Lissu kama una lengo la kweli la kushinda Urais 2025, basi njia hii hapa...

Lissu kama una lengo la kweli la kushinda Urais 2025, basi njia hii hapa...

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Kwanza kabisa napenda kuwasalim wana jf wenzangu mliopo humu. Ama baada ya salam, niende sasa kwenye mada. Ndugu zang leo nimekuja na ushauri, au njia mbadala itakayomsaidia ndugu yetu Lisu na chama chake kuingia Ikulu kiulaini kabisa bila kutumia katiba mpya, tume huru, wala maandamano yoyote yasiokuwa na tija. Njia hizo ni...

(1) Kwanza arudi nchini kukijenga chama na kuendeleza mapambano ya hoja, na kusimamia sera za chama kikamilifu ili kutupa imani kuwa mpambanaji wetu kaamua kusimama na sisi katika nyakati zote za shida na raha kama vile kina mzee Nelson Mandela, Robert Mugabe, Hakainde Hichilema na wengine wa aina hiyo ambao waliweza kupata ushindi wa kuongoza nchi zao kupitia sera zao na mapambano yao ya ndani.

(2) Abadili aina ya siasa zake kutoka katika siasa za chuki, hasira na visasi, hadi katika siasa za upendo, umoja, mshikamano na uvumilivu. Haiwezekani ugomvi wake na hayati Magufuli, au ugomvi wa chama chake na CCM uufanye kuwa ugomvi wa taifa. Yan aufanye ni ugomvi wa watanzania wote dhidi yake au dhidi ya chama chake. Mpaka kufikia hatua ya kuwaomba wafadhili wetu watunyime kabisa misaada ya pesa ambazo huwa zinasaidia kuboresha elimu yetu kwa manufaa ya watoto wetu, au kusaidia kununua madawa kwa ajili ya afya zetu na za watoto wetu nk.. Kibaya zaidi alitaka tuwekewe na vikwazo, ili sisi wenzangu na mimi tusijaribu hata kupata fursa ya kufanya biashara zetu nje ya mipaka ya nchi yetu. Hii ilishangaza sana watanzania kuona mtu mwenye elimu kama Lisu anawezaje kufanya maamuzi ya kipuuzi, na kikatili kwa nchi yako na watanzania wenzako namna ile. Omba msamaha kwa hili, nina imani utasamehewa na kura utapewa.

(3) Ajaribu kuwa na misimamo thabiti isiyoyumbishwa na mtu yoyote, mwenye chochote. Sio leo atuambie hivi afu kesho abadilishe kauli yake atuambie vile, hiyo ni sawa na unafiki, uongo au uzushi. Lazima ajue kuwa siku zote ukweli hujenga, na uongo hubomoa.

(4) Awaombe msamaha wanachadema na watanzania waliomuamini, kwa kitendo chake cha kuwadanganya, na kuwachukulia kama wao ni maboya wasioweza kutumia hata kilo nzima ya akili zao kujua ukweli na uongo wa kauli zake, kama tunavyoona pichani.

(5) Mwisho namshauri ili aweze kujenga siasa zenye malengo, basi akamtafute ndugu Hakainde Hichilema amfunze siasa za kweli. Huu ndio ujumbe wangu kwake, najua hapa kuna wapambe wake watamfikishia. Unajua dunia ya sasa mtu anaweza asikupe chakula, lakini akakuonesha njia nzuri ya kukipata hicho chakula. Na kuna mtu anaweza akakupa chakula lakini akakataa kata kata kukuonesha njia ya kukipata hicho chakula.

Asanteni sana!
 
Kwanza kabisa napenda kuwasalim wana jf wenzangu mliopo humu. Ama baada ya salam, niende sasa kwenye mada. Ndugu zang leo nimekuja na ushauri, au njia mbadala itakayomsaidia ndugu yetu Lisu na chama chake kuingia Ikulu kiulaini kabisa bila kutumia katiba mpya, tume huru, wala maandamano yoyote yasiokuwa na tija. Njia hizo ni...
Mh lissu CHADEMA IPO IMARA SANA, tutakuomba kurejea tz mda mhafaka sio KWA sasa
 
Kwanza kabisa napenda kuwasalim wana jf wenzangu mliopo humu. Ama baada ya salam, niende sasa kwenye mada. Ndugu zang leo nimekuja na ushauri, au njia mbadala itakayomsaidia ndugu yetu Lisu na chama chake kuingia Ikulu kiulaini kabisa bila kutumia katiba mpya, tume huru, wala maandamano yoyote yasiokuwa na tija. Njia hizo ni...
Lisu hana pesa ,HH ana pesa
 
You don't know him at all. Lissu ndiye mpinzani wa kweli kwenye hii nchi. We will count a substantial number of decades before getting another Lissu. Trust me. Lissu anaweza kushinda urais 2025 landslidely. Watanzania niligundua wanampenda sana Lissu kuliko CHADEMA. I personally love him and not his party.
 
