Tume kuweni makini na kusoma mazingira ya kampeni na lugha. Ni wazi Sasa tume bila kumung'anya wanaonyesha dalili za kumuonea Lissu. Polisi kwa upande mwingine nao wanajitahidi kuweka mikono yao kuwa Wana lao Jambo.
Kwa mtu makini anayemfuatilia Lissu japo vyombo karibu zote zinaminya taarifa ya Nini ameongea, Lissu Yuko juu ya wastani kugusa kero za wananchi. Wapiga kura wengi wanahitaji hiki anachokiongea Lissu. Wanamtaka kiongozi jasiri atakayesimamia haki zao na siyo chama Kama ilivyo kwa Magufuli.
Tofauti Ni ndogo Sana, Magufuli yeye anataka wachague chama ili wapewe maendeleo la sivyo hawatapewa ambayo kwa wengi wanaona ni kama ubaguzi na vitisho.
Lissu amejikita kwenye Uhuru, haki na maendeleo akisisitiza kuwa yeye atasimamia maamuzi ya wengi na kamwe hatoyaingilia. CCM hata wakipewa wabunge, hawatakuwa na meno Kama ambavyo tuliona bunge lililopita kwa kumnanga kwa kebehi CAG kisa ametoa Ukweli wake kuwa bunge Ni dhaifu.
Kuna mifano mingi kuhusu bunge lililopita ambayo iliongozwa sehemu kubwa kwa kuwa na wabunge wa CCM . Mizaha ya hapa na pale zilitawala na hii ndiyo maana Lissu anapata credit kubwa kwenye kampeni zinazoendelea. Maamuzi mengi yalikiuka misingi ya haki za binadamu na waliruhusu bunge kuingiliwa na mamlaka ya rais kutumia hela bila kupitia maamuzi yao.
Wananchi muda huu watakuwa na muda kupitia hotuba nyingi za Lissu na kuona Ukweli ulipo na kufanya maamuzi. Lissu atakaporudi Ni wazi atavuruga hasa uwanja wa kampeni. Kwanza atapata muda mpana kupitia hotuba za Magufuli na kufanya analyst. Kwa werevu wake atamvunjavunja Magufuli kwa pointi na hapa ndipo atawabadili watu wengi. Kuna zile kura za wale wasiokuwa na upande, watu wanaosubiri kuona mabaliko either kisera au tukio la namna yoyote.
Kwa Sasa tukio limetoka, polisi wanamuandama Lissu, tume wanamuandama Lissu na vyombo vya habari vimeegemea upande ule. Jukwaa la CCM limeshona watoto na mbaya zaidi watoto wetu wanalazimishiwa kupumzika ilimradi jukwaa lishone watu wa kushiba. Wasanii nchi nzima wamejazwa na kutoa lugha za kebehi. Wananchi watapima na kutoa maamuzi juu ya huku ambako hakuna wasanii wakubwa na magari ya kusomba watu dhidi ya kwenye jukwaa la fiesta.
Uchaguzi mwema na kwa hakika tume inaliingiza kupata doa kimataifa. Tume isidhani wanaendesha uchaguzi wa serikali za mitaa. Tujiulize tu, hivi Ni mahala gani hakuna kiongozi wa CCM ? Viongozi wote nchi nzima wenyeviti wa vijiji na mitaa Ni CCM .
Je, Kuna maendeleo kiasi gani? Kipimo hicho ndicho kinamuangusha Magufuli kuonekana Hana ajenda ya kutetea ilani yake. Lissu 60% imesimama wima ya ushindi