Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ipo nusu kaputi, Mbowe hataki kupambana na Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

sonofobia

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
1,171
Reaction score
4,295
MAHOJIANO YA LISSU NA VOICE OF AMERICA (VOA)

VOA: Nini kimetokea na uongozi wa sasa?

Lissu: Umekuwa madarakani kwa miaka 20 na muafaka tunatakiwa kufanya mabadiliko ya lazima ili tuweze kupeleka chama mbele.

VOA: Plani yako nini kama ukiwa M’kti, unapeleka chama vipi?

Lissu: Hapa tulipo, tupo kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa. Mabadiliko ambayo tumezungumza kwenye maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan kwa takribani miaka miwili, hakuna matunda yoyote. Njia ya kutoka hapa ni uongozi Mpya uje na uonyeshe na ukipeleke chama kwenye muelekeo tofauti. Kama maridhiano hayajafanya kazi, tuna nini mbadala?

Tunatakiwa tufanye mass mobilization (Nguvu Ya Umma) ili kukiongoza chama kwenye kuliamsha Taifa na kuunganisha nguvu na asasi za kiraia, vyama vya siasa, ili tuweze kuleta mabadiliko makubwa ya kidemokrasia ili tuweze kulazimisha mabadiliko.

VOA: Kwa hiyo, Tunaweza kusema kuna tofauti kati yako na M’kiti (Mbowe) Juu ya namna ya kukipeleka chama mbele?

Lissu: You are right on the money (Umepiga sehemu sahihi kabisa). Nadhani tuna tofauti ya kimsingi kabisa namna ya kukipeleka Chama mbele

VOA: Kumekuwa na mengi yanaendelea Kati ya serikali na chama chako, kuna wanachama wenu wamekuwa wanatekwa na hatujaona hatua kubwa kutoka kwenye chama chako

Lissu: Hiyo ndio hoja ya msingi kabisa. Hoja ni kuwa chama kinaonekana kime-paralyze (kipo nusu kaputi) kwa sababu M’kiti wa sasa haonekani kutaka kupambana na Samia.

M’kti Hataki kubomoa daraja na uongozi wa Samia. Viongozi wetu na wanaharakati wametekwa na wengine kuuwawa kwa namna za kikatili. Wanachama wetu, viongozi wetu wa Wilaya nao wametekwa na kupotezwa.

Yote haya yanatokeo ni wazi tumerudi kwenye zama za Giza za Magufuli. Na uongozi wa chama unaonekana kutokujua namna ya kutoka kwenye mkwamo huu. Kwa hiyo, nina gombea kwa sababu tunatakiwa kutoka kwenye huu mkwamo

VOA: Umesema No Reforms, No Election. Unaweza elezea hili?

Lissu: Tumekuwa na uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa kama wiki mbili au tatu zilizo pita. Ilikuwa ni MAJANGA! (total disaster!). Ulikuwa ni uchaguzi mbaya kuliko wa 2020 kwa minajili ya manipulation ya uchaguzi kwa kiwango cha kitaifa. Kama hili litakuwa kawaida kwenye chaguzi zetu, ni wazi kwetu kuwa hawapo (CCM) tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani. Kwa hiyo, kama hawapo tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani, kwa nini tushiriki chaguzi zijazo?

Kwa hiyo, tumeamua (CHADEMA) ili turudi kwenye uchaguzi, lazima tulazimishe mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

Kwa hiyo, msimamo wetu ni: tupiganie mabadiliko, tukisha pata mabadiliko, tutakuwa tayari kushirki chaguzi. Tunasimama kwenye No reforms, No Election.

VOA: Pia, Unataka mabadiliko ndani ya CHADEMA pamoja na ukomo wa uongozi?

Lissu: Kabisa, Hatuwezi kupambana na udicteta wa Samia kama sisi ndani tupo tulivyo sasa. Kwa hiyo, lazima tusafishe nyumba yetu kwanza.

Lazima tusafishe matendo yetu kabla hatuja pambana na uongozi wa Samia. Kama hatuta jisafisha, itakatisha tamaa watu wetu na tutashindwa kupambana na tatizo kubwa ambalo limekuwa linatuathili la utawala wa Samia Suluhu Hassan

VOA: Mr. Lissu, thank you very much!

TunduALissu: Thank you for having me on your program.
 
Hajamuuliza kuhusu Msigwa kumuendesha Lissu kama drone?
 
Lissu na machine kubwa ,angekuwa ni mwanachama mwingine nadhani Mzee Mbowe angekuwa ameshachuka hatua za kumfukuza kwenye hii kampuni yake.Hakika mzee Mbowe kayakanyaga,
Kweli maana MSIGWA anamzungurusha Lissu kila pembe kama drone
 
Back
Top Bottom