Pre GE2025 Lissu jitokeze ukanushe habari za Msigwa kugharamia Press ya kutangaza nia, vinginevyo umekwisha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa kusoma trend ,nashawishika kuamnini ameratibiwa kuandaa press na mtu au watu wa upande ule
 
Chadema mnaparuana tu na kutoa mimavi

USSR
 
Sasa Kama sio mjinga mbona unacheza mziki wa CCM

CCM wameleta iyo propaganda ili kudhoofisha harakati hata mtu ambaye Hana D mbili lazima ataelewa tu

Ndio maana nimekushangaa kuunganisha tukio la Dr Slaa na Lissu aisee umenishangaza Sana Chakaza

Kumbuka CCM wapo kazini kueneza propaganda na lazima watamtumia tu mtu wao Msigwa

Kama Lissu angelikuwa anataka pesa ya ccm kwani lazima apitie kwa Msigwa?

Si anaenda tu kwa Samia anamwambia nipe pesa nikutetee!!
 
Well said, Msigwa anaweza kuwa kachomekea hili kwa faida zake kisiasa na kumkera Mbowe. Lakini ni baya kwa sisi tunaotaka mabadiliko ya kikatiba yaende vizuri kwani naamini zaidi ya nusu ya wapiga kura wako neutral hivyo wanasubiri sera zitakazo mwagwa sasa uzushi kama huu kuwa Msigwa kamsaidia kufanya lolote ndani ya chama utaharibu image yake kwa wale wasio na access na ukweli.
Kuna watu wanashindwa uchaguzi kwa sababu tuu uongo dhidi yao haukukanushwa.
 
Hakuna kitu Kama icho huo ni uzushi
 
Lissu amewashika pabaya? atakanusha vingapi?
Yaaani mkiguswa tu uenyekiti mnapaniki, Ayatolla safari hii anang'ooka.
 
Mkuu kila siku Mbowe tunaambiwa kalamba asali, lakini hukuwahi kumtaka ajitokeze kujibu hizo tuhuma. Hivyo ni vyema kutotaka kwa Lisu kujibu kila uzushi utakaoletwa kwenye mitandao.
 
jambo la kwanza,
hoja za msigwa dhidi ya Chadema ni za msingi sana, chama kinapaswa kumjibu.

jambo la pili,
Msigwa akabiliwe kisiasa. Full stop.

jambo la mwisho ila sio kwa umuhimu, siasa ni sayansi ya mipango na sio makelele na mdomo

msigwa ni mtengeneza mapito tu ya ukombozi 🐒
 
Hoja hapa Lissu ajibu pesa za press kazipata wapi?? kama kachamgiwa na wanachama aonyeshe uthibitisho maana yeye ni mwanasheria, tunaanzia hapo kwanza.
 
Kajinga kalikoandika hii post.
Better tundu Lisu kuliko Mbowe,
Kwa akili safi kikanuni, Kisheria na maadili, Tundu lisu angekuwa Mwenyekiti wa chama enzi za 2015, Marehemu Lowassa asingepeperusha bendera ya chama aishie kukifukia kabisa,
Badala yake Dr. Slaa angekipeperusha kikakae mawinguni.
Tundu Lissu ni wazi ndio mwenyekiti ajaye.
 
Kwa kweli CHADEMA tuachane na siasa chafu, Tusifanye kugombea uenyekiti ni jambo kubwa sana kiasi kwamba tuanze kuokoteza maneno ya kumchafua mtu. Msigwa ana pesa gani ya kuandaa ukumbi kwa ajili ya Lissu?.
 
Hoja hapa Lissu ajibu pesa za press kazipata wapi?? kama kachamgiwa na wanachama aonyeshe uthibitisho maana yeye ni mwanasheria, tunaanzia hapo kwanza.
Masuala ya pesa za chadema anaehusika ni mtu moja tu.

Masuala mengini binafsi, kwa mfano hili la press conference ya lisu ya kutangaza azma yake ya kugombea uenyekiti wa chadema Taifa,

aliulizwa swali na muandishi wa habari juu ya wapi amapata fedha ya kuwaita wanachana wengi namna ile waliohudhuria ile ile press conference na pia alipata wapi fedha za kuwalipa media houses.

And,
the gentleman was very clear, kwamba waliohudhuria ile press conference, marafiki zake na wadau wengine wa siasa huenda ni pamoja na huyo msigwa ndiyo waliofikisha jambo hilo.

Ubaya ubwela uko wapi hapo gentleman, makosa yake ni nini ikiwa hata gari ya zaidi ya milioni mia moja alichangiwa na wadau na marafiki zake wa kisiasa, wa nje na ndani ya chadema?

hata CCM walimchangia, ile haikua mbaya, hii ndiyo mbaya? au gubu tu gentleman?🐒
 
Hoja hapa Lissu ajibu pesa za press kazipata wapi?? kama kachamgiwa na wanachama aonyeshe uthibitisho maana yeye ni mwanasheria, tunaanzia hapo kwanza.

Acheni kimdhalirisha Lissu kana kwamba hawezi kuwa na pesa ya kulipia ukumbi. Akianza kampeni ya kutembelea mikoano mtaanza kuulizia ametoa wapi pesa za nauli.
 
Hakuna kitu Kama icho huo ni uzushi
Mkuu sijui mimi na wewe tunatofautiana wapi! Hata mie nasema ni uzushi na sio wa kuuacha usambae kisha uwe na nguvu ya kumkosesha Lissu uungwaji mkono.
Tafadhali sana sikilizeni mahojiano haya ya Yerricko Nyerere na Radio moja mtajua kwa nini nina hofu na kuacha hili kujibiwa! Kumbuka huyo ni mjumbe wa mkutano mkuu, jee wajumbe wangapi watakuwa wanaamini hivyo?
Sikiliza mpaka mwisho uelewe hofu yangu please!
 

Attachments

  • All_Video_Downloader_yerickonyerere_AQNU_GZUqGScsIzDt04FH_R4_UnRQqLDD2HpJ0Fk1hUkMVm-qqdz8eCujt...mp4
    27.2 MB
Lissu kalipiwa kwa michango ya watu mbalimbali. Unajua kitu kinachoitwa Sauti ya watanzania? Nenda ClubHouse kama una simu. Fedha zote zilichangwa pale.
 

Yaani kutangaza nia nako mpaka walipie. Msigwa kawa Don siku hizi kumbe.
 
Sielewi kwanini watu wanamsakama Lissu, kwani katiba ya CHADEMA hairuhusu mtu kugombea uenyekiti? Kwanini kila mtu mwenye jina akijitokeza kugombea uenyekiti CHADEMA inaonekana ni kosa? Ilikuwa hivi hivi kwa Marehemu Chacha Wangwe, ikaja kwa Zitto na sasa Lissu anakuwa mbaya. Hiki chama kipo serious kweli kinataka kuongoza watanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…