Pre GE2025Lissu awasili Mlimani City akiwa ndani ya gari yake aliyopigwa nayo risasi Dodoma na watu wasiojulikana, tena ikiwa bado na matundu yake ya risasi
Mgombea wa Uenyekiti CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, amewasili Mlimani City akiwa ndani ya gari alilopigiwa risasi na watu wasiojulikana mjiji Dodoma mwaka 2017 likiwa bado na alama za risasi katika ubavu wa kushoto ambao alikaa wakati akishambuliwa, ambapo leo Januari 21, 2025 unafanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa juu wa chama hicho.
Lissu amewasili katika viwanja vya ukumbi huo saa 10:15 asubuhi, akiwa ndani ya gari jeusi la Land Cruiser lenye namba za usajili T216 DHH. Kitendo cha Lissu kuingia Mlimani City akiwa ndani ya gari aliyopigwa nayo risasi, tena ikiwa bado na matundu ya risasi, kumeibua hamasa kubwa kutoka kwa wafuasi wake.
Mgombea wa Uenyekiti CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, amewasili Mlimani City akiwa ndani ya gari alilopigiwa risasi na watu wasiojulikana mjiji Dodoma mwaka 2017 likiwa bado na alama za risasi katika ubavu wa kushoto ambao alikaa wakati akishambuliwa.
Labda nikose kitu cha kufanya kabisa yaani hata kulala kuwe tena siyo kitu cha muhimu ndiyo na mimi nitasema sasa ngoja nikasukume gari la mwanasiasa kuonyesha mahaba kwamba namkubali sana.
Huyu ndiye atanifanya niendelee kuwa Chadema ama lah
Haya yote, ni siku hii hii ya leo kati ya hayo mawili, moja litakuwa chaguo langu, na wala stajutia kwa lolote kama ambavyo nimekuwa sijutii kuwa Chadema kipindi kirefu kilichopita,
Chadema inapojinadi kuwa chama cha Demokrasia basi ni mhimu itofautiane na vyama vyote maana huko kote kuna kusiginwa wazi wazi kwa katiba zao pia katiba ya nchi
Labda nikose kitu cha kufanya kabisa yaani hata kulala kuwe tena siyo kitu cha muhimu ndiyo na mimi nitasema sasa ngoja nikasukume gari la mwanasiasa kuonyesha mahaba kwamba namkubali sana.