Naona wewe ni mzito kidogo wa kuelewa. Swali hapa ni kama alipewa ushindi kama anavyodai Lissu. Kupewa kuna maanisha alipendelewa na hakushinda uchaguzi. Aidha, kuwa alifanyiwa fadhila na CCM. Na kama alifanyiwa fadhila basi ana deni na aliyemfadhili. Ni character assassination ya hali ya juu maana hamna ushahidi uliotolewa zaidi ya kusema hajachangia na hachangii chochote bungeni.
Mimi ninasema ni kuwa Aidan alishinda uchaguzi wake kama walivyoshinda wenzake wengi. Tofauti yake ni kuwa alitangazwa mshindi ambayo ni haki yake wala sio fadhila. Sababu za yeye kutofanyiwa hujma zinaweza kuwa nyingi ( msimamizi wake wa uchaguzi hakupokea memo ya kumpora ushindi au alipokea akaidharau, CCM hawakutaka mpinzani wake ashinde, yeye na watu wa jimbo lake walipambana ili haki ifanyiken.k.) lakini ukweli unabaki kuwa alishinda. Kusema tofauti na hilo ni kumuonea.
Amandla...