Mtu unatakaje kuwa rais wa Tz na hapo hapo hutaki kuishi Tz, yule mliokuwa mnamuogopa ameshakufa sasa mbona hamrudi nyumbani.?
Kwani Mbowe sasa hivi amebambikiziwa kesi na huyo aliyekufa? Kwa sasa dola haiko tayari kuona cdm inafanya siasa hapa nchini maana itaidondosha ccm. Sasa unataka aje wakati iko wazi kuwa hamna uwezo tena wa kufanya siasa za hoja zaidi ya kubambikizia wapinzani wa ukweli kesi?
 
Kutokana na hy Kauli yako bc hata ccm watasema 'tunaitaka katiba mpya lakini sio kwa sasa'
Ccm wasiotaka kusikia katiba mpya hawazidi watu mia,

Yana lengo lenu ni kutaka top leader wa Chadema mnawaweka ndani KWA kesi zenu za UGAIDI? Ngoja KWANZA tumalize la Mwenyekiti , mh Lissu atakuja tokana na mpangilio wa Chama , na KWA mda mhafaka
 
Kwani Mbowe sasa hivi amebambikiziwa kesi na huyo aliyekufa? Kwa sasa dola haiko tayari kuona cdm inafanya siasa hapa nchini maana itaidondosha ccm. Sasa unataka aje wakati iko wazi kuwa hamna uwezo tena wa kufanya siasa za hoja zaidi ya kubambikizia wapinzani wa ukweli kesi?
Chadema mlisema nchi inatakiwa impate dikteta ili isonge mbele, akaja Magufuli mkasema amezidi 😂😂😂 Bila shaka huyu mama ndio size yenu
 
You don't know him at all. Lissu ndiye mpinzani wa kweli kwenye hii nchi. We will count a substantial number of decades before getting another Lissu. Trust me. Lissu anaweza kushinda urais 2025 landslidely. Watanzania niligundua wanampenda sana Lissu kuliko CHADEMA. I personally love him and not his party.

..mimi nilianza kumsikia Tundu Lissu miaka ya 90 wakati akifanya harakati za kutetea wananchi wa RUFIJI DELTA ambapo serikali ilitaka kuliuza eneo hilo kwa muwekezaji. Tundu Lissu akiwa kijana mdogo aliyemaliza masomo ya sheria chuo kikuu akapambana mpaka akaishinda serikali na kilichobakia ni historia.
 
Ccm wasiotaka kusikia katiba mpya hawazidi watu mia,

Yana lengo lenu ni kutaka top leader wa Chadema mnawaweka ndani KWA kesi zenu za UGAIDI? Ngoja KWANZA tumalize la Mwenyekiti , mh Lissu atakuja tokana na mpangilio wa Chama , na KWA mda mhafaka
Na kwa kuwa mwenye uwezo wa kuiruhusu katiba ni rais bc nae amesema msubiri muda muafaka
 
Chadema mlisema nchi inatakiwa impate dikteta ili isonge mbele, akaja Magufuli mkasema amezidi 😂😂😂 Bila shaka huyu mama ndio size yenu

..hawakumaanisha "dikteta" anayedhulumu wapinzani.

..walimaanisha kiongozi mkali atakayewadhibiti wazembe na wabadhirifu waliokuwa serikalini.

..kwa bahati mbaya alipatikana dikteta mbadhirifu wa fedha za umma, na mkatili kwa vyama vya upinzani.
 
You don't know him at all. Lissu ndiye mpinzani wa kweli kwenye hii nchi. We will count a substantial number of decades before getting another Lissu. Trust me. Lissu anaweza kushinda urais 2025 landslidely. Watanzania niligundua wanampenda sana Lissu kuliko CHADEMA. I personally love him and not his party.
true
mmoja wapo mimi si mwanachama wa chadema sina chama sitaki kuwa na chama chochote cha siasaTz

but TAL nilimpa kura yangu oct 28.2020
japo nilijua hawazi kushinda hilo alilisema mwenyew kufunga kampeni zake kawe siku ya oct 27
 
Uzeni hoja za kueleweka ili wananchi wawaelewe, wananchi wakiwaelewa CCM hata iibe Kura zitapelea tu.

..Wapinzani wanaweza kuwa na sera nzuri lakini kukiwa na Amiri Jeshi mkuu toka CCM mwenye UJASIRI kama wa Magufuli ni kazi bure.

..Hivi unafahamu Tume ya Uchaguzi haijawahi kuengua wagombea wengi wa upinzani kama ilivyotokea ktk uchaguzi wa 2020?

..Pia hakuna kipindi cha uchaguzi ambapo vyombo vya habari vilizuiliwa kutangaza kampeni za wapinzani kama mwaka 2020.

..Magufuli alikuwa na uwezo wa kumshinda Tundu Lissu, lakini sijui ni kwanini akaamua kuuvuruga uchaguzi kwa kiwango kile.
 
Back
Top Bottom