Lissu haelewi maana ya ‘Jeshi la Akiba’?

Acha upotashaji wewe, hii haiko kwenye matakwa ya kisheria ya hiyo ajira ya JWTZ. Lakini kwa migambo na JKT wakati wa vita wanaweza kupekekwa mstari wa mbele kama chambo, kusaidia logistics zingine za kivita nk.
Kwahiyo sasa hivi tuko kwenye vita hao migambo wa kuchonga mmewatanguliza kama chambo ?
 
UMETOA DOZI KUBWA KWA MWANAFUNZI WA CHEKECHEA LABDA MWONGEZEE KWAMBA MKUU WA JESHI LA AKIBA ANA CHEO CHA MAJOR GENERAL KUTOKA JWTZ LABDA YEYE NA WAPAMBE WAKE WATAELEWA
Jeshi la akiba linatoa wapi mamlaka ya kulinda mikutano ya kisiasa ?
 
Tunahoji uhalali wao kisheria ni sheria ipi imeunda hilo jeshi la akiba ?

Je lini mikutano ya kisiasa imeanza kulindwa sungusungu ?
Ujuaji mwingi utawaponza ukihoji uhalali wa wanamgambo maana yake unahoji uhalali wa Jeshi la wananchi wa Tanzania kwakuwa mgambo ni sehemu ya jeshi hilo. Kwa taarifa yako na wenzako kila mtanzania ni mlinzi wa nchi yake popote alipo, mikutano ya siasa ni sehemu ya shughuli za watanzania na wanahitaji ulinzi bila kujali anayelinda ni nani ili mradi anayelinda hajavunja sheria ya ulinzi na usalama.
 
Soma michango hapa, yuko mchangiaji kesha weka screen short yake kutoka kwenye katiba ya lugha ya Kisukuma. Kama wewe ni Msukuma ama ulishawahi kuishi Usukumani.
Mkuu tupe kifungu cha sheria kinachounda hili jeshi haramu la kuchonga.
 
Mkuu kwani tuko vitani kiasi cha jeshi la akiba kuwa sanctioned??

Unajua sheria ya uchaguzi inasemaje kuhusu ulinzi kwenye mikutano ya kisiasa ?
 
Jeshini kuna Active Force Na Reserve force Na maana Ya Reserve Force ni Jeshi la Akiba ambalo hapo nyuma liliitwa Mgambo ila kwa sasa ni Jeshi la akiba Na lina MKUU wao kabisa so hapo Lissu kajichanganya sana
Sasa si wangevaa kimgambo ili waeleweke?,,hivi viswahili vya jeshi la akiba havijaxoeleja
 
Unajua sheria ya uchaguzi inasemaje juu ya ulinzi kwenye mikutano ya kisiasa ?

Unajua mipaka ya jeshi la wananchi na reserves zake pamoja na majukumu ya jeshi la polisi ??
 
Jeshi la akiba linatoa wapi mamlaka ya kulinda mikutano ya kisiasa ?
Pole sana Jeshi la akiba kwa maana ya wanamgambo wakati wa amani hufanya kazi kama polisi wasaidizi na wanawajibika polisi mojakwa moja na kwa maana hiyo hawana mpaka wa ulinzi kwamba walinde eneo fulani tu eneo jingine wasifike hakuna kitu kama hicho , na ukileta za kuleta utankong'ontwa kama wahalifu wengine tena usiombe kukamatwa na mgambo ni kama umekamatwa na mwalimu wa wanamgambo JW wao wanajua kupiga tu na siyo hizo brabra zenu za vifungu vya sheria mara mia ukamatwe na polisi kuliko mgambo rejea Dar alivyowatumia Hon. Makonda nini kilitokea? Waheshimu sana watu hawa wanapokuwa kazini waliowafundisha hawapendi kudhalilika.
 
Mkuu nijibu kwanza tuko vitani mpaka tuite jeshi letu hilo mnalosema la akiba ???
WAKATI WA AMANI WANAMGAMBO HUTUMIKA KAMA POLICE AUXILIARY rejea usimamizi wa mitihani, Mwenge, ugeni wa viongozi kitaifa huwa wanatumika hivyo nakushangaa unapouliza swali la kitoto kama hilo labda wewe siyo mtanzania kwa mtanzania hashangazwi na askari wa jeshi la akiba popote atakapowakuta na ndiyo wanatumika kila mahali ikiwemo kulinda migodi kwa asilimia kubwa migodi inalindwa na wanamgambo na ukileta fyoko utadhibitiwa kwa nguvu zote , polisi wakichelewa hawakukuti bali watakuta historia yako tu . HIVYO WAHESHIMU SANA WANAMGAMBO UPATE KUISHI KWA AMANI POPOTE ULIPO.
 
Si Tundu mwenyewe mtupu hata wanaoamini anajua kila kitu
 
Tanzania jeshi ni moja tu, nalo ni Jeshi la Wananchi la Tanzania. Polisi, Uhamiaji, JKT, Mgambo hayo yanatambulika kama majeshi ya akiba. Hii ina maana kuwa, siku likitokea la kutokea na nchi ikaingia vitani basi majeshi hayo ya akiba yanaungana na JWTZ kuongeza nguvu. Ndio maana mkuu wa JWTZ anaitwa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama, hayo majeshi ya Akiba yapo chini yake. Sare za Polisi, JKT, Uhamiaji na Mgambo tunazijua. Sasa hao vijana wa Tshirt Nyekundu wametoka wapi? Hata angekuwa nani angestuka.
 
Kwenye hiyo sheria uliyoambatanisha hapo kwenye kifungu cha 19 (1) kinasema when Tanzania is at war... ndio bla blah zingine za reserve force zinaendelea.

Japo hiyo sheria haijafafanua jeshi la akiba ni kitu gani. Kwa nilivyo elewa mimi reserve force itatumika wakati wa vita tu.
Swali langu ni je uchaguzi ni vita?
 
Safi mkuu, nadhani hapa ndipo wengi wanashindwa kuelewa na ndiyo maana hakuna anayejibu swali la Lissu kuwa hili jeshi la akiba limeanzishwa kwa mujibu wa sheria ipi ndani ya katiba?

Na swali la kuongezea, Je nani kalipa mamlaka ya kusimamia shughuli za kampeni/uchaguzi?
 
Hatuna jeshi la anga, hatuna jeshi la nchi kavu,hatuna jeshi la maji, tuna VIKOSI!
Acha kupotosha
 
Unajua hitaji la sheria ya uchaguzi kuhusu ulinzi wa mikutano ya kisiasa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…