Uchaguzi 2020 Lissu aweza kuwanadi wagombea Ubunge & Udiwani

Uchaguzi 2020 Lissu aweza kuwanadi wagombea Ubunge & Udiwani

Watumishi wote na familia zao kura kwa lissu

Mungu kumbuka chozi langu dhidi ya mja wako Lissu nililotoa wakati ameumizwa.Endelea kumlinda,kumbariki Na kumpa nguvu.

Amen
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Kassim Majaliwa akiendelea kupita sehemu mbalimbali kuwanadi wabunge na madiwani wa CCM .

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA na mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA naye ana haki ya kuwanadi wabunge na madiwani wa CHADEMA.
Wazungu wanasema

Ngoma inogile
 
Vipi kuhusu haki stahiki anazopewa na dola akiwa kama mgombea urais (mfano ulinzi ), je ataendelea kupewa akianza kupiga kampeni kama m/mwenyekiti?

Kama jibu ni hapana. Itakuwaje kuhusu usalama wake?
Ulinzi mbona anapewa hadi nyumbani au ofisini kama mgombea. Hivyo hata atakapofanya shughuli zingine za chama bado hadhi ya ugombea urais IPO palepale.
 
Mgombea wetu wa CCM ndiyo maana alikazana Sana kununua wabunge wa chadema kuepuka sekeseke la kampeni.

Kumbe afya ni mgogoro!
Kweli hakuna kitu kichwani na amezungukwa na wanaoogopa kumwambia kweli, yeye alikuwa busy na kutumia rasilimali kununua wapigiwa kura badala ya wapiga kura.

Ndio maana haamini na kuna mbunge mmoja mwarabu mfipa wa chama kikongwe aliwahi kusema Magufuli hata akikaa nyumbani bila kampeni atapita tu

Akaamini, na hali anayokutana nayo ya Spana za TAL lazima aende gereji wakaweke grease kidogo
 
lissu anasema ana kikao cha kamati yake leo.
hivyo atasikiliza maamuzi ya kamati.

lakini msimamo wake binafsi ni kuendelea na kampeni wa nafasi nyingine aliyonayo"kuwanadi wagombe wa viti vingine"

hapa amekiri kosa,na kukubaliana na adhabu,ni vyema busara ikatumika aachwe afanye kinachomruhusu.
 
Wakuu heshima sana,

Sheria Number 5 ya mwaka 1992 viongozi ngazi ya kitaifa wa fursa ya kuwanadi wagombea Ubunge & Udiwani nchi nzima.

Kwakuwa Tume ya Uchaguzi imemzuia Lissu kufanya kampeni kwa siku saba, Lissu atatumia nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti Taifa kuwanadi wagombea Ubunge na Udiwani.

Ukijua hili wenzako wanajua kule

Ngongo safarini Zanzibar Kibanda maiti.
Tuko nyuma yako MH. TAL, tumia fursa yoyote itakayopatikana kuwapelekea tetemeko 'mabwana wale'. Ni dhaahiri kuwa hali zao ni mbaya, wameelemewa na karibia pumzi zinakata. UMEWASHIKA PABAYA, USIWALEGEZEE. Mwenyezi Mungu akulinde na Shari zao.
 
Tume kuweni makini na kusoma mazingira ya kampeni na lugha. Ni wazi Sasa tume bila kumung'anya wanaonyesha dalili za kumuonea Lissu. Polisi kwa upande mwingine nao wanajitahidi kuweka mikono yao kuwa Wana lao Jambo.

Kwa mtu makini anayemfuatilia Lissu japo vyombo karibu zote zinaminya taarifa ya Nini ameongea, Lissu Yuko juu ya wastani kugusa kero za wananchi. Wapiga kura wengi wanahitaji hiki anachokiongea Lissu. Wanamtaka kiongozi jasiri atakayesimamia haki zao na siyo chama Kama ilivyo kwa Magufuli.

Tofauti Ni ndogo Sana, Magufuli yeye anataka wachague chama ili wapewe maendeleo la sivyo hawatapewa ambayo kwa wengi wanaona ni kama ubaguzi na vitisho.

Lissu amejikita kwenye Uhuru, haki na maendeleo akisisitiza kuwa yeye atasimamia maamuzi ya wengi na kamwe hatoyaingilia. CCM hata wakipewa wabunge, hawatakuwa na meno Kama ambavyo tuliona bunge lililopita kwa kumnanga kwa kebehi CAG kisa ametoa Ukweli wake kuwa bunge Ni dhaifu.

Kuna mifano mingi kuhusu bunge lililopita ambayo iliongozwa sehemu kubwa kwa kuwa na wabunge wa CCM . Mizaha ya hapa na pale zilitawala na hii ndiyo maana Lissu anapata credit kubwa kwenye kampeni zinazoendelea. Maamuzi mengi yalikiuka misingi ya haki za binadamu na waliruhusu bunge kuingiliwa na mamlaka ya rais kutumia hela bila kupitia maamuzi yao.

Wananchi muda huu watakuwa na muda kupitia hotuba nyingi za Lissu na kuona Ukweli ulipo na kufanya maamuzi. Lissu atakaporudi Ni wazi atavuruga hasa uwanja wa kampeni. Kwanza atapata muda mpana kupitia hotuba za Magufuli na kufanya analyst. Kwa werevu wake atamvunjavunja Magufuli kwa pointi na hapa ndipo atawabadili watu wengi. Kuna zile kura za wale wasiokuwa na upande, watu wanaosubiri kuona mabaliko either kisera au tukio la namna yoyote.

