma mwaka 2017 likiwa bado na alama za risasi katika ubavu wa kushoto ambao alikaa wakati akishambuliwa, ambapo leo Januari 21, 2025 unafanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa juu wa chama hicho.
Soma, Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti & Makamu Mwenyekiti 2025: Ni Mbowe au Lissu?
Lissu amewasili katika viwanja vya ukumbi huo saa 10:15 asubuhi, akiwa ndani ya gari jeusi la Land Cruiser lenye namba za usajili T216 DHH. Kitendo cha Lissu kuingia Mlimani City akiwa ndani ya gari aliyopigwa nayo risasi, tena ikiwa bado na matundu ya risasi, kumeibua hamasa kubwa kutoka kwa wafuasi wake.
Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana