Juzi ulivyokuwa mwanza uliongelea kuhusu wakulima wa pamba kukopwa Pamba yao na wanunuzi binafsi wa Pamba. Naona mkuu haukuwepo nchini muda mrefu. Naomba nikusaidie.
1. Msimu wa pamba 2019/2020 hakuna mfanyabiashara aliyenunua Pamba moja kwa moja kwa mkulima, pamba ilinunuliwa na halmashauri za vijiji na hao wamiliki wa vinu vya pamba walienda kununua Pamba kwenye halmashauri za vijiji kwa kulipa taslimu hakuna pamba iliyokopwa na mnunuzi binafsi.
Tatizo lilikuwepo halmashauri ya Bunda ambapo halmashauri nyingi za vijiji ni za chadema na hao viongozi walivyopelekewa fedha badala ya kuwalipa wakulima walizitumia kwa shughuli zingine na kuwakopa wakulima pamba yao kwa kuwadanganya fedha hazijaja.
Serikali ilivyowafuatilia walianza kudai serikali inawafuatilia kwa kuwa wao ni wapinzani, nashukuru takukuru waliingilia kati na walirejesha fedha hili Wenje analijua Ester Bulaya analijua sijui kwanini waliamua kumpotosha muheshimiwa Lissu.
2. Kufujwa kwa mali za NCU, hili JPM kalivalia njuga za kutosha na mali zote za NCU zimerudishwa mikononi mwa ushirika na wapo wafanyabiashara wabishi ambao walidiriki hata kuwapiga risasi maafisa wa serikali waliokuwa wanafuatilia urejeshwaji wa mali za NCU, hivyo anavyosema mali za NCU zimefujwa hapana ziko salama na uongozi wa NCU uko imara.
3. Madai ya Lissu kuwa Pamba inanunuliwa na wana CCM, ni madai ya kijinga tu mnunuzi ambaye ni mwana ccm ni Gachuma naye ana hisa kidogo sana kupitia Bulamba Gingery, hisa nyingi ni za Sumaria Group. Wanunuzi wakubwa wa Pamba ni Bilchard na Gupta group hawana uhusiano wowote na CCM niwafanya biashara huru tu.
Naomba mumwambie Lissu asifikiri yuko Bungeni hivyo anaweza wajibika kisheria kwa uongo wake anaotapanya.