Pre GE2025 Lissu jitokeze ukanushe habari za Msigwa kugharamia Press ya kutangaza nia, vinginevyo umekwisha

Pre GE2025 Lissu jitokeze ukanushe habari za Msigwa kugharamia Press ya kutangaza nia, vinginevyo umekwisha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
tanzania-election-017.jpg
 
Wewe ni mjinga kumbe? Unawezaje kuniita mpumbavu au chawa wa Mbowe?
Kwa taarifa yako mtu mjinga ni kuwa mimi ni mtu ninaye Unga mkono mabadiliko ndani ya uongozi kidemokrasia hasa wakati huu.
Na sababu ya kumtaka ajibu uzushi huo ni kuwa sitaki Lissu wampoteze kwa sababu ya kufikiriwa kuwa ana uhusiano na Msigwa aliyekitukana Chama na akanyimwa kura pasipo ukweli wowote!
Sasa uchawa kwa Mbowe uko wapi hapo? Na pia Mbowe simpingi kwani kwa sasa ni mwenyekiti aliyechaguliwa na wana chadema hadi uchaguzi mwingine
Atajitokeza mara ngapi kwa kila uzushi jaribu basi kutumia akili hata kisoda
 
Mimi ni mmoja wa watu tusio amini kwenye uzushi wa mitandaoni. Lakini kwa hili nililosikia naona linahitaji ulitolee ufafanuzi wewe mwenyewe maana linaenda kukupoteza mazima katika siasa hadi ubaki nawe unatembezwa mitaani ukiwa unabeba picha za mwenyekiti wa CCM kama huyo Msigwa.

Je, ni kweli uliandaliwa ukumbi wa Mlimani city na Peter Msigwa na kulipiwa gharama zote?

Bado hatujasahau Dr Slaa alivyolipiwa gharama za hotel kufanya press yake na dola au Lipumba alivyo gharamiwa kuvuruga CUF kisha kupelekwa Rwanda kula Bata.

Hao wote mwisho wa heshima zao tumeuona ni back to Sq zero.

Nakuamini sana mimi na wanachadema wenzangu, lakini maneno haya yajibiwe yasije kupoteza imani yetu kwako.

Unao uhuru wa kufanya lolote kisiasa, lakini huna uhuru wa kutulazimisha kukuunga mkono chochote utakacho kufanya.

PEOPLES POWER!

View: https://www.instagram.com/reel/DDjJCL0twP-/?igsh=cXZrNDFldTA2MnRr
 
Kelele za wajinga, wanafiki, waongo zipo nyingi na zipo kila siku. Lisu atawajibu wangapi na mara ngapi?

Anayetoa tuhuma, kama ni za kweli, aweke uthibitisho. Lakini Lisu asipoteze muda wake kujibu kila kelele ya mnafiki, punguani anayefurahisha genge.
Lissu amesema kuwa mojawapo ya dosari kubwa katika CHADEMA ni kutokuwa wazi katika mapato na matumizi yake. Kwa sababu hiyo anapaswa kuweka wazi alichokusanya na nani aliyemchangia na ametumia vipi nchango huo huo. Hivyo hivyo kwenye mchango wa gari lake. Ama sivyo ataonekana kuwa ni wale wale wanaosema hili lakini wanatenda hivi. Kalizua hili mwenyewe na atakiwa kujibu.

Amandla...
 
Kwa kuwa mligharimia haiwezekani Msigwa nae kuchangia? Kama liliwekwa wazi mtandaoni tuwekeeni link ili na sisi tuone. Hii nchi imani kwa mwanasiasa yeyote imepungua sana hivyo mnapaswa ku counter allegations zozote zenye nia ya kumchafua mtu wenu. Mimi nilikataa kabisa kuwa Halima na wenzake wanaweza fanya waliofanya na sasa wako wapi! Sitaki kuamini kuwa Lissu anaweza kuwa kama wao lakini ninahitaji assurance kuwa sivyo. Simuamini Msigwa lakini ukiumwa na nyoka....

Amandla...
Uko sahihi kabisa, nia ya thread ni kutaka hizo allegations zijibiwe na kufutika ili hisia chafu zisiwepo lakini humu ndani kwa vile idadi kubwa wanaendeshwa na mihemko badala ya akili wanadhani ametuhumiwa na mleta mada.
Kwa taarifa ni kuwa hapa anaungwa mkono Lissu kwa hatua yake na kinachofanyika ni kumlinda yeye.
Hoja ya kuwa Msingwa hana hela sio hoja, maana hata kama ametumwa kuratibu tuu ni kosa kubwa la kimkakati kwa timu ya Lissu.
 
