Lissu kuhusu mustakabali wako CDM, jifunze Kwa JK kuliko kufuata ya Lowwassa.

Lissu kuhusu mustakabali wako CDM, jifunze Kwa JK kuliko kufuata ya Lowwassa.

Ni kweli bila Mbowe Lisu angepata wapi chama cha kumpa ubunge na umaarufu,hao watu wakae chini watulie na washauriwe kushambulia sufuria iliyokupikia chakula ni makosa makubwa.
Mbowe pia aliyafanya hayo chini ya mwamvuli imara uitwao CHADEMA.

Nje ya CHADEMA, Mbowe na Lissu ni watu WADOGO tena wanapita.

Muhimu chama kipite salama katika Uchaguzi huu.
 
Hakuna mahali Lissu amesema akishindwa atahama kwenda chama kingine.
Hata Msigwa alisema hivyo hivyo hatohama baada ya kukata rufaa,

Lissu pia ameanza Yale Yale kwamba Kuna viashiria vya kuibiwa kura.

Ndipo ushauri unaenda kwake, afumbue macho yote yawe wazi aone sawasawa.
 
Hellow!!

Kuna wajinga humu wanakudanganya kuwa Eti ikitokea umeshindwa uenyekiti Kwa namna yoyote Ile kwamba ukiondoka CHADEMA utasomba umati wa wanachama wengi na kukiua CHADEMA!

Hii Si Kweli, ni kujillisha upepo, wewe ni mtu mmoja, CHADEMA ni Taasisi.

Ni vyema ukajifunza Kwa Jakaya Kikwete aliyekataliwa akiwa ni maarufu na kijana kumzidi Benjamin Mkapa, angechukua uamuzi wa kuhama chama, asingefikia ndoto zake za kuwa Rais wa Nchi.

Kamwe usichukue mkondo wa Lowwassa ,aliaminishwa kuwa akihama, ataiua CCM, Hilo halikutokea, na hakuweza kuwa Rais, angevumilia, angekuwa Rais hata Kwa miaka miwili tu baada ya Magufuli.

Ushauri Kwa Lissu: Matokeo yoyote kutokana na mchakato wa uchaguzi yapokee, ukishinda hewalaaaa, ukishindwa Kaa tulia subiri wakati wako ufike.

Ushauri Kwa Mbowe: Bado una muda wa kujiondoa kwenye kinyanganyiro Ili ukabidhi chama kwa Heshima.

Mungu ibariki CHADEMA,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni!!
Shida sio TAL kuhama au kubaki shida ni wananchi maana washaelewa michezo ya vyama vya upinzani nchini.
 
Back
Top Bottom