Lissu kama una lengo la kweli la kushinda Urais 2025, basi njia hii hapa...

..hawakumaanisha "dikteta" anayedhulumu wapinzani.

..walimaanisha kiongozi mkali atakayewadhibiti wazembe na wabadhirifu waliokuwa serikalini.

..kwa bahati mbaya alipatikana dikteta mbadhirifu wa fedha za umma, na mkatili kwa vyama vya upinzani.
Wakati mnamsifia huyu mama na sasa hv mnapompinga ilikuwaje.?
 
Bc usingesafiri kwa barabara mana zilijengwa ndani ya wizara yake

..wako mawaziri wengine wa ujenzi na miundombinu.

..kuna wakati magufuli alikuwa wizara ya uvuvi, na wizara ya ardhi.

..mawaziri wengine wa ujenzi ni anna abdalah, shukuru kawambwa, andrew chenge, na basil mramba.
 
Ndo maana nimesema bado Sera za upinzani hazijawaingia wananchi vzr, siku zikiingia vzr hata hao polisi wanao tumiwa watapigia upinzani chapuo, namanisha upinzani hapa kwetu bado Sana.
 
Wakati mnamsifia huyu mama na sasa hv mnapompinga ilikuwaje.?

..Rais SSH alianza vizuri, na kulikuwa na matumaini.

..katika mazingira hayo ilikuwa sahihi kumsifia na kumtia moyo.

..ila sasa hivi anaonekana kuwa amekengeuka, hivyo ni sahihi kabisa kumlaumu na kumpinga.

..Nadhani Watz tunakosea kuamini kwamba tunatakiwa tuwe na msimamo mmoja kuhusu siasa wakati wote.
 
..ila sasa hivi anaonekana kuwa amekengeuka, hivyo ni sahihi kabisa kumlaumu na kumpinga.
Nmeipenda hy kauli, bc mtambue kuwa mbowe, lissu na wengine wa chadema nao pia wanaweza kukengeuka wakipata madaraka hvy msiwaone wao ndio wana haki kuliko wengine.
 
Ndo maana nimesema bado Sera za upinzani hazijawaingia wananchi vzr, siku zikiingia vzr hata hao polisi wanao tumiwa watapigia upinzani chapuo, namanisha upinzani hapa kwetu bado Sana.

..Kunatakiwa kuwe na sera nzuri, na mazingira yanayowezesha wapinzani kutangazwa, ikiwa wameshinda.

..Sheria zetu za sasa hivi zinawalinda viongozi wanaoharibu uchaguzi na kudhulumu wapinzani.
 
Nmeipenda hy kauli, bc mtambue kuwa mbowe, lissu na wengine wa chadema nao pia wanaweza kukengeuka wakipata madaraka hvy msiwaone wao ndio wana haki kuliko wengine.

..Moja ya ahadi za Chadema wakati wa kampeni za 2020 ilikuwa ni kuondoa kipengele cha katiba kinachosema Raisi hatashitakiwa kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.

..Kwa hiyo, wapinzani wanaelewa kwamba madaraka hulevya, hivyo ni vizuri kukawa na sheria inayowa-discourage viongozi wetu kutumia madaraka vibaya.

..Labda nikupe mfano. Hivi ukimwambia mwanafunzi kwamba hata akiiba mtihani hatapewa adhabu unategemea mwanafunzi huyo atajisomea kweli? Vivyo hivyo, kwa Raisi, na viongozi wengine wakuu, ukiwaahidi kwamba hawatashtakiwa, basi ujue watayatumia madaraka yao vibaya.
 
Ndo maana nimesema bado Sera za upinzani hazijawaingia wananchi vzr, siku zikiingia vzr hata hao polisi wanao tumiwa watapigia upinzani chapuo, namanisha upinzani hapa kwetu bado Sana.