Acha hizo

Mchungaji Msigwa ana madeni kibao ambayo analipiwa kidogo kidogo na ASAS Misasa

Kwa Sababu unaishi machame basi unadhani ukumbi wa Mlimani City ni wa gharama sana

Hapo tunafanyiaga sherehe za komunio ya kwanza 😀😀
Umepiga kwenye mshono
 
Uko sahihi kabisa, nia ya thread ni kutaka hizo allegations zijibiwe na kufutika ili hisia chafu zisiwepo lakini humu ndani kwa vile idadi kubwa wanaendeshwa na mihemko badala ya akili wanadhani ametuhumiwa na mleta mada.
Kwa taarifa ni kuwa hapa anaungwa mkono Lissu kwa hatua yake na kinachofanyika ni kumlinda yeye.
Hoja ya kuwa Msingwa hana hela sio hoja, maana hata kama ametumwa kuratibu tuu ni kosa kubwa la kimkakati kwa timu ya Lissu.
Ungekuja na uthibitisho wa miamala inayoonyesha lisu katumiwa fedha na msigwa na baada ya hapo ungetaka lisu ajibu

Huna ushahidi wowote ajibu nini ni kama unarusha jiwe gizani
 
Alichangiwa na Wadau SAUTi ya watanzania na watu wengine Baki ...sio msigwa
 
Mimi ni mmoja wa watu tusio amini kwenye uzushi wa mitandaoni. Lakini kwa hili nililosikia naona linahitaji ulitolee ufafanuzi wewe mwenyewe maana linaenda kukupoteza mazima katika siasa hadi ubaki nawe unatembezwa mitaani ukiwa unabeba picha za mwenyekiti wa CCM kama huyo Msigwa.

Je, ni kweli uliandaliwa ukumbi wa Mlimani city na Peter Msigwa na kulipiwa gharama zote?

Bado hatujasahau Dr Slaa alivyolipiwa gharama za hotel kufanya press yake na dola au Lipumba alivyo gharamiwa kuvuruga CUF kisha kupelekwa Rwanda kula Bata.

Hao wote mwisho wa heshima zao tumeuona ni back to Sq zero.

Nakuamini sana mimi na wanachadema wenzangu, lakini maneno haya yajibiwe yasije kupoteza imani yetu kwako.

Unao uhuru wa kufanya lolote kisiasa, lakini huna uhuru wa kutulazimisha kukuunga mkono chochote utakacho kufanya.

PEOPLES POWER!
Sasa kila lisemwalo ajitokeze kukanusha ataweza kweli????
Ukiwa kiongozi huwezi ukawa unamjibu kila mtu alizike.
Huwezi kunfurahisha kila kiumbe.
#CRITICAL THINKER.
 
Ungekuja na uthibitisho wa miamala inayoonyesha lisu katumiwa fedha na msigwa na baada ya hapo ungetaka lisu ajibu

Huna ushahidi wowote ajibu nini ni kama unarusha jiwe gizani
Samahani nikisema huna akili ingawa ni kweli. Mimi ndiye nimesema? Nimemwambia awajibu wasemao hivyo ili uvumi huo usiendelee unaniuliza mie ushahidi? Usiukubali ukilaza ukakuzoea na kukuganda!
 
Miye nilivyoona Msigwa nikajua Msigwa msemajj wa Serikali kumbe Msigwa Pastor? Mwenyewe huko CCM tegemezi labda kama huyo ndugu yake Msigwa msemajj ndio kapenyeza huo msaada kupitia kwa Pastor
 
Lissu amekuwa mbunge na wakili Tanzania hii miaka kadhaa, hawezi kukosa pesa ya kukodi kijiukumbi mlimani city , Lissu ni wa kimataifa.

Mwambieni mbowe aachie uenyekiti, kila mwanachama wa chadema yuko na haki sawa na uwezo wa kuwa mwenye kiti, hilo la kusema ohh mbowe ndo anafaa sijui akitoka chama kitakuwa vile ni njaa za wapambe wake.

20yrs ni mingi sana, nini atafanya ambacho hajawahi fanya? Hana jipya zaidi ya kupiga pesa.
 
Back
Top Bottom