Lissu hofu yako ya fedha chafu ndani ya Chadema inatoka wapi?

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Nimemsikikiza vizuri sana makamu mwenyekiti wa Chadema kwa makini sana kupitia kituo komoja cha habari jana.

Anasema anahofu kuwa fedha haramu zinaweza kuingizwa ndani ya Chadema.

Lissu ni makamu mwenyekiti wa Chadema ambaye yupo ktk top 3 ya viongozi wakuu wa chama.

Inakuwaje awe na mashaka wakati na yeye ni mmoja wa waongoza chama?

Binafsi naanza kuwa na mashaka sana na uwepo wake ndani ya cdm na hizi comedy zinazoendelea Kati yake na Msigwa.

Ukweli huwa ni mchungu sana lkn Wana cdm wenzangu huyu Lissu ni suala la muda tu tutasikia amehamia CCM au ameanzisha chama chake.

Tuombe uzima ili tuyashuhudie yajayo.

 
Nafikiri hayo mashaka yako juu uwepo wa Lissu Chadema na hisia kuwa anaweza kusajili chama chake ameyatolea maelezo ya kutosha kabisa.Lissu yupo sana Chadema na uwezekano wa yeye kwenda CCM hilo ni jambo gumu kwake.Lissu ndiye mgombea wa Chadema nafasi ya Urais 2025 na ni Makamu Mwenyekiti Taifa ajaye.
 
Mtajijua wenyewe huko!
 
Ni vizuri kuwa na mashaka. Na yeye alifafanua kuwa wakitaka fedha za kufanya mikutano na mambo mengine ndani ya chama majibu huwa ni kwamba fedha hakuna ila alishangaa wakati wa uchaguzi fedha zilikuwepo kila kona.
 

Anachokisema Tundu Lisu huku ukizingatia yuko nafasi 3 za juu, huo ni ushahidi kuwa mwenyekiti wa cdm ni tatizo. Ni muda sahihi wa mwenyekiti wa cdm kukaa pembeni na kuruhusu uongozi mwingine. Inaelekea kwenye vikao vya ndani mwenyekiti amegoma kutii mabadaliko huku akilazimisha business as usual. Mbowe atambue wakati ukuta.
 
Mwenyekiti tena? Anazungumzia pesa chafu na sio Mwenyekiti, tubakie kwenye mada kuu!
 
CCM wanataka kuonesha Lissu yupo kinyume na Mbowe ama Mbowe yupo kinyume Cha Lissu.

Kama wao wanampenda Lissu basi wahakikishe wanawataja waliotaka kumuua...

Wasiishie tu kumwita Simba..😛😛😜😄😆😃
 
chama kina madeni makubwa kupindukia, na mkopeshaji mkuu ni muandamizi chamani, na chama kinaendeshwa kwa mkopo, kwahivyo ni Lazima awe na hofu 🐒
 
Umesahau zile bilioni 3 karibu na uchaguzi na zilizozuiwa na UTAWALA wa awamu ya 5?!!

Zikielekezwa kwa NGO's sijui ya yule ndugu wa kutoka huko Ngororongo na Serengeti ?!![emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787]

Alaa ya ukiona panafuka moshi....
 
chama kina madeni makubwa kupindukia, na mkopeshaji mkuu ni muandamizi chamani, na chama kinaendeshwa kwa mkopo, kwahivyo ni Lazima awe na hofu [emoji205]
Kumbe...

Mkuu unasema hiki chama kinaendeshwa kwa madeni...ni vipi kuhusu mgawanyo wao wa ruzuku ?!!!
 
Kumbe...

Mkuu unasema hiki chama kinaendeshwa kwa madeni...ni vipi kuhusu mgawanyo wao wa ruzuku ?!!!
ruzuku inaenda moja kwa moja kwenye akaunti ya mkopeshaji ingawa hata robo ya marejesho ya kila wakati haifikii 🐒

hali ni mbaya sana
 
Akili imeanza kurudi!
 
Nakubaliana na mawazo yako mkuu kumbuka hata mimi kama mwana chadema tena hai ninapata mashaka makubwa mzee
 
Kwani CHADEMA kinaongozwa na Malaika walioridhika na maisha yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…