Pre GE2025 Lissu jitokeze ukanushe habari za Msigwa kugharamia Press ya kutangaza nia, vinginevyo umekwisha

Pre GE2025 Lissu jitokeze ukanushe habari za Msigwa kugharamia Press ya kutangaza nia, vinginevyo umekwisha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mimi ni mmoja wa watu tusio amini kwenye uzushi wa mitandaoni. Lakini kwa hili nililosikia naona linahitaji ulitolee ufafanuzi wewe mwenyewe maana linaenda kukupoteza mazima katika siasa hadi ubaki nawe unatembezwa mitaani ukiwa unabeba picha za mwenyekiti wa CCM kama huyo Msigwa.

Je, ni kweli uliandaliwa ukumbi wa Mlimani city na Peter Msigwa na kulipiwa gharama zote?

Bado hatujasahau Dr Slaa alivyolipiwa gharama za hotel kufanya press yake na dola au Lipumba alivyo gharamiwa kuvuruga CUF kisha kupelekwa Rwanda kula Bata.

Hao wote mwisho wa heshima zao tumeuona ni back to Sq zero.

Nakuamini sana mimi na wanachadema wenzangu, lakini maneno haya yajibiwe yasije kupoteza imani yetu kwako.

Unao uhuru wa kufanya lolote kisiasa, lakini huna uhuru wa kutulazimisha kukuunga mkono chochote utakacho kufanya.

PEOPLES POWER!
Lissu kanyaga twende, hizi kelele za chawa wa Mbowe achana nazo
 
Back
Top Bottom