Kwa Sasa tukio limetoka, polisi wanamuandama Lissu, tume wanamuandama Lissu na vyombo vya habari vimeegemea upande ule. Jukwaa la CCM limeshona watoto na mbaya zaidi watoto wetu wanalazimishiwa kupumzika ilimradi jukwaa lishone watu wa kushiba. Wasanii nchi nzima wamejazwa na kutoa lugha za kebehi. Wananchi watapima na kutoa maamuzi juu ya huku ambako hakuna wasanii wakubwa na magari ya kusomba watu dhidi ya kwenye jukwaa la fiesta.

Uchaguzi mwema na kwa hakika tume inaliingiza kupata doa kimataifa. Tume isidhani wanaendesha uchaguzi wa serikali za mitaa. Tujiulize tu, hivi Ni mahala gani hakuna kiongozi wa CCM ? Viongozi wote nchi nzima wenyeviti wa vijiji na mitaa Ni CCM .

Je, Kuna maendeleo kiasi gani? Kipimo hicho ndicho kinamuangusha Magufuli kuonekana Hana ajenda ya kutetea ilani yake. Lissu 60% imesimama wima ya ushindi
 
IMG-20201002-WA0117.jpg
 
Ni ukweli uliowazi kuwa kutokana na vyombo vingi vya Habari kutokua huru kuonyesha mikutano ya Lissu ya kampeni Wananchi wengi mitandao imekua Njia ya kupata hbr ya Sera za Upinzani. Hivyo hamasa ya Lissu kuwa nje ya Kampeni itafanya biashara ya vifurushi kushuka. Nashauri kwa kuwa serikali itakosa kodi na kwa kuwa pia anaonekana Hana kosa alilovunja, basi wamuache tu Mheshimiwa Lissu aendelee na kampeni kwa kuwa hata serikali yenyewe itkusanya kodi. TANZANIA NI YETU SOTE TUIJENGE KWA PAMOJA!mwachieni MH.Lissu aendelee na kampeni ili pia nchi ipate kodi...!!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Sisi makamanda tutaandamana kumshawishi lissu aendelee na kampeni [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Tundu Lissu ni Makamu Mwenyekiti Taifa wa CDM. Ijapokuwa uamuzi wa kamati ya maadili una kila viashiria vya kuwa "impartial, bogus and unacceptable" bado ana uwezo wa kutumia nafasi hii kuwanadi wabunge na madiwani wa chama chake.
 
Ni ukweli uliowazi kuwa kutokana na vyombo vingi vya Habari kutokua huru kuonyesha mikutano ya Lissu ya kampeni Wananchi wengi mitandao imekua Njia ya kupata hbr ya Sera za Upinzani. Hivyo hamasa ya Lissu kuwa nje ya Kampeni itafanya biashara ya vifurushi kushuka. Nashauri kwa kuwa serikali itakosa kodi na kwa kuwa pia anaonekana Hana kosa alilovunja, basi wamuache tu Mheshimiwa Lissu aendelee na kampeni kwa kuwa hata serikali yenyewe itkusanya kodi. TANZANIA NI YETU SOTE TUIJENGE KWA PAMOJA!mwachieni MH.Lissu aendelee na kampeni ili pia nchi ipate kodi...!!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Kabla ya uchaguzi pato lililotokana na mauzo ya bundle lilikuwaje?
Kuna wapenzi wa filamu, wengine mipira nk.
Wengine muziki. Kwa hiyo mauzo hayataathirika.
 
lissu alishaibadilisha nchi, tukaanza kujadili mambo ya msingi ikiwemo haki, sheria, maendeleo halisi na mambo mengi positive, sasa hawa jamaa wa kijani wanataka waturudishe kwenye discusion Za kina dai na kiba na konde boy, au zile za connection zisizo na tija.

inasikitisha msema kweli anapoonekana adui.

umbumbumbu umeendelea kuwa mtaji wa chama jike
Ni ukweli uliowazi kuwa kutokana na vyombo vingi vya Habari kutokua huru kuonyesha mikutano ya Lissu ya kampeni Wananchi wengi mitandao imekua Njia ya kupata hbr ya Sera za Upinzani. Hivyo hamasa ya Lissu kuwa nje ya Kampeni itafanya biashara ya vifurushi kushuka. Nashauri kwa kuwa serikali itakosa kodi na kwa kuwa pia anaonekana Hana kosa alilovunja, basi wamuache tu Mheshimiwa Lissu aendelee na kampeni kwa kuwa hata serikali yenyewe itkusanya kodi. TANZANIA NI YETU SOTE TUIJENGE KWA PAMOJA!mwachieni MH.Lissu aendelee na kampeni ili pia nchi ipate kodi...!!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Ikitokea mheshimiwa lissu kuendelea kunadi hata wagombea ubunge na udiwani, kitakachofuata ni kwamba NEC watamuondoa kwenye orodha ya wagombea urais Mheshimiwa Lissu, na wakishamuondoa, kwa hasira Chadema kitaazimia kususia uchaguzi, kikisusia, lengo la watu Fulani litakua limetimia Kama serikali za mitaa.

Ndicho kinacholengwa. Kama hamuamini subirini au itatafutwa sababu nyingine ya kumuengua kwenye wagombea upresidar.

Haya ni mawazo yangu tu.
 
Back
Top Bottom