Aaa wapi, yaani unadhani hatujui uhalisia? Au unataka mpaka yatokee machafuko ndio ujue watu wameichoka hiyo ccm? Hii kauli yako ni kama unataka kuhalalisha machafuko kuwa ndio dalili kuwa watu wamechoka. Ukishaona box la kura haliheshimiwi, hiyo ni dalili tosha kuwa chama kilichopo madarakani kimepoteza ushawishi.
 
Ok ila lissu hawezi wala hajui siasa. Anatumia uanasheria kwenye siasa halafu anajiona anajua siasa. Wanasheria wengi wanatafuta tu ushindi wa kesi sio haki. Wala sheria na haki sio kitu hicho hicho. Wanasheria wanaweza kuuza na kununua haki kwa wateja wao. Siasa haiko hivyo inataka mtetezi wa haki.
Ndio maana lissu ni kibaraka wa ubeberu.
 

..Tatizo la Lissu ni mwanaharakati zaidi kuliko mwanasheria, au mwanasiasa.

..Lissu anafuata zaidi HAKI kuliko kitu kingine chochote kile, na tabia hiyo ndio imejengea maadui ktk siasa.

..Na msimamo mkali wa Tundu Lissu kuhusu masuala ya HAKI umepelekea baadhi ya watu kumuona ni MKOROFI, na wengine kama IGP Sirro wanamuona MJEURI.
 
Labda aende ACT sawa maana mbowe kasema hapeleki timu uwanjani hadi kuwe na katiba mpya.
 
Tatizo lenu chadema mnadhani viongozi wenu wako sahihi wakati wote, huwezi kujua huko kwenye madaraka kuna nini mpaka ufike ndo utajishangaa ww mwenyewe unabadilisha msimamo
 
Tatizo lenu chadema mnadhani viongozi wenu wako sahihi wakati wote, huwezi kujua huko kwenye madaraka kuna nini mpaka ufike ndo utajishangaa ww mwenyewe unabadilisha msimamo

..Hapo nadhani umetuonea.

..Chadema wanapendekeza kipengele kinachowalinda viongozi wakuu wasishitakiwe kiondolewe.

..Msimamo huo unaonyesha kwamba Chadema wanaamini viongozi yeyote anaweza kufanya makosa, na wanataka akifanya makosa awajibishwe.

..Labda nikuulize mwana-CCM. Kwanini unaunga mkono kipengele cha katiba kinachozuia viongozi kushtakiwa ikiwa wamefanya makosa, madudu, au mauza-uza?
 
Dada dudumizi09 . Ushauri wako no. 4 haufai na hata zingine zina mushkel. TAL hakuwahi kuwa mtoro wa nchi hii mpaka mlipodhamiria kumuua. Na wenye dhamana na ulinzi & upelelezi wa kesi yake. Wanailemaza maksudically . Waliodhamiria kumuua wengine bado wanayo mamlaka na hawakuwajibishwa. Atarudi Je?!. Tofautisha wakati wa uchaguzi alikuwa akilindwa na Tiss. Leo hana ulinzi mdomoni mwa mamba wenye kiu na damu yake .

Ccm inaweza kushindwa hata na nld kama tu tume itakuwa huru.
 
Na kwa kuwa mwenye uwezo wa kuiruhusu katiba ni rais bc nae amesema msubiri muda muafaka
Mda wa kubembeleza umepitwa na wakati ,ila jua katiba inakuja hakuna wa KUZUIA asema bwana, Mbowe atatoka iwe mvua au jua, ilisha kuwa , labda Kama mungu anitumiaye amesinzia, kitu ambacho hakiwezi kua
 
1. kesi zinazomsubiri mahakamani ata-deal nazo vipi?

2. jamaa waliotaka kumuua atajilinda vipi wasimdhuru tena?
Ataomba ulinzi serikalini, na serikali itamlinda bila wasi wasi. Kuhusu ishu ya case hayo ni mambo ya mahakama, kama kesi inayomkabili haina ushahidi basi atashinda tu wala haina haja ya kuukwepa mkono wa sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…